-->

MWANAMKE ULIAMBIWA NA NANI KWAMBA UKIFANYA HAYA NDIYO UTAMFANYA MWANAUME AKUPENDE?

Image result for sanchiworld
Mwanamke uliambiwa na nani kwamba ukifanya Haya ndiyo utamfanya Mwanaume akupende?;
KUZAA📌
KUWA KIBURUDISHO📌
KUJIGHARAMIA KUOLEWA📌
KUMPA MWANAUME KITU ILI KUMLINDA ASIENDE KWA MWINGINE📌
Na mengine ambayo yanafanana na hayo kwamba lazima ushiriki kumfanya Mwanaume KUKUTAKA kuliko KUKUPENDA.
Wahenga na misemo yao "KAMA IPO IPO TU" Maana yake kama ANAKUPENDA ATAKUPENDA TU wala hutakiwi kulazimisha UPENDWE.
Heshima yako ni wewe KUHUDUMIWA KWA NAMNA YOYOTE ILE iwe kwa umasikini ama utajiri kikubwa UWE NA MTU AJUAYE KWAMBA WEWE NI MWANAMKE WAKE.
Wanaume wa sasa uwe na kazi ama usiwe na kazi UTAJINUNULIA NGUO wala hawajishitui hata akiona Una nguo mpya kisa wanakimbia majukumu😅😅
Kama ingekuwa KUZAA ndo mwanaume anatulia unadhani Mwanamke yupi angelilia MAPENZI?
Kwamba unapomvulia👙 mwanaume ndo anakuwa wako unadhani Kuna Mwanamke angelilia MAPENZI?
Wapo waliojichumbia na kujitolea mahari Lakini Bado wanalilia MAPENZI wewe ni nani usililie?
Lakini kama wewe ndiye unayetoa pesa Mwanaume akakulipie MAHALI wewe ni mhanga.
kama wewe ndiye ambaye unasimamia mahitaji ya familia na una mume hakika wewe ni mhanga.
Kama wewe ndiye unayetoa mwili wako kama kiburudisho sikufichi wewe ni mhanga.
Kama wewe ndiye ambaye unalea watoto na kuwatunza na unajiita mke wa mtu kwa hakika WEWE NI MHANGA.
Nature ya UPENDO ni Mwanamke kusimama eneo linalomhusu lakini vivyo hivyo MWANAUME KUJUA YEYE NI KICHWA ila kama wewe unalichukulia swala la kuishi na mtu asojua majukumu yake kwa kigezo cha MAISHA KUSAIDIANA kisa unayo nafasi ya kufanya hivyo kwa hakika wewe DUNIA IMEKUACHA MBALI SANA japo nikushauri kwamba;
Ikiwa Mume alikuoa kwa gharama zake, alijua kukuhudumia wewe na watoto, alitekeleza MAJUKUMU YAKE KAMA BABA baadaye akaugua ama kupata tatizo ambalo limemsababisha kuwa TEGEMEZI Basi dadaangu MSHUKURU MUNGU
Kinyume cha hayo WEWE UMEOA wala HUJAOLEWA
Hata wahindi pamoja na ukweli kwamba MWANAMKE NDIYE ANAYEOA ila inabaki kuwa tamaduni yao ila kwenye UUMBAJI WA MUNGU MWANAUME ANABAKI KUMHUDUMIA MWANAMKE KWA KILA KITU😎
Ukiona Mwanaume hasikii aibu KUHUDUMIWA NA MKEWE ujue huyo ni MPAKATO Mpakate Mama😅😅😅
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria💪
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU