π·π·π·π·π·π·π·π·π·π·π·
πΏMkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.
πΏUsivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.
πΏUsiruhusu mtu yoyote amwite mwanao βMchumbaβ, βMke wanguβ au βMme wanguβ.
πΏKila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi....
πΏKama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
πΏInashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
πΏMwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.
πΏMfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.
πΏMwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.
πΏUsipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!!