-->

🙆‍♀SIMULIZI FUPI : UPENDO WANGU UMENIPA UKILEMA♥

Irene Uwoya is still Dogo Janja to break in her marriage – Habari ...

Ni mwaka mmoja tu umepita tangu mimi Aisha
nifunge ndoa na Mume wangu Ally.Mwanzo maisha
yalikuwa mazuri kiasi kwamba nilitamani hata
tusizeheke wala kufa lakini ghafla mwenzangu alianza
kubadilika.Nilimchunguza nikajua kuwa tayari
ananisaliti na ana mwanamke mwingine nje.

Nilichukulia tu kama kawaida ya wanaume
kutokuridhika lakini nilichojivunia ni kuwa mimi ndie
mke halali na mwenye pete kidoleni hao wengine ni
wapita njia na wala hata siku moja hawataweza
kusogea kwenye mji wangu zaidi ya kuishia kuchezewa
tu na kuachwa,Pamoja na hayo yote japo niliwaza
sana na kuwa na hofu endapo sasa mme wangu
ataniletea magonjwa ya zinaa itakuwaje.

Ila niliishia kujipa moyo na kutupilia mbali mawazo
kama yale na zaidi ya hapo sikutaka hata kumuuliza
mme wangu chochote kuhusu huyo mwanamke
alienae nje,Niliishia tu kusema mimi ni mke halali na
nina mamlaka na Ally wangu.
Sikujua kama ukimya ule na upendo ule kwa mume
wangu baadae utakuwa mateso makubwa sana.

Siku moja nikiwa nimekaa sitting room naangalia Tv
niliona sms imeingia kwenye simu yangu na namba ni
ngeni.Niliifungua Sms ile na kukuta ujumbe
unaosema"Achana na Mume wako vinginevyo
tutakuachanisha".Nilijiuliza sana hii namba ni ya wapi
na inatoka wapi sikupata jibu.Lakini moja kwa moja
wazo likaja huyu ni mchepuko wa mume wangu yule
ambae nilikuta sms zake kwenye simu ya mume
wangu.Sikutaka hata kujibizana nae kwa sababu
niliona ni ujinga na wala sikutaka hata kumuuliza
chochote mume wangu japo sms ilikuwa ni ya
vitisho.Niliona tu kuwa huyu mdada hana jipya kakosa
la kufanya zaidi ya umalaya wake na anataka tu
kunigombanisha na mme wangu.Sikutaka hata siku
mmoja mimi na mume wangu tuje tugombane au
nimuwekee kinyongo chochote.Nilichokuwa napenda
ni kumuona mume wangu anafuraha siku zote hilo tu
lilinifanya nijisikie raha na kujiona kuwa nina mume
nimpendae hivyo sikutaka kujua au kusikia ni
wanawake wangapi wanatoka na mume wangu na
anawahonga kiasi gani haya yote sikuyataka.

Hivyo niliamua kuifuta ile sms wala nisibaki nayo
kwenye simu.Kufanya hivyo kumbe ndio nilikuwa nazidi
kujichimbia zaidi kaburi.
SIKU moja wakati natoka saloon kutengeneza nywele
zangu mida ya saa moja inaelekea saa mbili
usiku.Nilikuwa kwenye kiuchochoro napita ili
nikatokezee barabara kubwa kisha kupanda pikipiki
nielekee nyumbani.

Nikiwa kwenye kale ka uchochoro ghafla wadada
watatu walijitokeza na kunizuia njiani.
Kabla sijafanya chochote mmoja wao aliniziba
mdomo kisha kunivuta pembeni.Nikiendelea
kutahayaruki mwingine alinishika kwa nguvu zaidi
nisiweze kufanya chochote kisha yule kiongozi wao
akaniambia"Si nilikutumia sms uachane na mumeo
ukaniona mimi fala.Anaefaa kuolewa na mumeo sio
wewe ni mimi hapa sasa leo tutakufundisha"Nikiwa
siwezi kuongea chochote kutokana na kuzibwa
mdomo yule dada alitoa kitu kama chupa yenye maji
maji.Nilitamani kupiga kelele lakini
ilishindikana.Nilitamani niombe msamaha lakini
ilishindikana zaidi nilibaki kutoa macho kuangalia nini
anataka afanye.Nikiwa nimetoa macho yangu
nilishangaa kuona anaitikisa ile chupa kama mtu
anaechanganya dawa kabla ya kunywa.

Mara ghafla bila huruma mwanamke yule alinipulizia
dawa ile machoni mwangu ambapo muda huo
nilikuwa nimeyatoa zaidi kwa ajili ya kushuhudia
tukio.Niliyafumba kwa maumivu makali sana ya ile
dawa aliyonipulizia na ghafla macho yangu yakaanza
kuuma.Nilijalibu kufumbua angalau nione kitu ama
hakika huo ndio ulikuwa mwisho wangu wa kuona
DUNIA

Nilisikia sauti ya yule mwanamke akisema"Na bado
leteni nyundo".Moja kwa moja nikajua sasa
wananimalizia uhai wangu.Nyundo kali ilitua katika
mguu wangu wa kulia na kusababisha maumivu makali
sana katika mwili wangu.Nilipiga kelele ya
kuungurumia ndani kwa ndani kwenye tumbo pasipo
hata kutoa sauti kutokana na Maumivu makali
niliyoyapata.Kabla hata maumivu ya mguu huo
hayajapoa mara........

.....Nyundo ilinyanyuliwa na kunivunja mguu wa
pili.Hapo maumivu yalizidi zaidi na kujikuta naanza
kulia ijapokuwa tayari ni kipofu."Hii ndio dawa
yake".Walisema wale wanawake huku wakicheka kisha
kuniachia na kunikimbia.Nilianza kulia damu nyingi
zilinitoka miguuni nilipiga kelele hatimae nikazimia.

Nilikuja kupata fahamu na kujikuta nipo mazingira ya
tofauti.Nilijaribu kufumbua macho lakini sikuona
kitu.Nilisikia kelele za hapa na pale na hatimae nilisikia
sauti ya mama ikisema"Jamani mwanangu
amezinduka".Mara pia nilisikia sauti ya mume wangu
ikinitakia pole huku kwa mbaali mama alianza
kulia.Niliuliza niko wapi hapa,Mama alichukua jukumu
la kunielezea."Uliokotwa na wasamalia wema na
kukufikisha hapa kisha wakatumia simu yako kumpigia
mme wako kuwa upo hospitarini leo ni siku ya pili
tangu uletwe hapa ulikuwa umezimia mwanangu
nilijua nimeshakupoteza."Mama alianza kulia kwa
kwikwi kitendo kilichosababisha na mimi nianze
kulia"Ona mwanangu dunia vile mbaya wamekuvunja
miguu na pia wamekuharibu macho sijui umewakosea
nini mwanangu".Maneno haya ya mama yalinifanya
nizidi kulia zaidi hasa baada ya kusikia nimekuwa
kilema wa milele.

Yote haya yamesababishwa na hawala wa mume
wangu.Nilijisemea moyoni,sikutaka kusema chochote
zaidi ya kukaa kimya na wao kuamini kuwa ni vibaka
ndio walionitendea haya.
Nilikaa hospitali takribani wiki mbili nikihudumiwa na
hatimae nililuhusiwa.

Nilipotoka hospitarini moja kwa moja nilifikia kwa
mume wangu lakini cha ajabu nilikaa siku ya kwanza na
ilipofika siku ya pili Mume wangu aliniambia niende
nyumbani na Mama nikakae kule mpaka nitakapokaa
vizuri na miguu itakapoungana vizuri
nitarudi.Aliniambia kuwa pale hamna mtu wa kusema
nikae nae na kuniangalia hivyo bora niende nyumbami
mama yupo.Alinipa maneno ya faraja kuwa japo kuwa
nimepoteza macho lakini mimi bado ntabaki kuwa
mke wake hivyo nitakapopona vizuri nitarejea
nyumbani na atafanya mpango zaidi ikiwezekana
tusafiri nje ya nnchi nikatibiwe macho.
Nilikubariana na nikasafiri mpaka mkoani kwetu na
mama na wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi
miwili.

ZILIPITA kama wiki mbili hivi tangu niludi kwetu.Siku
moja usiku sikuamini baada ya mume wangu kunipigia
cm na kuniambia"Mimi na wewe basi tena,Siwezi kuwa
na mke kilema taraka zitakufuata huko huko".Kisha
simu ikakata.Nilishindwa kuitafuta namba nimpigie
tena kwa sababu ya upofu wangu.nilibaki nalia
tu.Nilimuelezea mama yangu hayo maneno nae
akanitia maneno ya faraja na kunifanya nipunguze
kulia"Mwanangu angalia vilema wote vile
wanavyotengwa na jamii wewe sio wa
kwanza,Maadam nipo mimi mwanao nitakulea
mwanangu Mungu atakusaidia tu utapona zaidi
mshukuru Mungu kwa yote wewe pia sio wa kwanza
kuachika ipo siku Mungu atasikia kilio chako utapona
na kusimama na kuona tena mtumaini Mungu."

Hakika maneno haya yalikuwa ya faraja sana
kwangu.Siku hazikupita na kweli niliachika kwa Mume wangu nilianza maisha ya kukaa nyumbani na mama yangu huku nikijuta ni bora toka mwanzo ningefungua
kesi,Ni bora toka mwanzo nisingempenda mume wangu kiasi hiki,Ni bora ningeusema ukweli wote yaliyonikuta.Upendo wangu ka kukaa kimya kwangu kumeniponza.Nashukuru Mungu nilijifungua salama na nina Mtoto japo nae nasikia kaoa tena nadhani
atakuwa yule mwanamke alienitendea mabaya
haya.Sifa na shukrani naludisha kwa mola japo sioni.

Lakini napenda kuacha ujumbe huu kwa jamii na kuwauliza wanaume.KWANINI HAMTOSHEKAGI??

#MWISHO Shea na wengine waone
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU