-->

WALIOTULETEA MATATIZO SASA WANAHANGAIKA KUYATATUA...

utamuzaidiapp
Hawa jamaa wametumia miaka yote minne kutengeneza matatizo, sasa wanataka wautumie huu mwaka mmoja uliobaki kutatua matatizo waliyotengeneza wenyewe.
Eti walivuruga mfumo wa biashara kiasi kwamba watu wengi wamefilisika, wengine biashara zao zimeshuka, wengine wakaamua kuhamishia biashara zao nchi jirani na wengine wamepoteza hata uhai wao.
Halafu wakaharibu mfumo wa Elimu, sasa hivi elimu yetu imepoteza dira. Walisema elimu ni bure lakini bado tunailipia, walisema wataongeza kuajiri walimu lakini uhaba wa walimu umeongezeka.
Kwenye elimu ya msingi kuna mkanganyiko mkubwa kiasi kwamba walimu, wanafunzi na wazazi hawaelewi kinachoendelea. Mfano; Walimu wanafundisha kwa mtaala mpya wenye muhtasari wa kuishia darasa la sita lakini Waziri mwenye dhamana anadai wataishia darasa la saba!

Kana kwamba haitoshi wakavuruga sekta ya kilimo hadi inatia kinyaa. Bei za pembejeo ziko juu lakini bei za mazao ziko chini sana!
Vivyo hivyo wameharibu sekta zote binafsi, hali iliyopelekea watu wengi kupoteza ajira zao na wanaotafuta ajira kupoteza kabisa matumaini ya kupata ajira baada ya kuhitimu taaluma mbalimbali.
Viwanda vingi vimefungwa, vyuo vingi vimekufa, shule nyingi zimefungwa na taasisi nyingi zimekufa kabisa.

Pia wamevuruga sana maisha ya watumishi wengi baada ya kuleta sheria kandamizi ya urejeshaji wa mikopo, kusimamisha upandaji wa madaraja sambamba na usimamishaji wa upandaji wa mishahara.
Vile vile wamevuruga amani, umoja na mshikamano wetu kwa kuleta watu wasiojulikana wanaoteka na kuua watu na kuleta ubaguzi wa kisiasa.
Hawakuishia hapo wakaharibu demokrasia ya nchi yetu kwa kuzuia bunge live na kuzuia shughuli za kisiasa, kununua wanasiasa wa upinzani na mengine mengi!
Sasa wanahaha usiku na mchana kuyatatua matatizo wenyewe ili wajinusuru kwenye uchaguzi mkuu ujao wa hapo mwakani 2020.
Wanapaswa kuelewa kuwa watanzania wote sio wapumbavu kama wale maprofesa!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU