-->

USIOGOPE KUANZA😎 Tambua hata 0 ni namba kwa sababu iko nyuma ya 🔢

Image may contain: one or more people, people standing, outdoor and nature
Unapokuwa Uko kwenye 0 maana yake unatakiwa kufungua mwendelezo wa namba, Ndo maana nasema MUOGA WA KUANZA ni ngumu sana kufanikiwa Kwani ALIPO ANAAMINI PANAMFAA AMA KUMTOSHA japo anatamani kuwasogelea ambao wanamzidi nafasi aliyopo, Dhiki haitesi NAFSI japo inahangaisha MOYO
Lakini kinachoitesa NAFSI ni MAPENZI kwa sababu Mapenzi yana nguvu kwenye AKILI, MOYO wa bin adam hazina yake ni NAFSI ndo maana VITA ILIYOKO NDANI JUU YA MAPENZI NI KALI KULIKO VITA YOYOTE ILE KWENYE MWILI WA BIN ADAM.
Ni rahisi kuanguka kwenye MAISHA mtu akaikubari hali aliyonayo, Lakini ni NGUMU mno kwa Mtu kukubari kuipoteza AMANI YA NAFSI YAKE yaani kumkosa Mtu ambaye UNAMPENDA ni maradhi ya siri, Lakini ikiwa umepambana kuhakikisha UNAILINDA AMANI YAKO bila mafanikio huna budi KUKUBARI.
Ukikubari utakuwa unaiweka NAFSI yako kwenye MAJARIBIO YA KUANZA na ikiwa nafsi itakubari usiogope KUANZA.
Kuanza kunajengwa na NGUVU iliyoko ndani yako, Mtu anaeweza kuanza ANAYO MAFANIKIO YA KUTIMIZA NDOTO ZAKE kwa sababu amejua Makosa/Udhaifu wake ndo maana ameona ni bora KUUMIA KWA MUDA MFUPI ukapona jumla, Kuliko kudhania UTAPONA huku ukiendelea kutunza FUKUTO LA MAUMIVU likiiva hilo UTAJUTIA.
MUNGU anayo Mamlaka ya kukutoa kwenye MATESO lakini ukiisha kuondoka kwa hayo, Kataa kuishi kwenye udhoofu wa FIKRA kwa kufikiri kwamba UMEYAZOEA MAISHA ULIYOPO ni mazuri ama mabaya kikubwa AMANI ikiwa unayo amani GO AHEAD ila kama UPO UPOO TU kisa woga wa kujikomboa WEWE NI MWIKO WA MBOGA hata ukwepe vipi kulia😭😭😭 MOTO LAZIMA UUGUSE maana kazi yako kuzungusha vinavyopikwa, Muda ni rafiki wa MAISHA chunga MUDA wako Kwani MUDA ndo unaweza kukupeleka kwenye MAFANIKIO ila usipoulinda ANGUKO LINAKUHUSU.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria ðŸ™‹
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU