-->

*MBINU NA SIRI YA KUFANIKIWA KIUCHUMI MAISHANI MWAKO*

UTAMU KITANDANI APP
Kwanza kabisa tambua ndoto yako Ni nini au unataka kuwa nani ktk maisha yako.
Panga malengo yako,
Weka mipango ya kufanikisha ndoto yako,
Weka utekelezaji wa mambo uliyopanga,
Simamia mipango yako kikamilifu bila kulegeza wala kupunguza Kasi,
Usiache fursa yoyote ikakupita bila kuifuatilia, hakikisha unaifuatilia hadi mwisho ili ujiridhishe.
Pia penda kusoma vitabu mbalimbali vya kiuchumi, kijasiriamali, mambo ya fedha, pia unaweza kutumia simu yako Kama silaha ya kuufuta umaskini Maishani mwako.
Usipuuze fursa yoyote Ile, pia usisikilize maneno ya watu Wala kuhisi kuwa watakuonaje.
Bali fanya utafiti wa kina kuhusu kina fursa yoyote kabla ya kuifanyia kazi ili ujiridhishe Kama Ni ya kweli au hapana, ukishaona kuwa Ni ya kweli na itakulipa fanya bila kuogopa chochote au mtu yeyote.
Kingine ili ufanikiwe kimaisha, inabidi ujifunze kwa waliofanikiwa siyo walioshindwa.
Maana walioshindwa maisha watakukatisha tamaa kuwa haiwezekani kupata mafanikio ktk kitu fulani unachotaka kufanya wakati huenda yeye alishindwa kwa kufanya fulani au kukiuka kanuni za mafanikio ya jambo hilo bali waliofanikiwa watakupa mbinu za kufanikiwa ktk maisha yao.
Jambo jingine Kama unataka kufanikiwa ktk maisha yako,
jifunze kuwa na msimamo mkali ktk maamuzi yako unayofanya hasa ukishagundua na kujiridhisha kuwa unachotaka kufanya kina manufaa kwako au jamii Wala usikubali mtu au kitu fulani kikuyumbishe ktk maamuzi yako hasa pale unapogundua kuwa jambo unalofanya lina manufaa kwako au kwa jamii yako inayokuzunguka,
maana binadhamu tunafanana kwa nje tu ila kwa kifikra na kimaono pamoja na kimtazamo tunatofautiana sana tena mbali sana.
Focus yako si sawa na ya mwingine, kumbuka kuwa maisha yako Ni dhamana yako.
Hivyo hakuna atakaayekujali au kuyajali maisha yako Kama wewe hauyajali,
Mwisho kabisa uwe mkweli na muwazi kwa watu wako wako unaofanya nao kazi halafu mwombe na kumtdnguliza Mungu ktk kila jambo unalofanya.
Nakuhakikishia kuwa ukifuata kanuni hizo utapepea juu tu Kama tai, nakutakia mapambano na maisha mema yenye mafanikio tele.
Share:

πŸ’‹JAMANI GOLI LA ASUBUHIπŸ’‹ πŸ’‹LINAUMUHIMU WAKE πŸ’‹MPE MUMEO GOLI TAMU LAπŸ’‹ πŸ’‹ASUBUHIπŸ’‹

UTAMU KITANDANI APP
😍
 Mwanaume aliyekamilika lazima aamshwe asubuhi. Tena siyo kwa kurukaruka, la hasha! Mwamshe kwa utulivu,unapomwamsha mumeo asubuhi kwakumpa k.....a asubuhi na mapema kabla hamjatoka kitandani..... unajuwa kinachomtokea? moja utamwondolea uchovuπŸ‘ŒπŸ½utamchangamshaπŸ‘ŒπŸ½nakumfanya mwepesiiiiii na hapo atakuwa tayari kwa ujenzi wa taifaa hata chapa kazi hatari
😍Nadhani mpaka sasa ushajuwa mumeo unamwamshaje si ndio eee haya tuendelee
Na hii inawahusu hasa wale wanawake wanao amka nakujifanya wapo bize kazi ndo kila kitu hivi ngoja niwambie mumeo akitoka akaenda kuamshwa na wenzio huko nnje hiyo kazi unayokimbilia mbiombio nakuiwaza muda wote itafanyika mwingine akiwa na mabiashara ndo kabisaaa ukiuliza oooh mzigo umepanda mzigo umeshuka ooooh madeni ooooh nyoho nyoho fulu kujipa ubizee akidakwa huyo na wadakaji waliotoka kufundwa kwenye JUMBA LA MAHABA wakafundikaaaaaaπŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½ shogaa atageuka huyo atakukumbuka huyoo ....hata hizo biashara unazozizungumzia nakujipa ubize nazo utazifanya kweliiiii he he heeeeee halloooooo shaulilooooπŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½
😍😍Mwingine anakurupuka SAA kumi za usiku ukiuliza nn anawahi usafi wa nyumba eti mume amuone ni msafii acha mambo hayo we we mpe mumeo kiamshiooo ,unapoacha kumuamsha mumeo unamwacha na uzito wake anashindwa Ku Fanya kazi kwa ufasahaa.kazi kwenu wavivu wajuzi wa kazi maofisini mahodari wa biashara na wale wanaomkia vibarazani mwa watu nakuwacha waume zao ndani kwenda kupiga umbea,mume kwanza ndo aliekutowa kwa wazazi wenuuu au shuri zenuu.
😍😍Naomba nitowe angalizo hapa simanishi kila siku eee maana hapa kama nawaona macho yalivyowatoka mlivyowapania watoto wawatu unaweza ukamwamsha Mara tatu kwa wiki pangilia vzuri siku zako za kumuamshaa hizi siku tatu unaweza ukazipanga na kuzichaguwa zile siku unazohisi atakuwa bize sana kazini we ndo unampunguzia uchovuu ,mm nimekwambia tatu lakini unaweza kwenda siku saba kama kama unanguvuu ahahahhaha upo

 πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½

Unamwamshaje?amka alfajiri anza uchokozi kwa kumuamsha taratibu tenshuo ndo muda wa kumwonyesha utalaamu wako wote na kumfanya hawe tayari kupokea kiamshio toka kwako ,maana muda uwo ye atakuwa na mawazo ya kazi tu hivyo utamsaidia kumfanya amke akiwa mchangamfuuu πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½
😍😍Mwisho nakukumbusha kuwa karibu na haziba wako hii itakusaidia kumjuwa vzuri mkikaa pamoja mguse guse mpapasee hii itamsaidia kumfanya akutamanii muda wotee πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½haya mie nishatimiza wajibu wangu kukukumbusha kazi nakuachia weweeeeee πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½
πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½πŸ‘ŒπŸ½
Share:

MAMBO YANAYOSABABISHA MIGOGORO KWENYE MAHUSIANO AU NDOA

✍️Kuna vitu vingi ambavyo husababisha ugomvi na migongano ndani ya mahusiano ya Mume na Mke na hapa naeleza sababu kuu ambazo kwa kawaida hutokea karibu katika kila mahususiano
πŸ‘πŸΎ Wivu na Kukosa Kujiamini
Wivu unatokana na jinsi ambavyo Mwanandoa mmoja anavyohusiana na watu wengine wa jinsia tofauti. Inaweza ikawa marafiki,wafanyakazi wenza au wapenzi wa zamani. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba wivu unasababisha ugomvi katika mahusiano mengi.
Kunatakiwa kuweka mipaka ya kutosha na iliyo wazi ili kujenga uaminifu kwa Mume/Mke wako na kumpa kujiamini. Mwanandoa ambaye hajiamini ni tatizo kubwa kwani uwezekano wa kuanzisha ugomvi ni mkubwa.Hivyo ni vizuri ukamjengea Mume/Mke wako katika mapenzi kujiamini kwa kuwa mwaminifu.
Uaminifu ni kitu kimoja kikubwa sana katika Ndoa πŸ  Kama Mume/Mke wako akikuamini hakutakuwa na wivu wa kupita kiasi na pia atakuwa anajiamini kuwa yeye peke yake ndio chaguo lako na hakuna mwingine.
πŸ‘πŸΎ Mawasiliano Finyu
Mawasiliano yanapovunjika katika mahusiano ugomvi ni kitu cha kawaida kutokea.
Mawasiliano ya kawaida kati ya Wanandoa husaidia sana kutoa wasiwasi wa nyendo za Mume/Mke wako. Huleta amani na kujenga uaminifu kwa Mpenzi Mume/Mke kwako.
Kuzungumza juu ya mipango yako ya mendeleo kama ujenzi au biashara ni vitu ambavyo ni muhimu sana kuvifanya vinginevyo utajenga wasiwasi kwa Mume/Mke wako na itasababisha ugomvi wa mara kwa mara.
Kuwa muwazi kwa mipango ya maendeleo binafsi,ya familia yako na ndugu.
Utafiti unaonyesha kuwa Wanandoa wanaoongea na kusikilizana mara kwa mara hawagombani mara nyingi kama wale wasio na mawasiliano ya kutosha.
πŸ‘πŸΎ Masuala ya Fedha
Japokuwa fedha si msingi wa Mapenzi katika Ndoa,lakini ni kitu ambacho kinahitajika sana katika maisha ya kila siku ya kila mtu na ya familia. Na kimekuwa ni mojawapo ya vitu ambavyo Wapenzi katika mahusiano ndoa hugombana sana juu yake.
Mwenza mmoja anapokuwa mtumiaji mbaya wa fedha na mwingine siyo,huibua malalamiko na ugomvi. Baadhi ya Wapenzi Wanandoa hasa Sisi Wanawake hatutaki kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya msingi ya nyumbani na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa Wanaume.
Hili linaibua malalamiko mengi kwa baadhi ya Wanaume,na wakati mwingine toka kwa Wanawake kulalama juu ya Matumizi mabovu ya pesa kwa Waume zao. Matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya pombe na sharehe nyingine kwa baadhi ya Wanaume na baadhi ya Wanawake kumekuwa mojawapo ya sababu za ugomvi juu ya fedha katika mahusiano.
Ni muhimu kwa wenza wawili Wanandoa kupanga jinsi ambavyo fedha zao zitapatikana na kutumika. Vipaumbele vya kufanyika kwanza na kiasi cha kutumika kwajili ya starehe na urembo kwa Wanawake kwa mfano.
πŸ‘πŸΎ Masuala ya Familia
Familia ya nani ianze kwanza na ipi ifuate ni tatizo kubwa katika mahusiano. Upendeleo wa upande mmoja ambao kwa asili huwa unatokea tu ni chanzo cha ugomvi ndani ya nyumba.
Mitazamo tofauti kati ya mmojawapo katika Wapenzi Wanandoa na familia ya mwenza wake husababisha kutoelewana kwa Wanandoa hao ndani ya nyumba.
Mbaya sana inakuja pale Wanandugu wanapoingilia mambo ya ndani ya nyumba yenu. Wazazi wa Kike na Mawifi mfano, wamejulikana kusababisha matatizo mengi kwenye familia za Watoto na Kaka zao.
Kuepukana na hili ni muhimu kwa Wanandoa ndani ya nyumba kuweka mipaka kwa ndugu ambayo haitaathiri uhusiano nao kama ndugu.
Pia ni muhimu kwa Wanandoa hao kuweka mikakati ya pamoja juu ya kuhusiana nakusaidia ndugu toka katika familia zao mbili.
πŸ‘πŸΎ Suala la Unyumba
Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa Wanandoa ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa Wanandoa hasa ambao wana uhitaji tofauti.
Wengine wanaona kama Mume/Mke ambaye hahitaji kufanya mapenzi mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.
Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni tatizo jingine kubwa katika mahusiano ya NDOA kama nilivyoonesha mwanzoni.
πŸ‘πŸΎ Vipaumbele katika Maisha
Wapenzi Wanandoa wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.
Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.
πŸ‘πŸΎUaminifu
Uaminifu katika mahusiaono ni jambo la muhimu sana. Bila uaminifu ni ngumu sana kwa mahusiano yoyote kudumu.
Uaminifu ni kitu ambacho hujengwa kwa muda mrefu na kikipotea ni ngumu sana kukirudisha. Japo inawezekana kujenga upya uaminifu lakini huchukua muda mrefu sana.
πŸ‘πŸΎWapenzi,Marafiki na Maisha ya Zamani
Mojawapo ya vyanzo vya ugomvi kati ya Wanandoa ni wapenzi wa zamani. Mawasiliano ya aina yoyote na wapenzi wa zamani huleta wasiwasi mkubwa kwa mpenzi wa sasa. Ni kitu ambacho wapenzi wawili Wanandoa wanahitaji kuongea na kupanga jinsi ya kuepukana na matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na historia zao za maisha ya zamani.
Kuepukana na hii ni vyema kuvunya uhusiano wa aina yoyote na wapenzi wa zamani labda tu kama wapenzi hao ni wazazi wenza au mnafanya kazi pamoja na ni ngumu kutokuonana au kuwasiliana.
Suala linalofanana na hili ni uhusiano na baadhi ya marafiki wa jinsia moja ambao wanachukuliwa kuwa mfano mbaya na mpenzi Mume/Mke wako. Kama haiwezekani kutowasiliana na kuonana na wapenzi wa zamani au marafiki, basi ni vyema wakawa marafiki wa familia nzima na mawasiliano yoyote kati yenu nao yawe wazi pasipo kificho.
πŸ‘πŸΎWatoto
Suala la uleaji na ukuzaji wa watoto linasababisha ugomvi mara nyingi kati ya Wazazi. Jinsi gani mtoto avae au shule ipi aende linapelekea Wazazi wengi kugombana.
Ni jambo la muhimu sana kukubaliana juu ya mambo ya msingi juu ya malezi ya watoto. Tofauti za Wazazi ziangaliwe kwanza vinginevyo zitaingilia malezi ya Watoto na kusababisha ugomvi juu yao.
πŸ‘πŸΎKazi za Nyumbani
Imekuwa kama utamaduni kwa Waafrika kuacha kazi nyingi kama si zote za nyumbani kwa Mke. Kwa Wanawake ambao wanafanya kazi pia inakuwa ngumu sana. Hili linasababisha pia ugomvi kwa Wanandoa nyumbani. Kama nguo ambazo Mume anazivaa na kuzichafua tu bila ya kujali kuwa Mke wake ataumia wakati wa usafi na ikiwa yeye mwenyewe hajishughulishi na kufanya baadhi ya kazi za nyumbani ni wazi itasababisha ugomvi.
Ni vyema Wanaume kuchukua baadhi ya majukumu nyumbani hata kama kutengeneza bustani au kulisha chakula mifugo.
,☑️Japokuwa ugomvi ni kitu cha kuepuka,lakini kina uzuri wake katika mahusiaono kama kikichukuliwa vizuri na kutumika kama kioo.
Kama mtu anagombana na mpenzi Mume/Mke wake kwa madhumuni ya kuboresha ni kitu kizuri. Hii inaonesha kuwa anahitaji kuwa na Wewe na anahitaji amani.
☑️Ugomvi na mifarakano pia inatoa nafasi kwako kujiangalia vizuri na kama kinacholalamikiwa na Mume/Mke kina ukweli basi ni nafasi ya kujirekebisha.
Ni mategemeo kuwa kuna kipindi ambapo ugomvi utakuwa mkubwa na baadae Wanandoa hao wataelewana na kurekebisha mambo yao.
πŸ‘‚ Ugomvi Unatoa Nafasi ya Kuongea Mambo Magumu
Wakati mwingine mazungumzo ya kawaida hayatoi nafasi ya Wapenzi Wanandoa wawili kusema yale ya ndani na yanayozizonga nafsi zao.
πŸ‘‚Ugomvi hufungua milango ya hisia za ndani na huenda vyanzo vya matatizo vikawekwa wazi na hivyo kufanyiwa kazi.
πŸ‘‚Ugomvi unaonyesha Kuwa Mnajali na Mnataka Maboresho
Katika uhusiano ambao Wanandoa hawajali,au hawana malengo ya muda mrefu huwa hawatoi duku zao juu ya utofauti na Waume/Wake zao.Hivyo Wapenzi Wanandoa wanaogombana wanaonesha kuwa wana nia ya dhati na Waume/Wake wao na sio tu kupitisha muda.
πŸ‘‚Ugomvi Unaboresha Uhusiano
Kwa kweli ugomvi unaibua hisia zilizojificha toka kwa Wapenzi Wanandoa ni wakati mzuri kuona matatizo ya kila mmoja. Na kama Wapenzi Wanandoa hao wana nia ya dhati ya kuwa pamoja basi watafanyia kazi tofauti na mataizo waliyonayo. Hivyo kuboresha mahusiano yao
Kuna sababu nyingine nyingi ambazo zinachangia ugomvi kati ya Mume na Mke katika mahusiano lakini haya ni yale yanayotokea katika mahusiano mengi.
❤️NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE NA MALAZI YAWE SAFI MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU (WAEBRANIA 13:4)

Stamina atoa somo ndoa yake kuvunjika - Mtanzania
Share:

#MKASA_HUU_UTAKUFUNZA_SANA_SOMA #UJIFUNZE_KITU.


Inasikitisha pole sana Irene
πŸ‘‡
Irene baada ya kufeli darasa la saba kule kijijini kwao #SONGEA alichukuliwa kufanya kazi ya HOUSEgirl jijini Dar es Salaam, alikua akilipwa elfu 40 kwa mwezi, elfu 20 alikua akiituma kwa Wazazi kijijini na 20 inayobaki anahifadhi akiba, nyumba ile alianza kukumbana na misukosuko ya kutisha ambapo Baba mwenye nyumba alikua akimlazimisha kufanya nae mapenzi wakati Mkewe na Watoto wakiwa hawapo nyumbani.
πŸ‘‡
Baba yule alimpa vitisho kuwa iwapo akitoa siri basi ndio utakua mwisho wake kukaa mjini, Irene alifikiria tabu za kijijini kwao akaamua kuvumilia, Baba yule alimpa zawadi na hela zingine za ziada kwa siri kubwa.
πŸ‘‡
Mtoto wa nyoka ni nyoka amini usiamini ila ndio hivyo, kijana wa kiume wa Baba mwenye nyumba ambaye alikuwa anasoma form 5 shule ya boys boarding akawa akirudi likizo anamlazimisha Irene kufanya mapenzi kwa vitisho vile vile kama vya Baba yake.
πŸ‘‡
Irene aliogopa sana mchezo ule mchafu anaofanya na Baba mwenye nyumba na mwanae Ali. "Hivi siku Mama Ali akijua itakuaje" alijiuliza kimoyomoyo Irene, miaka ilienda akivumilia unyanyasaji ule alipata mimba akaitoa ila bahati nzuri hakupata magonjwa, alipendeza sana Irene kwa namna familia ile ilivyomjali japo siri ya mapenzi kati yake na Baba na mwanae Ali hakuna aliyefanikiwa kuijua.
πŸ‘‡
Alitokea kijana mmoja ambaye ni dereva akajitambulisha katika familia ile na kumchumbia Irene, kwa niaba ya Wazazi wake kijijini familia ile iliridhia japo Baba mwenye nyumba alikubali kishingo upande maana ananyang'anywa tonge mdomoni, mahari ilitumwa kijijini Irene akaolewa.
πŸ‘‡
Mumewe alikua na kipato cha chini ilibidi Irene atumie hela zake alizokusanyaga kipindi cha HOUSEgirl kufungua kibanda chake cha kusajili lines pale Gongo la Mboto , siku moja alikuja kusajili line jamaa mmoja, "Naitwa Coplo Gama kusajili line ya tigo "Ni kiasi gani" Jamaa aliuliza baada ya kukaa. Irene alimjibu, "Elfu moja tu Kaka, kwani wewe ni polisi" Irene aliuliza. "Hapana mimi ni Mwanajeshi"jamaa alijibu. Wakati zoezi la usajili likiendelea, ghafla simu ya Irene iliita alipokea kumbe ni Wazazi wake waliongea kwa lugha ya KINGONI.
Irene alipomaliza kuongea na Wazazi wake Coplo Gama alimsikitikia na kumwambia, "Pole sana my kumbe mngoni mwenzangu, dunia ina shida sana ila hao ndio Wazazi wako na wanakutegemea huna budi kuwatumia chochote ulichonacho hata kama ni kidogo"
πŸ‘‡
Irene alihamaki kumbe Coplo ni mngoni na alielewa mazungumzo yote ambapo Wazazi wake kijijini walikua wakimlilia njaa na kumuomba awatumie japo chochote maana hali ni mbaya sana huko kijijini. "Kwani kwa mwezi unaingiza kiasi gani kupitia kazi hii⁉️" Coplo aliuliza. "Tigo wanatulipa laki 4 kwa mwezi" alijibu Irene."Umeolewa "Coplo aliuliza." Ndio, nina Mume na mtoto mmoja tayari "alijibu Irene." Hongera sana, una mtoto ila bado mrembo kweli kweli "Coplo alisifu." Asante"alijibu Irene.
πŸ‘‡
Maongezi yaliendelea hata baada ya zoezi la usajili wa line kukamilika, Coplo alimwambia Irene kuwa anataka amsaidie kumuingiza jeshini, Irene alifurahi kwa hoja hiyo akasema haina shida hata Mumewe atakubali tu maana ni mtu mpenda maendeleo.
πŸ‘‡
Baada ya kupeana namba za simu waliendelea kuwasiliana, ilipofika mwisho wa mwezi, Coplo alimwambia Irene aandae cheti cha kuzaliwa kopi 3, kitambulisho cha uraia kopi 2 barua ya ukazi kutoka serikali za mitaa yenye muhuri wa mjumbe na shilingi laki 3 na nusu kwa ajili ya fomu ya usaili jeshini.
πŸ‘‡
Irene alifanya yote hayo akishirikiana na Mumewe hela iliyokasoro akakopa. Coplo alimwambia Irene sasa aje nyumbani kwake siku ya Jumamosi pale Tabata ili ampe mbinu za kujibu maswali ya usaili apite moja kwa moja, Irene hakuuliza mara mbili alimuamini sana Coplo na kumchukulia kama ndugu na Kaka yake.
πŸ‘‡
Jumamosi alienda akakaribishwa ndani, baada ya story mlango ulifungwa, Coplo alimsogelea akaanza kumtomasa akamwambia, "Irene utanisamehe bure najua umeolewa ila kiukweli nakupenda sana toka siku ya kwanza nlipokuona, lazima nkusaidie uingie jeshini ila naomba japo nionje"
πŸ‘‡
Irene alibaki hajielewi alifikiri sana ila kwa kuwa ana shida na kazi alimkubalia. Baada ya mahaba mazito Coplo alimpa vijimaelekezo eti vya kujibu kwenye usaili. Irene aliondoka akiwa na huzuni ila akajipa moyo, ilikua siri yake moyoni hata Mumewe hakumwambia kuwa katafunwa.
πŸ‘‡
Baada ya wiki 3 Coplo akamwambia Irene aende tena nyumbani kwake akajaze fomu tayari ameshakuja nazo aje na passport 4 na damu kwenye kichupa kwa ajili ya vipimo ila akamsihi hatomfanyia chochote kama siku ile ya kwanza. Irene alienda akijipa moyo kuwa sasa zoezi linaelekea mwisho hivyo huzuni ile ya mwanzo itaisha, alipewa fomu za kujaza kweli ila baada ya zoezi Coplo akamfosi tena wafanye mapenzi kwa mara ya mwisho Irene hakuwa na cha kujizuia, alipigwa mtama chali kitandani akashughulikiwa.
πŸ‘‡
Irene aliondoka, baada ya mwezi Coplo alimuita, wakiwa sebuleni Coplo akijifanya analia na kusikitika alimwambia Irene, "Vipimo vya damu yako vimeonyesha uliwahi kutoa mimba kwa hiyo ombi lako la kuingia jeshini limekataliwa" Irene alihamaki, Coplo alimtimua, akiwa na huzuni zaidi,Irene njiani alilia sana akimlilia Mungu, "Kwa nini mimi eeh Mola⁉️" alifika nyumbani ila Mumewe siku ile aligundua Mkewe hayupo sawa, alimbana akamwambia, "Niambie kila kitu nini umefanywa huko na huyo Coplo‼️‼️⁉️ na kama huniambii nakupa talaka leo leo".
πŸ‘‡
Kwa uchungu huku akilia Irene aliamua kukiri yaliyotokea Mumewe alisikitika mno ila akamwambia, "YOTE HAYA NI SABABU YA SHIDA ZETU MKE WANGU, ILA MUNGU YUPO ATATULIPIA".
πŸ‘‡
Baada ya miezi kadhaa Irene alidhoofu kwa mawazo akifikiria muda na fedha alizopoteza kwa ajili ya utapeli wa Coplo. Irene aliugua alipopelekwa hospitali alipimwa na kukutwa amepata maambukizi ya virusi vya ukimwi, Mumewe pia alipima akakutwa nae ameshaambukizwa ukimwi, ilikua ni kilio kikubwa sana ila Mumewe alimfariji akamwambia, "USIJALI MKE WANGU, NAJUA UNAJUTIA KULETA MAUTI KATIKA NDOA YETU ILA NAJUA HUKUPENDA, ULIDANGANYIKA KUTOKANA NA UMASIKINI WETU, NAAHIDI SITOKUACHA NTAKUFA NAWE, USILIE TULIA TUMLEE MTOTO WETU HADI HAPO KIFO KITAPOTUFIKA".
πŸ‘‡
Irene alilia sana na kumuomba msamaha Mumewe, baada ya wiki 2 Irene alichanganyikiwa akawa taahira anazurura mitaani akilia, Mumewe alianza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARV na hadi muda huu anaendelea kumlea mtoto vizuri alozaa na Mkewe Irene.
πŸ‘‡
Skendo ile ilivuma wasamaria wema wakapeleka taarifa polisi Coplo akakamatwa akakiri akafukuzwa kazi kwa aibu baada ya mwezi mmoja akajinyonga akaacha ujumbe usemao, "NAFSI IMENISUTA, NMEDHULUMU NAFSI ZISIZO NA HATIA, BORA NIFE".
#Funzo
Kama wewe ni MWANAUME jiulize ni nafsi za WANAWAKE wangapi unazidhulumu au umezizulumuJiulize wewe ni kama Baba mwenye nyumba au , mwanae Ali au Coplo Gama
Tambua malipo ni hapa hapa duniani na MWENYENZI MUNGU πŸ‘‡ anakuona kwa dhuluma unazowafanyia WANAWAKE na MABINTI wa watu ipo siku utajutia.
Binti jiulize unatumia njia zipi kutatua shida zako⁉️ Je Unafanya kama Irene au
Ni vema binti kuepuka kutumia mwili wako kimapenzi kama njia ya kutatua matatizo yako yasijekukukuta matatizo makubwa zaidi hata ya hayo uliyofikiri unayatatua.
Kama umeguswa kwa namna moja au nyingine na mkasa huu na ungependa uwafikie watu wengi zaidi katika jamii tafadhali πŸ™ SHARE STRAIGHT AWAY WITHOUT DELAYS
πŸ‘πŸΎπŸ‘€πŸ‘‚#NZINGATIOπŸ‘‡
❤️ NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE NA MALAZI YAWE SAFI MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU
(WAEBRANIA 13: 4)
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU