Mpaka kuingia migogoro kwenye ndoa maana yake mambo hayako kama yalivyotakiwa yawe, Wengi wao kwenye NDOA badala ya kutafuta chanzo cha MGOGORO wamejikita kwenye kutafuta UWIANO WA MAISHA YA NDOA kwamba ikiwa ananisumbua Basi ninaweza kuwa na MTU MWINGINE NJE ambaye atanipa AMANI.
Rafiki yangu huo ni Sawa na ulevi, Kwamba unajua unapitia magumu ili kupoza japo stress unaamua kunywa pombe, Ni kweli utapoza je TATIZO UNALITATUAJE?
Jibu la swali hilo hata wenye PhD hawajaweza kulifafanua.
Migogoro inatatuliwa kwa mambo mawili;
▪ KUJUA KOSA.
▪ KUKUBALI KOSA.
Baada ya hapo ni MARIDHIANO na kukumbushana mlikotoka na mlipo sasa, Kinyume chake ni KUACHANA.
Ni bora kujua kwamba UMEPIGANIA NDOA YAKO ILETE MAANA HALISI YA NDOA LAKINI MWENZA WAKO HANA MTAZAMO HUO UKAAMUA KUPAMBANA JINSI YA KUJINASUA KWENYE KITANZI HICHO ili kuutafuta UHURU kuliko kutafuta mbadala, Rafiki yangu unajipunguzia siku za kuishi tu, Maana Stress ndiyo ISRAEL mkubwa kwa DUNIA tuliyopo kwa sasa kuliko hata KISUKARI.
Maradhi mengi yana tiba na ukifuata masharti ya ugonjwa ulionao unaweza kuishi kwa matumaini ila sio STRESS
Stress ya MAPENZI imeua wengi lakini walipokwenda hospital walikutwa na BP, KISUKARI, VIDONDA VYA TUMBO maana hayo ni pacha wa stress, Kuliko kulazimisha NDOA kama unaipenda NDOA yako JUST FIGHT na ukishindwa KUFA Taratibu ukiwa hapo hapo, Wenzio kwa sasa hawang'ang'anii JEHANAM maana maisha ni MATAMU wallah
Kama unaishi na Mtu kama MKE NA MUME lakini maana ya NDOA haipo kumbe mnatofauti gani na WAZINZI?
Maana migogoro ikianza huzaa USALITI kumbe ukisaliti unaitwaje?
MIGOGORO inatatuliwa kwa kuijua chanzo chake, Na kama haitatuliki kumbe unangoja nini? Asikudanganye ataacha ikiwa ni TABIA yake, Utangojea abadilike mpaka UNAZEEKA
#Elista_Kasema_ila_Sio_She