Kuna fasheni imekuja siku hizi, nasema fasheni kwani kimekua kama kitu cha kawaida. Mwanaume anamuambia mwanamke, tena mchumba wake ambaye ashamsotesha miaka mitatu.
Yaani miaka mitatu Dada wa watu amekua kama mkewe anampikia na kumpakulia, anamfulia na kumdekia anamkatikia kiuno na kumpigia pasi halafu mwaka wa nne dada akiuliza jamani unanioa lini?
Dada wa watu kachoka na kaona anachakaa muda si muda hata faa hata kujiita tena msichana anauliza halafu jamaa anajibu. “Nataka tuzae kwanza nidyo nikuoe!” Kweli yaani ulivyomchosha hivyo hujaridhika unataka na kumzalisha tena?
Yaani unaona kuzaa kama kitu rahisi, hivi unajua anabeba mimba miezi tisa, hivi unajua akishazaa hakuna kurudia ubinti. Halafu unaongea tu kama kitu cha kawaida kama mtu anasema “Tuoge kwanza ndiyo twende mjini!”
Sasa hapo mimi nashindwaga kuelewa, unachotaka kuoa ni nini Mtoto au Mama yake, kwamba miaka yote mitatu mko pamoja umeona hana sifa, hana vigezi vyakuwa mke wako mpaka umzalishe.
Kama Mungu hajampa kizazi inamaana hutamuoa, vipi kama akizaaa na mtoto akawa bahati mbaya napo hutamuoa. Mungu epushia mbali lakini yapo, dada wa watu kakuzalia sasa, umesema yes namuoa. Mipango ya harusi inakiamilika mtoto Mungu kamchukua miezi mitatu kabla ya ndoa, je utamuacha au mpaka azae mwingine?
Dada zangu kama mwanaume anafanya kazi, anaweza kujitegemea na anauwezo wa kukuoa halafu anakuambia kua nizalie kwanza ndiyo nikuoe kimbia kabisa. Muulize hivi unataka kunioa mimi au mtoto?
Kuna sababu mbili kwanini wanaume wanasema hivyo, sababu ya kwanza nikuwa wewe si wa type yake na umri umeenda hivyo anaona wakati akisubiri kupata mchumba basi apate mtoto kwanza, hapa kuna mawili, akikosa anayemtaka akuoe au akipata akutelekeze.
Lakini kuna jambo la pili, inawezekana ana mtu wake tayari lakini anamzingua hataki kuolewa hivyo anaona azae kwanza na hapo jua kuwa yule mwingine akishaona kashakupa mimba anajirudisha na unaachwa huku uking’aang’aa macho.
Hivyo zaa na mwanaume kama unataka na si kwasababu ya ndoa. Labda na wewe ulishachoka kusubiri una hamu ya mtoto na kwavile huwezi kuzaa mwenyewe ndiyo unaamua uzae naye ukijua kuna mawili anaweza kukuoa au kukutelekeza.
Usifikiri labda mtoto ndiyo kitakua kigezo cha kumshikilia mwanaume hapana. Kama huamini angalia tu yule rafiki yako ambaye ni Single Mother, muulize kama nayeye si alikua anapendwa kama wewe na katelekezwa na mtoto?
Wanaume siku hizi ni vichomi hivyo acha kujishikiza kwa mwanaume kwa kutumia mtoto. Kama watu wanatelekeza watoto wao wa ndoa huyo ambaye si wandoa unafikiri atamhudumia.
Ukiamua kuzaa nnje ya ndoa basi jua na kulea na si kutegeme amwanaume, kama imetokea bila mipango hapo sawa ila unapanga kabisa kua nizae atanioa au nizae naye anapesa atatunza mtoto…Pole Dada muulize jirani yako kilichomkuta???
#SHARE Kama #IMEKUBARIKI