![Image may contain: 1 person](https://scontent-mrs2-2.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/15726967_1423176047701780_8478130998812870812_n.jpg?_nc_cat=102&_nc_sid=2d5d41&_nc_eui2=AeE202XMMD_katt-sPHvn_Pvi98mzEK8p5-TbpFDS-kmm1H6WRZcknaJB_OuCK7Sox-ssGQ7bXKktVGF9sPSSqqsufTwZZtvGHZz9tKss6IBNg&_nc_ohc=YAai3JwYYeoAX8LE0_U&_nc_ht=scontent-mrs2-2.xx&oh=9684985e86199f320e909bd1cd868b48&oe=5E91C845)
Tunaendelea na dondoo za matumizi ya lugha katika kuhakikisha mawasiliano yetu kwenye mahusiano yanakuwa mwanana. Na leo nitaongeza aina mbili za lugha ambazo si nzuri kutumia kwa yule umpendaye hata kama ukiwa na hasira.
JE WAJUA?
🔱Awezaye kutawala kinywa chake ana nguvu kuliko awezaye kuteka mji, tena nikukumbushe kuwa ulimi ni kiungo kidogo lakini kinaweza kuponza maisha yako yote!
❎Lugha ya kudhalilisha.
1. Nguo hii chafu kwani ilivaliwa na nguruwe.
2. Vipi mbona unaparamia kama mbwa.
3. Jamani hii harufu ya jasho au kuna kitu kimeoza?
✅Badala yake ungeweza kusema
1. Naomba usivae nguo zaidi ya mara moja inachafuka kupita kiasi.
2. Mpenzi taratibu, mambo mazuri hayataki haraka.
3. Dia una jasho naomba ukaoge ndipo uendelee na mambo mengine (huku unamsaidia kuinuka hadi kufika bafuni)
❎Lugha ya kashfa.
1. Na wewe unaongea kama mwehu!
2. Unaacha nyumba shaghala baghala kama mtoto!
3. Unafanya mambo kama hujaenda shule (huku unajua amesoma hadi chuo kikuu)
✅Badala yake ungeweza kusema
1. Ukitaka kuongea tuliza mawazo, ongea taratibu, nitakusikiliza tu.
2. Naomba usiache chumba bila mpangilio mzuri, sijisikii vizuri vitu vikiwa hivi.
3. Mpenzi wewe umesoma nategemea vitu bora zaidi.
NB.
Hakuna mtu anapenda kudhalilishwa au kutukanwa, hata kama mtu atavumilia au kuzoea lugha hizo ukweli ni kwamba zinaua ukaribu wa kimapenzi (intimacy) kati ya wapenzi!
🍎 Haya mpenzi msomaji wangu, naamini unazidi kunufaika na dondoo hizi za mawasiliano. Huo ni mwongozo tu, naamini unaweza kuboresha zaidi ili ufurahie mahusiano! Endelea kufuatilia makala zangu!