
......ππ _Ifuatayo ni mada husika:_
1. Anaporudi kutoka kazini, safarini au kwenye shughuli yoyote iliyowatengenisha, anza kwa salamu nzuri.
πππππππππ
2. Unapompokea au kukutana naye basi fanya hivyo ukiwa na uso wa bashasha.
πππππππππ
3. Vaa mavazi nadhifu. Jipambe na upake manukato kwa ajili yake.
πππππππππ
4. Unapoanza kuzungumza naye anza na mambo au taarifa nzuri, na kama kuna taarifa mbaya subiri mpaka atakapopumzika.
πππππππππ
5. Mpokee kwa maneno ya upendo na lugha ya kumpongeza au kumpa pole au lugha yoyote inayoonesha kumhurumia kwa kazi za kutwa nzima.
πππππππππ
6. Ipendezeshe na uilainishe sauti yako kwa ajili ya mumeo⦠usifanye hivyo mbele ya wanaume wengine.
πππππππππ
7. Utunze mwili wako na kujiweka katika hali ya umaridadi na siha njema.
πππππππππ
8. Oga mara kwa mara, na pia baada ya siku zako.
πππππππππ
9. Epuka kuwa katika hali ya uchafu au muonekano mbaya.
πππππππππ
10. Epuka mapambo yaliyoharamishwa kama vile kujichora tattoo na kadhalika.
πππππππππ
[12/13, 19:33] ricon: 11. Tumia manukato, rangi na mavazi yanayopendelewa na mumeo.
πππππππππ
12. Jitahidi mara kwa mara kubadili mtindo wa nywele, manukato na kadhalika. Lakini usizidishe kiwango, na ufanye hivyo kwa mumeo tu au mbele ya mahram wako.
πππππππππ
13. Usichelewe kumpa mahaba pindi mumeo anapojiwa na hisia ya kutaka kufanya mapenzi.
πππππππππ
14. Mwambie maneno matamu na yenye mvuto wa mahaba.
πππππππππ
15. Ridhika na yale uliyoruzukiwa na kukadiriwa na Allah.
πππππππππ
16. Kumbuka kuwa utajiri wa kweli hupatikana katika imani na uchamungu.
πππππππππ
17. Usihuzunike kwa sababu mumeo ni masikini au anafanya kazi ya kawaida. Watazame maskini, wagonjwa na walemavu kisha umshukuru Allah kwa aliyowajaalia.
πππππππππ
18. Usimuombe mumeo mambo mengi yasiyokuwa na ulazima.
πππππππππ
19. Uchamungu hauna maana ya kutofurahia mambo mazuri nay a halali, bali una maana ya kuiangalia Akhera na kuyatumia yale uliyojaaliwa na Allah kwa lengo la kuifikia Pepo Yake.
πππππππππ
20. Mshajiishe na umhamasishe mumeo kupunguza matumizi na kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya sadaka na kuwasaidia maskini na wale wenye dhiki.
πππππππππ
21. Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo.
πππππππππ
22. Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.
πππππππππ
23. Ukiwa mtovu wa shukrani, mumeo atasikitishwa na hali hiyo na kuanza kujiuliza: βKwa nini nimfanye mambo mazuri mtu asiyekuwa na shukrani?β Epuka hali hiyo.
πππππππππ
24. Daima kuwa mtiifu kwake.
πππππππππ
25. Shikamana na mumeo, hususan katika nyakati za shida, dhiki, maradhi au mumeo anapofilisika au anapokuwa hana pesa.
πππππππππ
26. Muunge mkono kupitia kazi yako, fedha yako au mali yako pindi inapohitajika.
πππππππππ
27. Fuata maagizo yake, isipokuwa katika mambo ya haramu. Katika Uislamu, mume ni kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.
πππππππππ
28. Jaribu kuepuka yale yanayomkasirisha.
πππππππππ
29. Mfurahishe anapokuwa ameghadhibika.
πππππππππ
30. Ukimkosea muombe msamaha.
πππππππππ
31. Akikosea usihamaki kwa kumfokea au kuzozana naye. Subiri anapokuwa hana ghadhabu na uzungumze naye kwa amani na kwa kauli nzuri.
πππππππππ
32. Akiwa na hasira kutokana na mambo ya nje ya nyumba basi subiri mpaka atakapoondokana na hasira hiyo.
πππππππππ
33. Mpe faraja na kumuonea huruma, yumkini akawa amechoka, ana matatizo ya kikazi au kuna mtu kamtusi, n.k.
πππππππππ
34. Usimuulize maswali mengi au kungβangβania kutaka kujua yaliyotokea. Mathalan, kuna wanawake wengine wakiona mume ana hali tofauti huanza kusema: Niambie kumetokea nini? Lazima utaniambia kilichokufanya mpaka ukawa na hasira hivyoβ¦ unaficha nini? Nina haki ya kujua au kuna mwanamke kakuvuruga?
πππππππππ
35. Jilinde dhidi ya mahusiano yaliyoharamishwa.
πππππππππ
36. Tunza siri za familia, hususan mambo ya chumbani na mambo mengine ambayo mumeo hapendi watu wayajue.
πππππππππ
37. Usisahau kushughulikia vizuri malezi ya watoto na huduma za nyumbani. Mumeo atafurahia kula chakula ulichompikia na chenye virutubisho.
πππππππππ
38. Zilinde mali na fedha zake.
πππππππππ
39. Usiende matembezini au nje ya maeneo ya nyumbani bila idhini yake; unapotoka vaa mavazi sahihi.
πππππππππ
40. Usiwakaribishe au kukutana na watu ambao hapendi ukutane nao.
πππππππππ
41. Usikae faragha na mwanaume yeyote ambaye sio mahram wako.
πππππππππ
42. Kuwa mwema kwa wazazi na ndugu zake. Wakaribishe wageni wake.
πππππππππ
43. Jitahidi sana kuepuka migogoro na ndugu zake.
44. Epuka kumuweka katika hali na mazingira ambayo anatakiwa kuchagua kati ya mamaye na mkewe.
πππππππππ
45. Onesha ukarimu kwa wageni wake kwa kuwaandalia sehemu nzuri ya kukaa, chakula kizuri n.k.
πππππππππ
46. Mhamasishe kuwatembelea ndugu zake nawe uwaalike kuja nyumbani kwako.
πππππππππ
47. Wapigie simu wazazi wake na dada zake, watumie ujumbe mbalimbali wa kuwajulia hali, wanunulie zawadi, waunge mkono katika nyakati za matatizo na shida.
πππππππππ
48. Usifuatilie au kutengeneza shaka zisizokuwa na msingi.
πππππππππ
49. Wivu ni alama ya upendo wa mke kwa mumewe lakini usivuke mipaka ikafikia hatua ukawatukana watu au kuwavunjia heshima.
πππππππππ
50. Kuwa mwenye subira na stahmala mnapokuwa katika wakati mgumu kifedha au kimaisha. Kuwa mvumilivu mnapokutwa na majanga mbalimbali na hususan mumeo anapofukuzwa kazi, mpe nguvu.
πππππππππ
: 51. Shirikiana na mumeo na umkumbushe kutekeleza ibada mbalimbali za faradhi na za sunna.
πππππππππ
52. Mhamasishe kuswali swala za usiku. Sikiliza na usome Qurβan Tukufu unapokuwa peke yako na ukiwa na mumeo pia. Mdhukuru Allah sana, hususan baada ya swala ya Alfajr na kabla ya Maghrib.
πππππππππ
53. Jifunze sheria mbalimbali za Kiislamu na adabu za wanawake.
πππππππππ
54. Msaidie mumeo katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kumpa nguvu,
kumhamasisha, kumpa ushauri mzuri, kumfariji na kadhalika.
πππππππππ
55. Jitahidi nyumba iwe safi, ipanmbe na kuiweka katika mpangilio na mandhari mazuri.
πππππππππ
56. Andaa chakula kizuri na kinachojenga afya.
πππππππππ
57. Jifunze stadi zote muhimu za kuendesha nyumba kama vile ushonaji, mapishi na kadhalika.
πππππππππ
58. Jifunze namna ya kuwalea watoto vizuri na kuwapa mwenendo mwema wa malezi ya kimaanawi.
πππππππππ
59. Usitumie fedha zake bila ruhusa yake, hata kama itakuwa kwa ajili ya kutoa sadaka, labda kama una uhakika kwamba ataridhia.
πππππππππ
60. Jitahidi kuwaweka watoto katika muonekano mzuri, mavazi safi n.k. Wape chakula chenye virutubisho, zingatia sana afya yao, elimu na maadili mazuri. Wafundishe Uislamu na uwasimulie visa vya mitume na maswahaba.
Ninamuomba Allah azijaze nyumba na nyoyo zetu utuvu, upendo na kuhurumiana sasa na hata milele!!!