#inauma sana kiukweli
*Kuvunjika kwa mahusiano siku zote si jambo zuri kwani linagusa hisia na moyo, ndiyo maana linapotokea watu wanalia, watu wanakonda, wengine wanajiua kwa kushindwa kuvumilia lakini ukweli unabaki pale pale muda mwingine kwa kujua au kutojua tabia zetu zinaweza kupelekea mpenzi wako aachane na wewe licha ya yeye kukupenda.
*Mara nyingi hizi huwa ni sababu zinazopelekea wanaume wengi kuwaacha wapenzi wao, bila hata wao kutaka ila wanalazimika kufanya hivyo kulinga na tabia hizi au kutokana na mambo haya.
>1: Kufokeana naye na kutokuwa na maelewano naye
*Wapo wanawake au wasichana ambao wao wanataka kila jambo walitakalo wao ndiyo liwe linafanyika hivyo na ukifanya tofauti wanakuwa ni wakali wanaongea sana kiasi kwa kuwakera wenzao wao, kifupi hawajui namna nzuri ya kuongea na mpenzi wake. Wanashindwa kutofautisha lugha na tone ya kuongea na mtu haijalishi umekosewa au amekosea hupaswi kuongea ili uonekane wewe ndiye mwenye kauli. Usitake kuongea ili shoga zako wajue kuwa mimi ndiyo kichwa cha familia hata kama ndiyo ukweli, usitake kuongea ili kumshusha kwani tabia hizi kwa mwanaume hazivumiliki. Atavumilia kwa kipindi tu kwa kuwa anashida zake siku utashangaa anasepa utabaki unashangaa huyu si alikuwa ananipenda ndiyo kisha sepa hivyo.
>2: Mambo hasi (Negativity)
*Unajua kila kitu kikisha zidi kinakuwa sumu, unakuta mwanamke kila wakati kila saa akikaa na mumewe au mpenzi wake anawaza kusalitiwa tu, anawaza mambo mengine ya ajabu ajabu tu, mwisho wa siku mwanaume anakuwa hana amani. Maana anajua nikiwa na huyu mtu sasa hivi kinaweza kutokea kitu ambacho kitafanya tulumbane au kugombana. Ukiwa na tabia hii hakika utavumiliwa ila ipo siku yako huyo mtu hata kama anakupenda anashindwa kuvumilia na atasepa tu.
>3: Kuwa tegemezi kwa kila kitu
*Wanaume wengi huwa wanafanya maamuzi magumu hapa unakutana na mwanamke au binti ambaye amekuwa tegemezi kwa kila kitu, pesa, chakula, mavazi, mawazo, yaani inafika hatua hata ushauri wa nyumbani tunakula nini leo anatoa mwanaume. Ni jukumu la mwanaume kumlea, kumtunza, kumjali mwanamke na kumpa support katika mambo yake ikiwa pamoja na furaha na matatizo. Lakini mwanamke akiwa tegemezi kwa kila kitu. Wanaume wengi wanasepa maana wanaanza kuona huu ni kama mzigo.
*Mwanamke unaweza usiwe na pesa kabisa lakini unaweza ukawa msaada kwa mumeo au mpenzi wako hata kimawazo, ushauri ambao unaweza kuwa tija kwenu wote. Ukweli unabaki hapa wanawake wengi wanaachwa na watu wao kutokana na tabia zao.
>4: Umbali (Distance)
*Napozungumza umbali sina maana wewe sijui upo ulaya yeye yupo Mwanza hapana unaweza ukawa unaishi na mpenzi wako mkoa mmoja au kata moja lakini hamuonana au hampo karibu jambo ambalo linaweza kutngeneza njia kwa mtu mwingine kuingia kwenye maisha ya mpenzi wako huyo na kujikuta tayari umeshapinduliwa. Unaweza kuwa busy sana lakini unapaswa kuwa na muda wa kuonana mara kwa mara na yule unayempenda. Ukiwa busy sana na kukosa muda na mtu wako ipo siku utapata majibu ya ubusy wako huo kwani atasepa tu na kwenda zake.
>5: Mawasiliano mabovu
*Kila siku mmenuniana, kila siku mnagombana kila siku nyinyi hamzungumia vizuri, yaani ukipiga simu mbona simu yako ilikuwa inatumika? Mbona nilikupigia simu hukupokea? Yanii ukipiga simu badala ya kujenga mahusiano yenu unazidi kuyabomoa kutokana na mawasiliano yenu mabovu tabia hizi huwa zinavumilika kwa muda tu zikizidi utaachwa tu.
>6: Kupoteza mvuto
*Kuna wakati wanaume au wanawake wanaweza kutokuwa na sababu maalumu ya kuachana na mtu lakini ukweli unabaki pale pale kupoteza mvuto tena mvuto wa mapenzi ni jambo ambalo linaweza lisivumilike. Manaa mtu akipoteza mvuto na wewe simu zako ataona kero tu, maswali yako ataona shida tu, yaani kila kitu ataona taabu. Kila ukitaka kuonana naye hatakuwa tayari maana huna mvuto ule uliokuwa nao mwanzo.
MUHIMU
epuka kuwa chanzo cha sababu zisizo za lazima kuachana na akupendae maana mapenzi ni hisia alikupa moyo wake akiamini wewe ndio utakuwa faraja yake, furaha yake na tulizo la moyo wake sasa iweje umgeuke na kuanza visa na mikasa? Mapenzi ni kupendana, kuvumiliana, kurekebishana, kusaidiana, kushauriana na kuelekezana pasipo mambo hayo hakika ndoa/uhusiano wenu lazima utavunjika na kuwaachia vidonda vya moyo.
Leo ni siku yangu ya kuzaliwa, nimependa kuwakumbusha mambo hayo ya muhimu.