Nikamuuliza "UNA TATIZO GANI?" Majibu yake yalinipa sababu ya kuendelea kuwa Karibu yake maaana tayari alionyesha amekata tamaa, Hataki kukaa na bin adam anataka awe peke yake tu, Sitopenda tena na wala sitaki kitu kinaitwa MAPENZI... Yalikuwa maneno machache toka kwa binti huyo lakini yalibeba hasira yake yote na kudhihirisha kuwa KUNA MTU AMEMUUMIZA! Nikamwambia kuwa kuishi bila MAPENZI yataka rehema ya MUNGU maana yeye ndiye alikuumbia huo moyo na mwili unao hitaji MAPENZI kwani mapenzi ni sehemu ya maisha ya bin adam, Ukisema hutopenda tena utakuwa unamkosea MUNGU maana yeye alisema TUPENDANE. Binti akatoa mguno fulani kama vile anataka kusema neno lakini bado akawa kimya, Nilimwambia kuwa UWAPO DUNIANI HAKUNA JAMBO RAHISI na kila jambo lina changamoto zake lakini pia ufanisi wa jambo huja baada ya kuwa umepambana, Binti alitoa tabasamu nikauona uzuri wake na kumuuliza NI NANI HUYO HAJAJIVUNIA NAFASI ULOMPA? Akasema PENYE MITI HAPANA WAJENZI bali Kuna wahunzi, Nilichojifunza kwa binti huyu baada ya maongezi ni kwamba wanawake huchukuwa muda mwingi sana kuwaza jinsi ya kuingia katika mahusiano lakini akiingia huwekeza MOYO, AKILI NA MWILI wake kwa mwanaume kiasi akigunduwa kuwa aliyempa nafasi hiyo siye basi huingia maumivu yasoponyeka haraka, Ni jambo la busara kwa wanaume kutambuwa kuwa MWANAMKE ALIVYO MGUMU KUINGIA KATIKA MAHUSIANO basi ni vyema ukimtaka mwanamke kwa haja ya mwili bora umshirikishe katika hilo ili akiingia isiwe shida kutoka wakati ukimaliza haja zako kuliko kudanganya una mhitaji awe mke na huku wewe si MUME ila mtumiaji.