-->

UKIACHWA! USIJE KUBALI HILI LIENDELEE KUWEPO

Image may contain: one or more people, people standing, shoes and outdoor

Usikubari aondoke mguu mmoja na mguu mwingine uwe kwako, mruhusu aondoke mazima ili akampate ambaye anadhani yeye ni zaidi yako, Wala usijisumbue kusema nae kwa lolote asije kukumiss
Mwache aende akiwa HURU ili akajinafasi huko alikoona Kuna THAMANI kuliko wewe, Mapenzi ya kuachana ki mwili lakini MIOYO inakuwa mihanga ni hatari sanaa, Yaani mtu amekuona humfai lakini moyoni bado anataka uwepo wako hiyo ni hatari kwako kwani mwenzio tayari anayo maamuzi japo hayajawa kamili.
Tayari TASWIRA ya uhusiano wenu ni wazi hakuna mwendelezo, Mmetawaliwa kesi nyingi na kisababishi USALITI kumbe unamng'ang'ania wa nini best?
Mapenzi Yakiisha YAMEISHA TU hata ukienda kwa waganga kujaribu kuyarejesha sana sana unajipa muda wa kuendelea kumfikiria wakati MWENZIO ndo kwanza yupo kwenye MAHABA MAPYA
Mwache ajinafasi mwili Mali yake, Kutumika anatumika yeye wewe unaumia nini tena?
Ni wivu kwamba ana mwingine? Tayari anae wewe huna THAMANI tena ama kwa wakati huo ama ndo amekuacha mazima hilo wala lisikuumize moyo, Vaa ujasili kuendelea mbele ili UJUE KUTOFAUTISHA PUMBA NA MCHELE.
Hakupendi hilo lishabainika ya nini kujitaabisha kutwa kutaka akurudie? Rafiki MAPENZI YAKIISHA YAMEISHA wala usiyalazimishe utajipa BP BURE.
Aliyekupenda ni mwoga kufikiri kukuudhi.
Aliyekupenda hapendi uhisi anakukosea.
Aliyekupenda hupenda AMANI yako.
Aliyekupenda hatajua kupanga kukuumiza.
Iweje wa kwako aseme ANAKUPENDA wakati kutwa anakuingiza kwenye MAUMIVU?
Ukimlazimisha awepo hawezi kuijua THAMANI yako kamwe, ila ukimuacha akaenda yakamkuta ya kumkuta na akapanga kurudi maana yake THAMANI YAKO IMEJULIKANA KWAKE na hapo itakuwa ridhaa yako kukubali ama kukataa kuwa nae, Pamoja na kwamba ASALI HAINA MAKOMBO lakini kujua uliyempenda amekuacha na akawa na mwingine halafu ukamrudia Mmmmmh huko sio kuonjwa kwa ASALI bali MALI YAKO KUTUMIKA VIBAYA.
Msaliti kamwe hajui kuacha bali hubadilisha njia na mbinu ili usijue lakini tatizo lipo pale pale KAZI KWAKO NA AKILI YAKO KUFANYA UPEMBUZI YAKINIFU
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU