-->

WANAUME TWENDENI SAWA HAPA.

Image result for mapenzi wakubwa

1. Usijisahau katika mahusiano ukawa comfortable kiasi kwamba zile mbwembwe zote za kipindi unamtongoza unazipotezea. Mwanaume smart haachi kumfanya mwanamke wake ampende zaidi. Mwanaume anaemfanya mwanamke wake ampende zaidi mahusiano yao hudumu mpaka uchweo.

 2. Usisahau kufanya tabasamu kuwa kipaumbele cha mwanamke wako. Ole wao wanaume wanaowanyima tabasamu wapenzi wao wakaacha wanaume wengine ndio wawape tabasamu wanawake zao. Nawaambieni mpo kwenye matatizo makubwa. 

3. Yatunze maneno yako kwa uaminifu mkubwa. Uaminifu ni msingi imara wa mahusiano yenye afya. Mwanaume wa kweli hakimbii majukumu. 

4. Usiwe mkoloni katika mahusiano. Kuna haki ya kusikiliza na kusikilizwa (natural justice). Kuwa mwanaume, admit kama umekosea. Kuwa na ujasiri wa kurekebisha pale ulipokosea 

5. Usimfanye mwanamke wako aone kama anashindana na muda wako, mfanye ajisikie na yeye anathamani katika muda wako. Sio sababu ya kuwa na muda au laah! bali ni jitihada ya wewe kutengeneza muda wa pamoja. 

6. Usiwe mvivu. Kuna mtu mwingine pembeni ambaye anatamani kuwa na huyo mwanamke. Linda tunu yako kwa upendo, furaha na amani nae. Usiwe mvivu kumfurahisha, kumlinda, kumridhisha na kumsifia. Pombe na nyama choma zisije zikakuponza. 

7. Usihukumu. Kila mmoja anafanya makosa na anajifunza kwayo. Usihukumu makosa yake wala past yake. Na kitu cha muhimu usimhukumu kwa vile unafikiri tofauti na yeye. Binadamu tunatofautiana sana. Enjoy kuwa nae kwa jinsi alivyo. Usilazimishe awe kama wewe.

 8. Usi assume kwamba anajua kama unamjali, mwonyeshe kweli unajali. Mpe support katika shughuli zake i.e masomo, biashara, kilimo, etc. Mtumie sms, msikilize, msifie, muonyeshe mapenzi kwa maneno na vitendo na uwe mbunifu. 

9. Usiwe mwanaume jina, acha tabia ya kuzira na kususa ,onyesha kuwa wewe ni mtu wa majukumu na ni kichwa katika mahusiano, jenga mahusiano kwa busara zaidi na sio kwa ki imla (dictatorship). Maumuzi yako ya kijinga kijinga yatakutokea puani. 

10. Usikate tamaa kirahisi, najua maisha ni magumu ila mwanaume wa kweli anapotaka kitu, atafanya kila awezalo kukipata, unasubiri nini? fanya hivyo sasa.
Share:

Related Posts:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © 2025 UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU