Unajua Mwanaume ni tofauti na Mume na ndo maana wanawake wengi mnapata taabu sana kwa sababu NDOTO YENU NI KUWA NA MUME ila dunia imewapa UPOFU hata mkashindwa kutofautisha baina ya MUME NA MWANAUME.
Macho na mtazamo wenu umeangukia kwa MWANAUME kutokana na namna wanaume wamejua kuliteka SOKO LA MAPENZI kila mnapojaribu kupepesa macho ili muone ni nani zaidi mnajikuta MNAPATA BP YA MACHO maana kwa sasa WANAUME wote wamejua ugonjwa wenu mnachagua sana hivyo vijana wamejipanga kujikoki🚰 kwa mavazi ili wawavutie na hapo ndipo mnakutana na MWANAUME badala ya MUME.
Mume anapatikana kwa UTASHI WAKE kwamba anakuja kwako akiwa na shauku uwe MKE WAKE wakati huo Mwanaume anapatikana kwa UMARIDADI WAKE na hapo ndipo mmeshindwa kubaini njia sahihi na badala yake MNAJIBEBEA MWANAUME YEYOTE ili mradi anajua kuvaa na akapendeza eti mashoga wamsifie, kila MUME anatokana na zao la MWANAUME lakini sio kila Mwanaume anaweza kuwa MUME Kwani katika hali ya kawaida Wanaume wengi hawakui na badala yake wanafikiria zaidi MDINYO na wengine kuwazia MTEREMKO kwa kummiliki Mwanamke mwenye NAFASI ili kupata KIVULI ☔
Mwanamke Acha kujilengesha kwa Mwanaume ili akuoe bali msubiri MUME ambaye atakuhitaji uwe Mke wake ina heshima lakini Kuna DHAMANA YA UPENDO WA DHATI.
#Elista_Kasema_ila_Sio_She