-->

KUSHAWISHIKA KWA MWANAMKE NI ANGUKO LA IMANI YAKE KWA MWANAUME WAKE💯


Kwanza naomba nieleweke;
• HAKUNA MWANAMKE ASOKUWA NA MWANAUME NDANI YA MOYO WAKE IWE KWA TASWIRA AMA KWA UHALISIA😎
Kwa maana hiyo kila mwanamke anayempa nafasi Mwanaume tayari anakuwa na Mwanaume mwingine akilini mwake iwe anampenda ama hampendi lakini ni MWANAUME wake.
Moyo wa Mwanamke hubeba Mwanaume Mmoja tu na ukiona Mwanamke ana wanaume zaidi ya mmoja ujue ALIYEPENDWA AMESHINDWA KUKABILIANA NA JUKUMU LA KUULINDA MOYO WA MWANAMKE HUYO.
Nijuavyo mimi Mwanamke kushawishiwa na Mwanaume mwingine wakati anae mwingine ni wazi Mwanaume mwenyeji hajaweza kupambana na mahitaji ya Mwanamke huyo, Mara nyingi wanaume tuna imani kwamba;
• MWANAMKE AKISALITI NI TABIA ILA MIMI NASEMA MWANAMKE HUJIFUNZA TABIA NJEMA NYUMBANI KWAO NA TABIA MBAYA HUJIFUNZA KWA MWANAUME💯
Kwa sababu hiyo unapata jibu kwamba hakuna Mwanamke anapenda kuharibu UHUSIANO AMA NDOA aliyoingia Mwenyewe
Ila Mwanaume ndiye anaweza kumfanya Mwanamke akajiongeza namna ya kuishi na Mwanaume wake, na Mwanaume akija kugundua mara zote Jumba bovu humwangukia Mwanamke na kumpa alama mbaya kwamba ni tabia yake kumbe wewe Mwanaume ndo umempa MBINU mbadala Mwanamke😂😂
Mungu mwenyewe alisema;
• WANAUME MUISHI NA WAKE ZENU KWA AKILI.
Ujinga wetu Wanaume tunaamini kwamba WANAWAKE NI VIUMBE DHAIFU wallah tunajidanganya ndo maana Mwanamke akikuonyesha TRUE COLOUR yake tunajikuta kwenye maradhi ya BP na KISUKARI na kumbe chanzo cha hayo ni wewe kushindwa kukabiliana na MAHITAJI YA MWANAMKE WAKO.
Kinacho wapoteza Wanawake kwenye IMANI yao ya MAHUSIANO NA NDOA ZAO ni pindi Mwanamke anapokosa aliloamini kuwa atalipata kwa Mwanaume, na hapo ndipo akijitokeza Mwanaume mwingine akaongelea kilichokosekana kwa Mwenyeji wallah itakuwa rahisi kushawishika👀
Ndo maana ukiona Mwanamke anajiheshimu ujue hana linalopungua kwenye MAHUSIANO AMA NDOA yake, Hivyo Mwanaume ndo mwenye mamlaka ya KUMLINDA MWANAMKE WAKE NA MWANAUME WENGINE💯
Usipende kumshutumu Mwanamke kama hujatimiza mahitaji yake, Hawa watu bila kuwa na PACKAGE 🎁 YA UPENDO niamini huwezi kujitoa kwake nae atakuwa DHAIFU wanaume wenzio wakusaidie.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria 🔨
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU