-->

DALILI TANO KWAMBA MWANAUME ULIYEKUTANA NAYE NI TAPELI UNATAKIWA KUWA MAKINI!

KONA YA Mabinti - Posts | Facebook
Nawajua dada zangu, hasa nyie wastaarabu (mlozoea kuumizwa), mkishapenda, ukakutana na mwanaume anakujali basi unachanganyikiwa balaa. Tena kama ulishawahi kuumizwa au katika mahusiano yako umekua ni mtu wa kudharaulika, hujawahi kukutana na mtu anayejali kama huyo unachanganyikiwa sana, lakini mnalizwa sana na wengi wenu kwakua mnakuja kunilalamikia hembu niwape darasa kidogo.
Hapa labda nifafanue kitu kabla ya kuendele, si kila mwanaume wa namna hii ni tapeli, ila kama umekutana na mwanaume, hamjamaliza hata miezi mitatu ya mahusiano akakufanyia haya mambo, wewe utaona ni mapenzi lakini mimi nitaona kama ni utapeli, hasa kama katika haya mambo angalau matatu ndani ya miezi mitatu yashatokea, dada unahitaji kuamka.
(1) Anaanza Kwa Kukukopa; Hii ni dalili ya kwanza kabisa kuwa mwanaume uliyenaye sio kwamba tu ni tapeli bali ni tapeli wa kutupwa. Ashakuambia ana kazi nzuri na hata kukupeleka ofisini, amejisifia sana mara kwa mara. Lakini ghafla anapata katatizo flani, linaweza kuwa kubwa, labda kafiwa, kuna hela imepotea ofisini, Mama yake kaugua Ghafla na vitu kama hivyo, anakuambia nikopeshe labda laki mbili.
Hapo hata miezi mitatu nayeye hamna, halafu anakkukopa kipindi ambacho wewe una hela, labda kashahakikisha kuwa umelipwa mshahara, kama ni mwanafunzi boom limeingia au kama ulimuambia unacheza mchezo basi umepokea wewe. Yaani anakuja tu anakukopa na wewe ukiangalia unapesa na ushaanza kumpenda basi unaanza kujisikia vibaya kumnyima kwakua tatizo lenyewe ni la kweli na unaona hana raha kabisa.
Dada yangu huyo ni tapeli, kwanza ni kwasababu alishakuambia ana akazi nzuri na kujisifia. Pili mwanaume kamili anaogopa kuomba pesa kwa mwanamke, huona kama ni kujidhalilisha, hivyo atakopa kwa washikaji lakini si kwako tena mpenzi mpya. Hapana ukiona anakuja kukopa basi jua huyo anakulia timing, na ukikataa huwa anapunguza mawasiliano, anajifanya hana raha.
Mwingine mwizi zaidi ukimuambia huna utasikia anakuambia katika chanzo kilekile ambacho umepatia pesa, sijui si mna mchezo, si mshahara umetoka, sijui si umuambie Mama yako. Yaani anakuja kukupoka lakini anakuambia na sehemu ya kupata pesa. Dada yangu najua unampenda sana na utaniona muongo ila nakuomba akisha kuliza hembu nitafute niambie ulisoma hapa lakini hukuzinduka.
(2) Anajali Kupita Kiasi; Mwanaume hauna hata mwezi naye lakini anavyokujali mpaka unaona si ndiyo huyu. Labda hata hajatembea na wewe, lakini asubuhi atakupigia simu kukuuliza umeamkaje, mchana umekula, sijui nini na nini? Hatoi hela, narudia ishu ya hela hakupi yeye ni kukujali kwa kukupigia simu mara kumi kwa siku na kukukumbusha mambo ya maendeleo.
Yaani anajua mambo yako, anajua ratiba zako kiasi kwamba anaweza hata kukukumbusha kuvaa Pedi. Dada yangu kama hataki kukutapeli pesa basi jua kuwa anataka kutembea na wewe atimue na kama ashatembea na wewe na bado anajali sana usishangilie kihivyo atabadilika tu. Kuna wanaume ambao ni asili yao kujali lakini kama kukizidi mpaka unaona kama kero basi jua kuna tatizo sehemu flani!
Anaweza asiwe tapeli lakini akawa kimeo kuwa ana wivu na hana maisha yake binafsi hivyo anataka kucontrol maisha yako. Lakini unatakiwa kujiuliza hivi yeye hana kazi ya kufanya mpaka maisha yake yamenizunguka mimi tu, mbona muda wote ananihangaikia mimi yeye vipi, tena kama ndiyo akija na kukopa tena basi jua umeliwa.
(3) Ashakutambulisha Kwa Ndugu Zake; Mwezi wa kwanza wa pili utakuta kashakutambulisha kwa ndugu zake, watatu kashakupa simu uongee na Mama yake. Mambo yanaenda harakaharaka mpaka basi, dada yangu unachanganyikiwa, hujawahi kutambulishwa hata siku moja. Hembu kabla ya kuchanganyikiwa na kushangilia chunguza kidogo, kashatambulisha wangapi?
Je kweli anakupenda kiasi hivi miezi miwili mitatu kashakutambulisha, ana kasoro gani mpaka kipindi chote hicho hakua na mtu eti anasubiri uje basi akutambulishe. Usiingie kichwa kichwa, ukiona anakazania kukutambulisha hata kabla ya kujuana vizuri inawezekana ndiyo tabia yake, ndiyo aina yake ya kutongoza. Tena unakuta hata hajatembea na wewe anaanza habari za kutambulishana, amka acha kuingia kichwa kichwa.
(4) Anashinda Na Hata Kulala Kwako; Hataki uende kwake, anaweza kukuambia kuwa anaishi na wazazi wake au anakuambia anaishi na wadogo zake hivyo hawezi kukupeleka. Lakini kutwa kucha anashinda kwako na kuchezea rimoti utafikiri kalipia King’amuzi anakula na hata kulala kwako, yaani hamna hata miezi mitatu kashajifanya Baba mwenye nyumba.
Kuwa makini na mwanaume kama huyo, kwanza inawezekana kwake anaishi na mtu, mke au mchumba, lakini inawezekana ni mtu tu wa kulelewa hasa kama anashinda kwako lakini hata Kiberiti kikiisha hatoi au akitoa hela atalalamika mpaka basi. Huyo ni wa kulelewa na ukiacha kumlea anahamia kwingine yeye anaenda kwenye dau kubwa tu!
(5) Anataka Mshirikiane Katika Mambo Yake/Mfanye Kitu Cha Pamoja; Najua hapa ndiyo mnapofurahi, unakuta mwanamke mdada anajisifia ananipenda kashanipeleka kwenye miradi yake, hafanyi kitu bila kunishirikisha na mambo kama hayo. Yaani miezi mitatu tu ashakuambia anajenga, kashakuonyesha biashara zake, ashakuambia mipango yake yote na anakushirikisha katika baadhi ya maamuzi.
Si umetoka kwenye mahusiano na mwanaume ambaye alikua msiri sana hivyo unachanganyikiwa. Sasa mwanaume kama huyu akishaona umeingia kwenye laini utasikia anakuja kukukopa mmalizie nyumba, halafu alivyomjanza anakuambia “Tumalizie nyumba yetu” Yaani kila kitu anachofanya hata kwa pesa zake utasikia chakwetu, chetu! Anakushirikisha ujihisi ni sehemu ya umiliki!
Dada huyo kuna uwezekano mkubwa anataka kukupiga tu, tena kama una kazi au ndugu zako wana vihela amka kabisa kwani kuna wakati ukishazoea, ukishaanza kusimamia mafundi, akakupeleka na kuona au hata kukuambia mchague ramani ya nyumba basi atakuambia umkopee, kuna hela imepungua ya mafundi, kuna sijui nini na nini?
Ndugu yangu akishaanza hivyo kwakua ushajiona sehemu ya mali, ushajiozesha tena kama umetambulishwa basi unajiona mkeee unamchukulia na mkopo jua ndiyo umepigwa dada yangu. Najua kama uko katika hali hii hutaki kuamini kwani anakufanya ujisikie kama hiyo nyumba, hilo gari ni lako. Anakutambulisha mpaka kwa mafundi na wakati mwingine anakuambia wapelekee na pesa wewe unavimbaa unapendwa ila unaelekea kutapeliwa.
(6) Ndugu Zake Wanakuaomba Hela; Huyu sio kwamba yeye ni tapeli bali familia nzima ni matapeli. Kwanza alishaanza kukukopa, pili kakutambulisha kwao hata mpaka kwa Mama yake, wakakusifia na ana yule Dada yake ambaye kila siku anakupigia simu, Mama mkwe ndiyo ashakufanya shoga yake lakini mwisho wa siku wanakuomba hela. Yaani hapo si mwanaume tu, lakini wadogo zake ni wifiii, Mama mkwe ni mkwe wangu.
Wanakulilia shida na kukuomba hela na kama huna wananuna kabisa, ndugu yangu wewe umeingia choo cha mapopobawa, umeliwa. Kwanza hauko peke yako uliyetambulishwa, pili wala hawakupendi bali walisikia una kazi hivyo wanahitaji pesa zako na tatu hata hao wengine waliotambulishwa nao wanafanyiwa hivyo hivyo. Kwa maana hiyo kabla ya kushangilia hembu kuwa makini kwani ukiacha kutoa pesa unaachwa.
Mwisho hembu kabla ya kupaniki na kufanya uamuzi wowote chunguza, hembu acha kumpa hela akikuomba, kama ni ndugu acha kuwapa hela, lakini akitaka mfanye mambo ya pamoja muambie huna hela na fanya mambo yako kivyako. Acha kupaniki kwa kuonyeshwa upendo wa miaka kumi ndani ya mwezi mmoja bila kujua kuwa kuna wengine walikuepo wakaonyeshwa hivyo na wakaachwa tena kwa kulizwa.
Wakwako anaweza kuwa ni wale wachache ambao wanapenda kweli, labda yeye hana mpango wa kukutapeli. Ila acha kuwa mjinga, kama umesoma hapa na uko katika hali hii chunguza, chunguza na chunguza. Acha kuleta upofu wa kupenda, na kusema flani hawezi kunifanyia hivyo, kumbuka kazi ya kwanza ya mtu tapeli ni kukufanya kumuamini, huwezi kutapeliwa na mtu ambaye haaminini!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU