Wanawake wengi sana wameangamia kwa kukosa MAARIFA Yaani pindi anapokuwa amepevuka hitaji kuu la MWANAMKE ni KUWA NA FAMILIA👪
Kwa hakika Familia haiwezi kujengwa bila MUME NA MKE na hapo ndipo palipo na mtihani namna ya kuijenga FAMILIA ILIYO BORA na sio bora familia, Hapa hapana mjuzi wala mjuaji bali inategemeana na rehema za MUNGU ili kupata hitaji sahihi.
Kwenye MAHUSIANO Kuna DARAJA kubwa sana ama la kukuvusha kuelekea kwenye NDOA ama KUKUHARIBIA NDOTO ZAKO!
Nikisema Mahusiano ni DARAJA la kukuvusha kuelekea kwenye NDOA namaanisha kwamba NDIYO MWANZO WA KUMPATA MWENZA na nikisema kwamba Mahusiano yanaweza kuwa DARAJA la kuharibu ndoto zako namaanisha kwamba UKIKOSEA KUCHAGUA BASI WEWE NDO IMEKUGHARIMU MAZIMA.
Mwanaume akikosea kuoa na akajua anaweza kubaki kuhudumia familia yake japo nalo ni mpaka umpate mwenye MOYO huo, Ila Mwanamke akikosea kuolewa na akajua kwamba AMEINGIA CHOO CHA KIUME basi ataishi maisha ya UNYONGE mpaka MUME afe ðŸ˜
Wanawake wengi wamedumu kwenye MAHUSIANO mazuri na kuyafurahia sanaa ila walipoona hawaombwi kuolewa walihisi hawako mahala salama, Eti kwa sababu Mwanaume hajasema;
"MANKA NAOMBA UWE MKE WANGU"
Basi unaishi nae kijanja, Ili siku akija Mwanaume akatamka NDOA huyo ndo unamuona anakufaa na kumuacha mtu ambaye ulidumu nae kwa muda mrefu na ulimpenda kwa DHATI yako.
Hapa ndipo mnaangukia wanawake, Yaani shauku yako ilikuwa NDOA ila jamaa hakuwahi kuonyesha kama anahitaji uwe Mke wake ukajua amependa mpakato tu wala hana FUTURE na kumbe mwenzio alijua muda wake bado na ndani yake akiamini wewe ndiye mkewe 😅😅
Kwa sababu neno NDOA linaanzia nje wewe unalibeba mpaka ndani ya NDOA ukiamini unayoyaona leo ndo yatakuwemo kwenye NDOA masikini wa MUNGU kumbe unacheza na MPIGA LAMLI aliishajua unahitaji NDOA na akajua uko na Fulsa akaichangamkia, Hamad unakuja kushituka Una mimba ya miezi 6 unajigundua na kubaini ULIKOSEA UCHAGUZIðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜
Yule ulimuacha kwa kutokukuambia UWE MKE WAKE sasa amefikia uamuzi wa kuoa na AMEOA kwa mtazamo wa ndoa yao unabaini MKEWE ANAYO AMANI KWENYE NDOA YAKE wewe ukipitia MAGUMU hapo ndipo unabaini wazi wazi PAPARA YAKO IMEKULA FURAHA YAKO😂
Mjuage kusoma ALAMA ZA NYAKATI kuliko kutaka NDOA maana ni jambo linalotokana na uhitaji wa Mwanaume Wala sio wewe, Madhara ya kulazimisha NDOA yamewaliza wanawake wengi, Wamejikuta wanalea watoto peke yao na Mume yupo, Wengine ndo kwanza wanahudumia mpaka waume zao ili kulinda NDOAðŸ˜
MTAKA NYINGI NASABA HUPATA MWINGI MSIBA⚖
#Elista_Kasema_ila_Sio_She