Mkeo anapojisikia udhaifu na unyonge, shughulika naye kama baba anavyoshughulika na binti yake.
πAnapolia, shughulika naye kama mama anavyoshughulika na mwanaye.
πAnapofanya kosa, shughulika naye kama kaka anavyoshughulika na dada yake.
πAnapolalamika, shughulika naye kama rafiki anavyoshughulika na rafiki yake.
πAnapohisi khofu, muingize moyoni mwako na ushughulike naye kama mpenzi anavyoshughulika na kipenzi chake.
πAnapohitaji ushauri, shughulika naye kama dada anavyoshughulika na ndugu yake.
πNa mfanye ahisi kuwa daima uko naye na utaendelea kuwa naye mpaka pumzi yako ya mwisho.