*----•<°○●πππ●○°>•----*
ππBaadhi ya wanawake wanalalamika eti waume zao hawawapi mahitaji, wanajisimamia wenyewe kila kitu.
ππLakini ukiangalia maisha yao ya mwanzo wa ndoa yao utakuta mapenzi yalivyokuwa motomoto mke aliamua asimsumbue mume, vile anauwezo aliamua kujisimamia mahitaji yake mwenyewe.
ππSasa baadha ya muda kupita na kuzoeana, mke akataka kuwa kama wake wengine wanaonunuliwa kila kitu na waume zao.
ππSasa akianza kuitisha haki zake hutokea mvutano wa hali ya juu, kwanza mume hufikiria mapenzi yamepungua kwa mkewe, *"kwa nini ywaniitisha mahitaji na bado anapata pesa kama awali"*
ππEwe mwanamke, hata kama unapesa kuliko mumeo, muache mumeo abebe mahitaji yake yote, ila pale patapungua unaweza saidia ila isiwe ratiba.
ππPesa zako ewe mwanamke zitumie katika ndoa yako kwa kufanyia yale mambo ambayo yanazidisha mvuto na kuongeza mapezi na si kubeba jukumu la mumeo wewe ila kwa dharura.
*ππJinsi unavyoweza kutumia pesa yako kuzidisha mapenzi*
1. Unaweza kuchagua siku moja mkatoka out sehemu nzuri na gharama ukagharamikia wewe.
2. Unaweza kusema mume wangu leo tuwatembelee wazazi wako na ukagharamilia safari hiyo na ukafanya shopping mkabeba kwa pesa zeko.
3.Unaweza kununua vitu vya kuremba nyumba, mfano zulia zuri, shuka zuri, viti vya jikoni nk.
*ππMUACHE MUMEO ABEBE MAJUKUMU YAKE ILA KAMA HANA UWEZO KABISA MSAIDIE KUYABEBA NA UWEZO UKIWA MBEBESHE MWENYEWE*
*ππUSIMSAIDIA KUBEBA BAADHI YA MAJUKUMU YAKE ATAJIONA ANA UWEZO WA KUONGEZA MKE NA MWISHO YA KWISHA WEWE NDIO UTAUMIA.*
ππ➿➿➿➿➿➿➿➿ππ