-->

DALILI 10 KWAMBA MWANAUME MPYA ANAKUTUMIA KUMSAHAU X WAKE NA AKIMALIZA ANAKUACHA!


Moja ya vitu vigumu kwa wanawake ni kuanzisha mahusiano mapya, inakua ngumu kwakua wanawake ndiyo hutongozwa hivyo kwao ni ngumu sana kujua kama mwanaume anayemtongoza anania ya dhati naye au anataka tu kumtumia. Kuna vitu vingi vya kuangalia lakini leo naomba nizungumzie dalili yakuwa mwanaume uliyempata hana mpango na wewe lakini anakutumia tu ili kuweza kumsahau X wake aliyemuumiza na hata ujitahidi kumlamba miguu kuna uwezekano mkubwa wa yeye kukuacha.
(1) Ametoka kuumizwa/Kuachwa; Wiki moja, mbili au mwezi mmoja uliopita alikua katika mahusiano siriasi, walikaribia kuoana au walishatambulishana au watu wanajua ni mpenzi wake, kazini wanajua, mtaani na ndugu wanajua. Lakini ghafla kaachwa, mwanamke unasikia labda kaolewa na mwanaume mwingine, au kamuacha yuko na mwanaume mwingine au hata hana mwanaume mwingine lakini yeye ndiyo kaachwa. Anaonekana kabisa kuumia, ana mawazo, anamzungumzia sana au hata hataki kumzungumzia.
Wakati mwingine likitajwa jina la huyo mwanamke anakasirika kutukana au mood yote inapotea. Walishafanya mambo mengi pamoja ila kaachwa. Unamuona kabisa anaugulia, hapo dada yangu mwanaume kama huyo akikutongoza jua kuwa anataka kukutumia kumsahau na akimsahau anaweza kukusahau na wewe au hata asimsahau mwanamke akitaka kumrudia atakubali na wewe utaachwa. Nirahisi kuwatambua wanaume walioachwa kwani wanakua wanalialia, hasira na utasikia tu mtaani kua makini sana naye.
(2) Anakupost mara kwa mara katika mitandao ya kijamii; Najua mnapenda na mnasikia rah asana kuona labda yuko siriasi na wewe. lakini dada yangu, kama mwanaume ndiyo katoka kuachwa au kuahcana na mpenzi wake, wiki mbili tatu tu mmekutana hata hujamkubalia vizuri kashaanza kukupost, mara Instagram, Facebook, status zote ni wewe, yaani kila mahali ni kama anakutangaza basi jua kuna mtu anarushwa roho. Wanaume siriasi huchukua mud asana kumpost mwanamke katika mitandao kwani kwanza hawapendi na pili wanataka kumjua kwanza, ila kama kila dakika unapostiwa tena wakati mwingine na vijembe, acha kushangilia hupendwi unatumiwa tu kumruha mtu roho.
(3) Kila saa na mihasira ya ajabuajabu; Wakati mwingine hata wewe huelewi kwanini kakasirika, kila wakati kanuna na ukikosea kidogo ataongea mpaka basi, unaweza kuongeza sauti kwenye TV akaongea kana kwamba amekufumania, anahasira na utasikia manano kama “Wanawake wote mko hivi…mimi namuamini Mama yangu tu…kama na wewe unaweza ondoka…” kunakua na mihasira na utumbo utumbo mwingi ambao hata huuelewi umetoka wapi. Anaweza asikutafute wiki na asijali ukimtafuta kanuna au anakujibu mbovu bila kujua ulimkosea wapi? Ishu sio wewe dada yangu, ana hasira zake za kuchwa huko anazihamishia kwako kwakua hawezi kumfuata X wake.
(4) Kila saa anazungumzia mabaya ya X wake; Wewe unaweza kudhani labda ni jambo zuri, ukaona kuwa anakupenda na yule anamchukia, lakini mwanaume ambaye kamuacha mwanamke na kamsahau hawezi kumzungumzia. Lakini kama kila saa flani alikua mchafu, falani alikua na tabi mbaya, alikua hivi,a likua vile, alikua hapendi hiki sijui kile. Anakusifia lakini kwa kukulinganisha au kutaja baya la X wake. Ndugu yangu huyo bado anampenda na anamihasira naye, nikwamba anamtukana tu kwakua anampenda na wewe wala hakujali, anakutumia kutoa hasira zake na kumsaidia kumsahau.
(5) Kila wakati anakulinganisha na X wake; Hii ndiyo inaboa, sasa hapa kila kitu unachokifanya anakulinganisha na X wake, yaani kama huyo X alikua malaika. Mara “Mimi napenda hivi mbona flani alikua ananifanyia hiki…tukitoka nataka uvae kama flani…kwanini usiwe unafanya hivi kama flani…flani yeye alikua anaweka hivi na vile!” wengine hata wakati wa kuvunjana wanamtaja huyo flani, dada kama jina la huyo X wake halimtoki kila kitu anataka ufanye kama flani basi jua wewe unatumika tu, wew ni ‘Kaimu Mpenzi’ siku akikaa sawa au mwenye mali akirudi unaachwa.
(6) Bado anaongea na X wake pamoja na kumuumiza; Anamuongelea mabaya, anakuambia kuwa kamuacha lakini kwenye simu yake namba bado ipo. Akipiga anapokea na kama akiwa na shida basi atataka kumsaidia bila kujali kuwa inakuumiza au la? Umshaongea sana kuhusu kukata mawasiliano naye lakini hajali, anakuambia kuwa hakuna kinachoendelea lakini kama ikitokea hata mkakwaruzana na X wake basi lawama zote ni wewe kuwa una mdomo na usingemchokoza basi asingekutafuta, ndugu yangu huyo mwanaume hajamsahau na wewe ni mpenzi msindikizaji.
(7) Nimapenzi ya Kuvunjana tu na kuwa chumbani chumbani; Mara nyingi anakuita kwaajili ya ngono tu na mambo ya chumbani, hataki muongee mambo ya maana, hapa si maanishi ndoa, hapana wanaweza kutaka kuoana hata kesho yake lakini ni mambo kama kuwa rafiki, kuongea, kuzoeana na kukutana bila kufanya mapenzi. Kila mkikutana naye basi unaona ana stress na anataka kufanya mapenzi na wewe, hamuwezi kuzungumza kama watu, kama wapenzi bila kutaka kufanya mapenzi na wewe na kufanya kwenyewe anakua kama anakubaka kwani hakuandai na haonekani kama yuko kwenye mood nzuri.
(8) Rafiki zake wanakushangaa au wanamsangaa; Hapa angalia sana, kuna rafiki zake ambao walikua wanajua kuwa ana mwanamke, hawkaujua kuwa kaachana naye au hawaamini kama ataachana naye, wanahisi kuwa atarudiana naye, hawa ukikutana nao akilazimisha kukutambulisha basi watashangaa watakukubali lakini ukiangalia nyuso zao ni kama wanasema kweli umechana na flani? Wanajua alijkua anampenda sana hivyo wanashangaa labda kuwa kamsahau haraka au hata wanashangaa inakuaje anakua na mwanamke kama wewe yote haya yachunguze.
(9) Ana haraka sana ya ndoa; Hii mara nyingi hutokea kwa wanaume ambao wameumizwa sana na wameachwa mwanamke akaenda kuolewa au ana mtu mwingine. Hawa hupenda kuwakomoa ma X wao kwa kuoa mapema ili waonekane kuwa ni vidume hawajaumia. Umekutana na mtu hata mwezi hamjamaliza ashakutambulisha mpaka kwa mashamba ya mpunga huko kwao kuwa ni mpenzi wake,a nataka kuja kwenu na anataka kukuoa, dada chunguza unakuta kaachwa na X wake basi jua kuwa hana mpango na wewe bali kuna mtu anamkomoa huko.
Mwanaume wa namna hii ambaye hata miezi miwili haijaisha tangu kuachwa au mwaka umeisha lakini X wake kaolewa na yeye unaona umekutana naye ana mchecheto wa kukuoa basi jua hiyo ndoa itaisha pale akimsahau au pale ambapo X atapiga simu, hata kama tayari atakua katika ndoa lakini bado huyu mwanaume hawezi kumuacha. Usikimbilie sana ndoa ya namna hii, mtu hajapata hata muda wa kuumia, kutafakari na kukubali kuwa nimeachwa basi anaanza kutaka kuoa basi kuna walakini, hakuna ndoa hapo bali kuna kisasi cha ndoa.
(10) Anabadilika Ghafla; Alikua ni mtu wa kukutambulisha kila sehemu, katika mitandao na kwa marafiki tena kwa mbwembwe, lakini ghafla unaona kila kitu kimebadilika, hakuna kutambulishana, hakuna kupostiwa na ukiuliza kama si kipigo ni minuno na matusi. Hapa kuna mambo mawili, kwanza inawezekana kuwa akili zishamrudi ametambua makosa yake hivyo ameamuaa achane na wewe lakini hujamkosea hajui namna ya kukuacha hivyo anaanza kisirani lakini pili labda X wake kajirudi anataka warudiane na anataka asikuache kwa kukuumiza kama alivyoumizwa yeye hivyo anataka wewe mwenyewe ujitoe mapema na lawama ziwe zako.
Anakua na kisirani ili na wewe ujiongeze na kujitoa au mgombane aseme humfai akuache lakini wewe ujione kama ndiyo mwenye makosa. Akianza hivi basi jua kuwa ushaachwa muda mrefu hivyo jiongeze mapema, angalia matendo yake na si maneno. Najua kuwa ni ngumu na siwezi kukufanyia maamuzi ila naamini umenielewa na kama umesoma mpaka hapa, ana hizo dalili na abdo unahamu ya kung’ang’ania kwamba labda utamfundisha akupende, basi soma Kitabu changu cha “Ndoa Ynagu Furaha Yangu” angalau ujifunze namna ya kujipenda wewe kwanza.
Mimi nishamaliza ila hakikisha unafuatilia Makala zangu kama hizi Iddi Makengo
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU