-->

NINI CHA KUFANYA KAMA MUME.MPENZI WAKO HAJAMSAHAU X WAKE?

MAPENZI – Page 61 – My Blog
Kua makini sana na mwanaume ambaye ametoka kuachwa na mwanamke, hapa naomba mnielewe, mwanaume aliyetoka kuachwa na si maanishi kuachana au kumuacha. Huyu ni yule ambaye alikua anampenda mwanamke sana, lakini ndugu wa mwanamke wakamkataa na kumuambia hawezi kumuoa labda mwanamke akachukuliwa na mwanaume mwingine. Lakini pia huyu ni yule ambaye mwanamke kamuacha na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine au kamuacha na kwenda kuwa na mwanaume mwingine.
Pamoja na kuachwa au kufanyiwa kitu kibaya na mwanamke lakini akaonekana bado anampenda, labda yeye ndiyo anaomba misamaha isiyoeleweka na wakati unakutana naye unamuona kabisa yuko kwenye msongo wa mawazo. Najua unamuona na anakuambia kuwa anataka kumsamahau huyo mwanamke, au hasemi kuwa anataka kumsahau lakini maneno yake kila saaa ni kumzungumzia huyo mwanamke, inaweza kuwa ni kwa ubaya, labda kila kosa anakuambia uko kama flani, wanawake si waamini walishanitenda, au kila unachofanya anakulinganisha na huyo.
Pia inaweza ni kuwa kwa kumtukana huyo mwanamke wake, uko naye lakini mazungumzo ni X wake, kumtukana na kusema namna ambavyo hawamaini wanwake kwaajili yake. Lakini kaachwa na unajua kaachwa ila bado anamfollow katika mitandao ya kijamii, bado anampigia simu huyo mwanamke au huyo mwanamke akipiga au akiwa na shida basi hukimbilia katika kumsaidia. Kama una mwanaume wa namna hiyo basi kuwa makini nayue na wakati mwingine kuwa mbali naye, huyo anakutumia kumsamahau mtu wake na ipo siku atakudamp tu.
Mwanaume kama huyo hata akikuoa utateseka tu kwani mwisho wa siku huyo X wake akipiga tu simu mwanaume huyo atarudiana naye na utakua namba mbili. Najua kuna wengine ambao mshaingia kwenye ndoa au mmependa sana wanaume wa namna hii, ushauri wangu nikuwa acha kushindana na huyo X wake, acha kumzungumzia ahata kama yeye anamzungumzia, hata kama naakukera acha kumlalamikia, jinsi unavyomlalamikia kuna mambo mawili yanatokea.
Jambo la kwanza nikuwa unavyomtajataja inafanya kuwa ngumu mwanaume wako kumsahau kwakua nyie hamna muda wenu wawili, kuzungumzia mambo yenu mnazungumzia tu huyo mwanamke. Kwamba mume wako ukiwa haupo anchata naya, anamuwaza yeye na labda anamzungumzia yeye, sasa na wewe badala uzungumzie mambo yenu unamzungumzia huyo huyo, hatoki midomoni na wote mnakua kama mnamuabudu. Jambo la pili nikuwa unakua na kisirani na unaanza kumkera mwanaume wako.
Nikweli yehe ndiyo anasababisha lakini kama kila siku unalalamikia kitu kilekile basi inaboa, si uondoke au kama huwezi kuondoka basi nyamaza. Lakini kama kila siku umenuna, unalalamika, akipiga simu asubuhi basi mpaka jioni umenuna ni kama unamuambia mwanaume kuwa “Mimi nina kisirani ni bora uendelee na huyo!” Najua unaumia ila mtoe mdomoni mwako, unanapomtaja taja ni kama unamuogopa, ni kama unajiona wewe hutoshi na unatishiwa na simu zake, unatishiwa na yeye kuongea na mume wako na vitu kama hivyo.
Wakati mwingine mwanaume wako anaweza kuwa hatembei naye, ni kwakua tu walishazoena na anashindwa kumsahau kwakua alikua rafiki. Sasa badala ya wewe kujenga urafiki naye ili asimkumbuke sana basi wewe kunakua kisirani unamuacha anakua mpweke anamkumbuka na kutamani kuchata naye. Sijui kama mnanielewa ila iko hivi kama mwanaume wako hajamsahau X wake na umeamua kubaki kupambania Kombe basi funga mdomo na jifanye kama huyo X humuoni, acha kumtajataja na jifanye kana kwamba hakutishi na humuogopi.
Kitu kingine ni kwamba wanawake wana kitu kimoja, kama anatembea na bwana wakoa u yuko karibu na bwana wako ukamuonyesha kuwa anakutisha, ukamuonyesha kuwa anakunyima amani basi ndiyo huzidi kufanya manjonjo. Yaani kama akipiga simu unanuna na kutukana ndiyo kwanza anapiga na mechi anaweza kumpa tu ili kukukomoa, hivyoa chana naye, kuwa na furaha wala wasikuumize, hata kama unaumia basi usiwaonyeshe kama unaumia. Jifunze kuw ana furaha yako na kama hujui cha kufanya
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU