Unamjua Mpenzi Wako?
1. Tambua kuwa mwenzi wako ni mtu na akili yake, na ana mawazo yake, mengi yakiwa ni yale mazuri kwa mahusiano yenu.
2. Usishinikize maoni yako ndiyo yafuatwe. Kuzungumza pamoja kutaimarisha mawasiliano na upendo kwenye mahusiano yenu.
3. Sikiliza kwa makini mawazo ya mwenzako na elewa anacholenga, badala ya kusikiliza huku ukiwa umeyapinga akilini mwako.
4. Uwe mwanamke au mwanaume tambua kuwa wewe sio mtawala wa mapenzi yenu, na kuwa huna umiliki mkubwa katika mahusiano yenu. Ninyi nyote ni wawili ni kama macho mawili, yanayohitaji kushirikiana. Jicho gani ni bora zaidi?
5. Kaeni pamoja kufanya maamuzi muhimu. Kumbuka kuwa maadamu mpenzi wako ameridhia kuwa na wewe, anawaza mnatavyoboresha mapenzi yenu, na kuyafurahia. Hivyo, heshimu mawazo yake, na hata usipotaka kuyafuata tumia hoja na sio ubabe na hila zingine.
6. Kuwa muwazi kwa mwenzako ili kuimarisha ukaribu wenu. Mtu wako wa karibu na wa kumweleza hisia zako ni mke, mume, au mpenzi wako. Uhusiano wenu utaimarika zaidi ukifanya hivyo.
7. Mwombe Mwenyezi Mungu akusaidie usijione kuwa bora kuliko mwenzako, bali kama mwenzako. Akusaidie kuheshimu mawazo ya mwenzako, na kuyafanyia kazi yaliyo mazuri, na akuwezeshe kutambua kuwa mwenza wako ana malengo mazuri na mahusiano yenu. Pia, akusaidie kutambua kuwa mshauri na rafiki yako ya kwanza ni mkeo au mumeo.
8. Tumia muda wa kutosha na mwenzako ili ujifunze hisia na mawazo yake mbalimbali. Hilo litakuwezesha kumuelewa zaidi anapoeleza mawazo yake.

Furahia mahusiano yako kwa kumwona mwenzako kama wewe mwenyewe. Ana thamani sana na ni zawadi uliyopewa na Muumba.
Share na wengine ukiupenda ujumbe huu.
Share na wengine ukiupenda ujumbe huu.
Kama una jambo la kibinafsi au kisa fulani niandikie UJUMBE kwenye sehemu ya TUMA UJUMBE SASA.
LIKE PAGE
ENJOY
I LOVE YOU ALL.
LIKE PAGE
ENJOY
I LOVE YOU ALL.