-->

MAKOSA YA MWANAUME YANAYOSABABISHA MKE AMSALITI


Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:
1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI
Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya... atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla...
Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia... Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume... mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.
2. UKOSEFU WA MAHABBA
Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa... Mwanamke anahitaji kupendwa... mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono... ukimpa ngono tu basi, anaridhika... mwanamke anahitaji kuengaengwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu... mwanamke anataka hivyo.. anataka aone kama anapendwa... anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake... ampe lugha ya kimajnun... mwanamke anamtaka Majnun... sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu... mnanipata hapo?
3. USALITI WA MUME
Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti... Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa... Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi...
4. KUTOJIAMINI
Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini... iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa... Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.
Tofauti ya usaliti wa mwanaume kwa mke wake na usaliti wa mke kwa mume wake, mwanaume anaweza akamsaliti mke wake na bado akaendelea kumpenda mke wake. Na asilimia 88 ya wanaume wamekuwa wakiwasaliti wake zao na bado wakaendelea kuwapenda wake zao.
Hii ni tofauti kwa wanawake. Mwanamke akimsaliti mume wake, maana yake ni kwamba mwanamke huyo hana tena mapenzi na mume wake na ndio maana akaweza kumsaliti, kwakuwa wanawake si kawaida yao kuwasaliti waume zao.
Mwanamke si mrahisi kusaliti, lakini kuna mambo yakimkifu na vitendo vikauchosha moyo wake, mwanamke atakusaliti.
Mwanamke akikusaliti, jua tayari hakupendi tena. Lakini hii ni tofauti na wanaume walivyo, mwanaume anaweza akasaliti na bado akampenda mkewe kama kawaida, lakini mke akisaliti maana yake mapenzi yamekwsha kwako.
Share
Like Page
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU