Kuzisusia hisia sio unazikomoa,sio unamkomoa unayehisi hisia zako zimeenda kukaa,bali unajikomoa mwenyewe.
Na tunaelezwa kuwa hisia kuzificha ni ugonjwa unaulea,hazirudigi nyuma.
SITOPENDA TENA.
Wengine mpaka nife sitaki kusikia kitu mapenzi.
Jamani sio kweli,hata Kama umetendwa ukaumia vibaya,hisia Kuna wakati lazima zione mahali pa kuketi,isipokuwa ni uoga wa kuumizwa unakufanya uzibane hisia usiruhusu kuket mahali zinataka,unapenda ila muoga kutendwa.
SIO TIBA.
Ingetosha kujipa tiba kutibu moyo kwa Majeraha,usiingie kwenye mahusiano mapya kabla ujapona Majeraha,ni hatari kwa afya ya mahusiano mapya,unajikuta unayatibua upya na ukose hamu ya kuwa Duniani,utataka ufe.
Umemaliza kujitibia usihofie kupenda,penda tu kwa maana Mungu katika vitu ameviumba kea wanadamu wala hatufanani,sio sura,sio tabia,hata mitazamo,hata hulka na mengineyo.
Kuyasusa mapenzi ni kujitesa bure,kukosa haki ya moyo,nafsi na mwili kuyafurahia maisha.
Kuna mtu Leo anasema mapenzi Nini bhana Niko busy kusaka pesa.
Ila mida mida ikifika anajishughulisha mwenyewe,yuko chumbani peke yake anajisexisha,matango yanateseka Sana.
Wengine ni mwendo wa kujichua,sabuni xinaisha Sana.
Kiss tu alitendwa na Athman,basi ndio tutukanwe wanaume woote.
Alitendwa na Agnes ni kosa la wanawake woote.
Sio sawa sio kweli,aliyekutenda no mmoja tu,na usipoteze bahati kuzitupa hisia za mtu.
Wakati mwingine Mungu anamleta mtu kuja kutibu maumivu yako, na anapomleta hakuoteshi ndoto amemtuma Albano awe tabibu wako,Je Kama unamdhalau kwa kudhani ni wale wale utawakosa wangapi.
Tusizitupe bahati narudia kusema,hakuna binadamu ana milango yoote ya fahamu akaumbika akose hisia,hakuna labda Kama huna ukamilifu.
Kila kitu kimeumbwa kwa mipango ya Mungu wewe uwezi kujiongeza hata unywele mmoja kichwani,mnazojibebesha ni fake tu.
🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃
Sauti Veep niongeze au Kali sana nishushe.