Usifanye makosa katika kuchagua mke au mme maana iwapo ukipatia ndio FURAHA NA AMANI vitatawala maisha yako ILA ukikosea jiandae kwa MAJONZI NA MAUMIVU ndani ya ndoa maana kukosea kuoa au kuolewa na mtu asiye sahihi asiyethamini wala kujali hisia zako ni AJALI MBAYA kama zilivyo ajali zingine. Yakupasa kijana unaetarajia kuingia katika ndoa au uliyekwisha kuingia uhakikishe unaiteka akili na moyo wa huyo uliemchagua.
Maisha hutawaliwa na furaha, upendo, amani, afya njema, baraka tele na mafanikio pale familia yenu itapokua imeundwa na ndoa yenye mapenzi ya dhati na kweli. Hakika ni jambo la muhimu mno na bahati ya thamani kubwa kumpata mtu sahihi atakayezithamini na kuzienzi hisia zako na upendo wako kwake, hakika utatamani mda usimame miaka isiende mbele ubaki hapo hapo milele ukifurahi na huyo kipenzi faraja wa moyo wako.
Vivyo hivyo ni furaha kubwa kwake utaempata utakapokuwa na mapenzi ya kweli na kujali, kuthamini na kuienzi ndoa yenu. Wazungu husema, "What goes around comes around" pia maandiko matakatifu yanasisitiza, "Mtendee mwenzio yale unayotaka utendewe, tenda wema daima"
Mwanamke, kabla hujafikiria kugusa mfukoni kwa Mwanaume yeyote tangulia kugusa kwanza Moyo wake utakuwa umefanikiwa kugusa mfuko wa pesa zake na kuzipata zote. Mwanaume, kabla hujafikiria kutamani mwili wa Mwanamke yeyote na kugusa, tangulia kwanza kutamani kugusa Moyo wake utakuwa umefanikiwa kugusa kila sehemu nzuri sana unayotamani ya mwili wa Mwanamke. Jitengenezee mazingira rafiki sana katika maisha yako ya kuwa ndiye mwenzi bora ambaye kila mmoja anatamani na kuomba Mungu uwe ndiye wake kuliko watu wengine wote duniani kwanza; Lakini anza hivyo kwa kubadili fikra zako
Kabla hujataka mme bora au mke bora anza wewe kujiandaa kuwa mke bora au mme bora HIYO NDIO SIRI KUU YA UJENZI WA NDOA IMARA YENYE AMANI, FURAHA, MAFANIKIO NA BARAKA TELE.
NB: Mapenzi ya upande mmoja ni UTUMWA sawa tu na ule wa wanyonyaji maana unakuta mtu upo nae katika ndoa au uhusiano ila kila kitu umfanyie wewe yeye yupo busy kimya kama hakuoni vile yaan,
#umpende wewe
#umbembeleze wewe
#umjali wewe
#umfariji wewe
#umliwaze wewe
#umhudumie wewe
#umkarimu wewe
#umuombee wewe
#umthamini wewe
#umuamini wewe
#umkumbuke wewe
Yeye kimya tu wewe ndio wajishebedua na kujipendekeza kama bajaji inaotafuta abiria stendi, Hahahahahaaaaaa my friend AMKA hakuna mapenzi ya kweli hapo.
Imepenya... Haijapenyaaaaa?????!!...
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE
✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿
Jumapili njema
All true Best 😋😘