-->

KIPIMO CHA UPENDO NI MIGOGORO

Image may contain: 1 person, sitting and indoor

KIPIMO CHA UPENDO MIGOGORO lakini je unajua kutofautisha migogoro inayoendana na UHUSIANO uliopo?
Uliwahi kuwaza Kwanini UNAHITAJI MAHUSIANO kwenye Maisha yako?
Nataka nikwambie juu ya Maana ya neno;
"OA" ni maana ya KUOANA baina ya watu wawili ambao wao wameridhia kuishi kwa mtazamo wa MKE NA MUME
Kuwa wamoja ni KUFANANA sina maana ya sura, mwili, au wajihi bali namaanisha MATENDO YA KUCHUKULIANA kama vile Tabia pamoja mapokeo ya ki matendo ya upendo, Ndoa ni kama RAMANI inaunganisha mchoro, Ni ngumu wawili kuungana na kunia mamoja ikiwa MITAZAMO YAO NI TOFAUTI
Ni HASARA kuingia uhusiano ambao haukui na kama unakua ni wewe ndo unasababisha ukue, Utafaidika nini ikiwa uko na Mtu ambaye kipaumbele chake ni KUKUTUMIA WEWE.
Raha ya MAHUSIANO ni pale unapokuwa unapokea UPENDO kwa mwenza wako hata kama utakuwa ni mdogo kiasi gani unaweza kusitawi na kukusababisha kuhisi UNAPENDWA! Lakini kama hakuna viashiria vya UPENDO uwao wowote wala sipepesi macho ONDOKA KWENYE UHUSIANO HUO maana sio mahala sahihi, UHUSIANO unajengwa na UPENDO ama matendo yaliyo na vinasaba vya UPENDO.
Kila mmoja ambaye amefikisha umri wa kujua MAPENZI anayo historia ya uhusiano aliko ama atokako, Lakini lililo na THAMANI ni kuanguka na ukajua kilicho kuangusha ili baadaye UKIINUKA uweze kusahau MAUMIVU uliyoyapitia, Nje ya hapo USIJIDANGANYE KUBADILI UHUSIANO KAMA VILE NI NGUO Kwani hakuna kitu kinalinda UTU wa Mtu kama KUJIHESHIMU... Sasa wewe swamper👣 kama vile unalipwa ili wakati wako ukipita UJE KUTAFUTA HATA WA KUKUPA FARAJA USIMPATE
Maisha ni KUFURAHIA na kujawa AMANI ziada ya hayo UHURU ikiwa hayo huyaoni maishani mwako ama wewe ni MKIMBIZI au Mtu ambaye hujui TAHAMANI YA HAYO.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU