-->

ACHA KUVUMILIA MAUMIVU UNAYOYAPATA KWA KIGEZO CHA MAPENZI.

Acha kutumia kigezo cha MAPENZI kuvumilia maumivu anayokupa. Kama mpenzi wako hakujali, kila leo ni maumivu na huku HAUJAFUNGA nae NDOA jiongeze na achana na huyo haramia kabla hujachelewa.
Unawezaje kuvumilia Abusive relationship na mtu ambae hata kwenu hatambuliki? Naweza nikakuhakikishia kuna baadhi ya watu wanahangaika na ndoa zao huku wakitamani kuchomoka kwa sababu walikuwa na mahusiano ya hovyo kabla ya ndoa na wakadhani ndoa ndio itakuja kumbadilisha mtu na kuwa katika mstari ulionyoka.
Ndoa sio chuo cha mafunzo. Ndoa haimbadilishi mtu, ndoa huibua tabia halisi za mtu. Mahusiano kabla ya ndoa ndio chuo cha Mafunzo, ukimuona mwenzio haelewi somo, leave him/her for good.. Ondoa hiyo OIL chafu, subiri OIL safi.
"
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU