-->

UMETOKA KUACHIKA; SOMA HAPA

Image result for mapenzi wakubwa

UMETOKA KUACHIKA; Acha Kutaka Kuwa Malaika Kama Amekutongoza/Amekukubali Wewe Ni Mtu Sahihi Kwake; Najua kwakua umeachika labda uliumia sana basi una mawazo mengi, unajiona labda kuna sehemu unakosea, unakua unaangalia mapungufu yako mengi kiasi kwamba unakua makini. Kila saa unajiangalia na kutaka kufanya mambo kisahihi kama Malaika ukijiambia “Sitaki kufanya makosa kama ya zamani!” Nikuambie tu kuwa kama alikutongoza kwanza kavutiwa na wewe, lakini kama ulimtongoza na akakukubali pia kavutiwa na wewe.
Huna haja ya kuwa Malaika na wala usijaribu, inawezekana mahusiano ya zamani yalishindikana tu lakini kama uliona makosa yako basi jirekebishe lakini ujisamehe pia, acha kujihukumu kila siku, acha kutumia muda wako mwingi kujaribu kumfurahisha mhusika kuwa kama mtumwa kwake, kujaribu kufanya kila kitu anachokitaka yeye ili tu nayeye asikuache. Hii hutokea mara nyingi kwa wanawake, anapoachana na mtu aliyekua anampenda hujiona kama alikosea sehemu.
Hata kama yeye ndiyo alikosewa na labda alimfumania lakini bado huishia kuwaza “Labda alichepuka kwakua sina tako, nimenenepa, nina tumbo, sina hiki, nina tabia hii na hii…” Kwa sababu hii wanawake hujikuta wakihangaika kutaka kua Malaika, kutaka kuwaridhisha tu wanaume wapya. Hii huwafanya kugeuka kutoka kuwa wapenzi na kujikuta wanakua watumwa wa mapenzi, unapokua kama mtumwa au mfanyakazi kufanya kila kitu anachotaka mwanaume ili tu usimuudhi basi jua unaboa.
Kumbuka kuwa mwanaume anajua kua wewe ni binadamu, anatagemea ufanye makosa kwani hatayeye hufanya, lakini kama kila siku unaigiza kama Malaika basi utakua unamboa kwani ataona kabisa unaigiza, ataona huna furaha na itaharibu mahusiano mapya. Hivyo acha kuigiza, acha kujihukumu acha kuangalia mapungufu yako, kama alikutongoza jua una kitu cha kumpa huna haja ya kuigiza kuwa binadamu.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU