-->

BARUA YA SEID KWA MADADA ZANGU WOTE WA MJINI.

Image may contain: 2 people

Dada Zangu vipenzi.. mdogo wenu nawapenda sana ndio maana nimewaandalia hii nakala muweze kujifunza japo kwa asilimia chache.. mdogo wenu sina elimu ya digree lakini naweza kuandika somo zuri mkajifunza kutokana nalo..

Nimeyaona haya na kuamua kuyaepusha kwa kuwafikishia ujumbe ili nisije kuwa na kesi kubwa kwa Mungu. Dada zangu najua wengi mmezoea kuvaa nguo ambazo zinawaachia uhuru wa mili yenu. Kwa kiswahili cha hekma tunasema nguo fupi fupi au ambazo hazijaruhusiwa kidini. Na kwa kwa kiswahili cha mtaani tutasema Vichupi au nusu uchi. Naomba usichukie wala usinichukie kwani ni moja ya njia ya kujifunza. Dada yangu hakuna kitu kinapendeza mbele ya jamii kama kuvaa nguo nzuri ya kuuficha mwili wako. Dada yangu hakuna kitu kitachokufanya uwe na muonekano mzuri na kuwafanya wanaume waliostaarabika wakutolee macho kama kuvaa sketi nzuri ya kuendana na mwili wako. Dada yangu kuvaa mavazi yanayouacha mwili wako nusu uchi ni kukaribisha maradhi nyumbani kwako. Dada yangu ukivaa nguo zinazoonesha maungo yako ya ndani ni kusababisha hatari ya maisha yako kwani hakuna mtu mzima ataekusema vizuri.

Utaitia aibu familia yako. Kila ataekuangalia ataitupia lawama familia yako. Utakuwa na mikosi ya kila sehemu sababu ya watu kukusema vibaya. Wala usije ukaona unapita sehemu na kuwageuza watu ukasema acha niwakomeshe. Unakuwa unajikomesha wewe mwenyewe.. utaonekana malaya hata kama sio malaya... DADA YANGU UKITAKA KUISHI VIZURI NA WATU JIEPUSHE NA NGUO ZA AIBU.. UONEE HURUMA MWILI WAKO KWA KUUFANYA KILA MMOJA AUONE BILA SABABU ZA MSINGI....

DADA YANGU JIEPUSHE NA VIKAO VISIVYOKUWA NA MAANA.. SABABU KWENYE VIKAO VYA KIPUMBAFU NDIPO KUNA UJINGA MWINGI USIOKUWA WA KIMAENDELEO...

Dada Yangu jiepushe na wanaume za watu, onyesha heshima kwa wake zao. Ndoa ni taasisi iliyotengenezwa na Mungu mwenyewe tokea kuumbwa kwa misingi ya Dunia. Usiruhusu mwili wako utumike kuharibu ndoa ya watu. Usiruhusu mwanamke mwenzako adondoshe chozi lake kwa sababu yako, alie na kujuta kwanini aliolewa hiyo ni laana kubwa. Najua maisha ni magumu na mnataka kitonga ila Haijalishi ni kiasi gani huyo mwanaume anakusaidia kimaisha, muepuke, sio wako. Tulia na wa kwako na Mungu wetu wa rehema atakubariki. "Karma is a bitch"- kuna wakati wa malipo! msije sema sikuwaambia!...

Dada zangu msione tunakaa kimya bali mambo mnayoyafanya ni mabaya sana. Na uenda kwa mara moja au nyengine yanapelekea hasira za Mungu kuja juu na kushusha mabalaa yaliyokithiri kwenye dunia..

Vitabu vya dini vinasema.. Mwanamke asivae mavazi yatayomfananisha na mwanamume. Wala mwanaume asivae mavazi yatayomfananisha na mwanamke. Lakini leo imekuwa kanuni. MWANAMKE HAISI KABISA KAMA AMEPENDEZA IKIWA HAJAVAA SURUAL... hilo sio vazi lenu dada zangu. Lipo vazi lililoumbwa kwa ajili yenu ili mfanye stara ya kila kona kwenye maungo yenu...

YANGU NI HAYO KWA LEO... NAOMBA MNISAMEHE KWA KUYAONGEA HAYA KWANI NAJUA WAPO BAADHI WASHAJIANDAA KUNICHUKIA...

Usinune kwa sababu ukweli unauma... na bila shaka hata kama unafanya hivyo na umeusoma huu ujumbe.. ikiwa akili zako ni timamu unajua kabisa nakuwa nakosea bali tu ni udigital uliosababisha misingi ya dini zote iingie makwapani....

MUWE NA MCHANA MWEMA....
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU