Kaka mimi nimeolewa, ndoa yangu ina miaka miwili na nina mtoto mmoja na mume wangu, lakini kabla ya kuolewa na mume wangu nilikua na mtoto ambaye niliza ana mwanaume mwingine. Sikumuambia mume wangu kuwa nina mtoto kwani alikua anaishi na Baba yake. Baba yake alimchukua mtoto tangu akiwa mdogo kipindi hicho mimi nipo chuo akamlea na sikumchukua tena, sasa hivi mwanangu huyo wa kwanza ana maika 7.
Tuligombana na Baba yake tukaachana, sababu ya kuja kwako ni kwamba, mwaka jana mwishoni mwanangu huyo alikua anaumwa. Basi, kipindi anaumwa alilazwa hospitalini, nilimdanganya mume wangu kuwa Mama yangu anaumwa nikaenda kumuona mwanangu kwa Bibi yake kwani mume Baba wa mtoto alikua nnje ya nchi. Basi akati narudi niakwa nawasiliana na Bibi wa mtoto, hapo ndipo Mume wangu aliona meseji tunatumiana.
Sikua na namna tena ilibidi nimuambie kuwa nilikua na mtoto ambaye nilizaa kabla ya ndoa na sikumuambia kwakua alikua akiishi na Baba yake na mimi sikua na mawasiliano nao. Mume wangu alikasirika, nilimuomba msmaaha sana, aliniambia nisimuambie mtu yoyote kuhusu mtoto, lakini baada ya hapo kila kitu kilibadilika, alianza kuwa msiri, akaanza kuwa mtu wa hasira, yaani haeleweki eleweki.
Sababu ya kuja kwako kaka ni hivi, sasa hivi mume wangu ananaimbioa kuwa hawezi kuendelea kuishi na mimi, tugawane mali tulizochuma kwakua yeye hawezi kuishi na mwanamke aliyezaa, anasema alishaapa hivyo tangu zamani kuwa hawezi kuishi. Nimejaribu kuomba msamaha lakinia mekataa, ananiambia tulee tu mtoto ila hawezi kuishi na mimi tena.
Kaka wiki iliyopita mume wangu alinipa talaka, na sasa hivi nipo Eda, naomba ushauei wako kaka, nisaidie, mimi nina mtoto lakini siishi naye, yaani nimechanganyikiwa Kaka. Naomba nisaidie hata kuongea na mume wangu, nilimficha kuhusu mtoto kwakua nilikua nahofia kuwa akijua kuwa nina mtoto basi anaweza kuniacha, nisaidie Kaka sijui nifanye nini, nimechanganyikiwa.