Kuna aina nyingi za ushindani na kila maahindano yana mshindi mmoja, Usiombe ushindanie MAPENZI halafu wewe ndo ushindwe kwa ufupi inauma sana... Ilikuwa ndoa takribani ya miaka minne, Mume aliishi Mwanza na Mke aliishi Morogoro, Mapenzi ni IMANI japo penzi la mbali lina TAFAKALI nyingi lakini haina maana kuwa usimuamini mwenzi wako, Walipendana sana na kila mmoja aliwekeza IMANI kwa mwenzie, Alikuwa Mke ndiye aliyependa zaidi kumtembelea Mumewe huko Mwanza, Siku mbaya huonyesha asubuhi wakati wa Mapambazuko! Mke alijiandaa kwa safari bila kutoa taarifa kwa mumewe, Safari ni hatua hatimaye Harieth akafika mwanza na kuelekea huko anakoishi Mumewe, Niligonga mlango na kuulizwa na sauti ya mwanamke WEWE NANI? Kwanza nilipata Hofu lakini nikajisemea hapa ni kwangu, Ni Mimi hapa... alikuwa Harieth ambaye alijibu kwa kujiamini kabisa, Mlango ulifunguliwa na Mwanamke ambaye sikuwahi kumfahamu wala kumuona akaniuliza TUKUSAIDIE NINI? Sikuwa Nina mashaka ila sasa nikahisi kuwa na mashaka maana maswali yale sikuyaelewa kwa mara moja, Nimekuja kumuona MUME wangu Steve, Jibu langu lilimsemesha mume wangu na akanikaribisha nikaingia ndani, Nikamuona Mume wangu amebeba mtoto nikamsogelea na kumuuliza mtoto wa nani huyu? Sauti ya mwanamke ikasikika akisema MTOTO WAKE HUYO! Nisiye amini wala kusadiki kile nimekisikia nikarudia tena kumuuliza Mume wangu, Steve Huyu mtoto wa nani? Si ushaambiwa kuwa mtoto ni wangu sasa wewe unadadisi nini? Alikuwa Steve mume wangu alijibu huku akiwa amejawa Hofu nyingi, Ooooh ni jambo zuri Una maana uko na Mimi na kumbe una mwanamke mwingine na mpaka mmezaa? Sikia Harieth Huyu ni mke wangu kama wewe hivyo wewe ni mkubwa yeye mdogo na kama Kuna mmoja ataona hawezi Mbio hizi Basi akae pembeni, yalikuwa maneno machache lakini yalibeba maana pana, Nilisikia kama roho inataka kutoka tena nikiona wazi Nipo mbele ya shimo lakini nilijipa moyo na kuziimba ZABURI ya 23:5 "WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU, UMENIPAKA MAFUTA KICHWANI PANGU NA KIKOMBE CHANGU CHAFURIKA" Nikajisikia mwenye amani tele na nikapata ujasili wa kumwambia Mume wangu kuwa nimekusikia baba na nimekuelewa ila Nina swali ninaomba kujuwa STEVE BADO UNAHISI UNANIPENDA? Harieth nimekujibu kuwa ninyi ni wake zangu hivyo Sina kinyume cha hapo, Majibu ya Steve yalinipa hakika kuwa AMEJIPANGA... usiku ushaingia ikabidi niulize mahala pa kulala ndipo mume wangu akasema TUTALALA CHUMBA KIMOJA Kwani ninyi ni wake zangu, Majibu ya Steve yalizidi kuubomoa moyo wangu lakini Nikamuomba Mungu anipe moyo wa ujasili kukabiliana na hili Kwani nilikumbuka kitabu cha YOSHUA 1:9 "JE SI MIMI NILIYEKUAMURU UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA, USIOGOPE WALA USIFADHAIKE KWAKUWA BWANA MUNGU WAKO YU PAMOJA NAWE KILA UENDAKO" Nikajitutumua kuaga usiku ule Kwani niliona sintolala pale kwa hali ile niloiona, Steve amejaa kiburi kiasi haoni shida kujibu apendavyo, Safari njema Harieth! Majibu hayo yalinipa mwanga kuwa sihitajiki japo moyo bado ukiteseka juu ya Mume wangu Kwani nampenda bado, Nikabeba mkoba wangu ili nitoke ghafla simu ya mkononi ikaita na kuipokea japo sikuijuwa namba ile, Hallooooo... Ilikuwa sauti ya mwanaume nami nikaitika Hallooooo ndipo upande wa pili ukajitambulisha NAITWA FRANK NAONGEA NA HARIETH? Ndiyo Frank Habari za siku? Nilijibu huku nikisikia amani moyoni Kwani kwa upendo nilimpenda sana Frank lakini wazazi wangu hawakumpenda na ndipo walinichagulia Steve, Mume wangu akiwa ananiangalia na akiwa makini kufuatilia maongezi hayo, Moyoni nikajisemea Frank amefikwa na nini leo ananipigia? Kabla sijapata majibu Frank akasikika akisema HARIETH WEWE NI MWANAMKE WA HISIA ZANGU NA PIA WEWE NI MWANAMKE WA MAISHA YANGU NAOMBA KUKUONA KESHO tafadhali uniweke katika ratiba zako, Nikawa natoka sasa nyumbani kwa Steve ili nikatafute mahala pa kulala ghafla Steve akaniita na kuniuliza naongea na nani? Amaa kweli Mkuki mchome Simba bin adam anayo maumivu, Naongea na Frank yule alikuwa Boy friend wangu! Majibu yale yalimuumiza sana Steve kiasi alisimama na kunifuata nyuma, Nilijuwa tu utakuwa na mwanaume Kwani siku hizi una kiburi sana, Maneno yake Steve yalinipa tabasamu nisijue hata la kusema... Nikapiga hatua mbele ghafla Steve akanishika mkono akiwa amejaa wivu na kutaka kunipokonya simu, Sikiza Steve imekuwa kama MUUJIZA Mimi kupata simu ya Frank na kwanza sijajuwa anataka nini Kwani tangu niwe nawe hakuwahi nitafuta wala sijamuona na simu kapiga nikiwa nawe ila Nimeona kama kanipa ahueni ya moyo, Nipe simu niongee nae asikusumbue tena, Steve akiendelea kutaka kuongea na Frank, HAPANA STEVE SIWEZI KABISAA KUFANYA JAMBO HILO! Na kwanza wewe tayari unapo pa kukimbilia ukiona nakusumbuwa JE MIMI AMBAYE TANGU UNIOE SIHAWAHI FIKIRIA KUWA NA MWANAUME MWINGINE NAKIMBILIA WAPI? Ni kama Steve ananichelewesha nikaondoka na kumuacha kwake, Maswali mengi kichwani juu ya hatma ya ndoa yangu pamoja na ujio wa Frank, Ulikuwa wakati muafaka wa kuushibisha amani moyo wangu ilibidi nirudiane na Frank na niliona jinsi ambavyo Frank alikuja wakati ambao nilihitaji mtu kama yeye, Nilichochifunza juu ya mahusiano na ndoa kwa ujumla WANAUME NI WABINAFSI SANA WANAPENDA WASIUMIZWE WAKATI WAO NI WAANZILISHI WA KUUMIZA.
USIPENDE USHINDANI KWA MAPENZI