-->

WANAWAKE UJUMBE UNAWAHUSU HUU.

Chumba cha wakubwa App Ranking and Store Data | App Annie
1. Unapokua mke usifikiri unaenda kwa mume ili upate furaha. Furaha huwa inaanza na wewe mwenyewe ndani yako. kwenye nafsi yako, moyo wako, roho yako na mwili wako.
Ukipata mume mwenye mapenzi, anayejali hiyo inakuwa ni kama Bonus tu kwako, na Bonus hio itakuchochea au itaendeleza kile ambacho tayari kimeanza ndani yako.
Mwanamke asiye na furaha yake binafsi hata apate mume wa aje, huwa hafeel chochote na saa zote hua anahangaika na mapungufu ya mume wake.
2. Unapokua mke kumbuka wewe una thamani zaidi ya ndoa yako. Kuna wanawake wanachanganya thamani yake na uhusiano wa ndoa. Wewe umezaliwa kwa kusudi, na una mambo mengi ya kufanya, ndoa ikiwa mmoja wapo ukiwa umejaliwa.
Sasa inapotokea uhusiano uko ndivyo sivyo, usifikiri ndiyo mwisho wa ulimwengu. Kuna mambo mengi zaidi ya kufanya huku ukiendelea kumuamini Mungu kwa habari ya mahusiano yako!
3. Unapokua mke tambua Wanamume ni tofauti na wanawake. wameumbwa tofauti, wanafikiri tofauti na wanatenda tofauti.
Kwaio wewe ukimlazimisha mwanaume awe na akili ya kike utajinyanyasa bila sababu.
4. Unapokuwa mke jitahidi Mume wako ajue msimamo wako kwenye mambo ya msingi. Mambo haya ni marahisi zaidi kufanya kabla ya ndoa au pale mwanzoni mwa ndoa, Huyu mtu ajue kukupiga ni kosa la jinai, na anaweza pelekwa polisi kwa hilo, kukutukana na kukutishia maisha ni kosa la jinai, ili anapodeal na wewe, hata kama ana hasira awe anakumbuka.
Mbona hawawafanyiagi maboss wao?? Mbona hawaendagi kupiga polisi??? ni kwasababu wana uwezo wa kujizuia kuyafanya hayo! Hivyo kama anaweza kuheshimu watu wengine, anaweza pia kukuheshimu wewe, hivyo kwa lugha yoyote mnayoelewana, ni vema akajua wewe sio mpira wa kupiga, wewe sio punching bag.
5. Unapokua mke usiwe mchokozi yaani usiruhusu kutengeneza mazingira ya kutendewa ndivyo sivyo. Kwa mfano mume kakosa, unaanza kumchamba, ni rahisi kumfanya mkono wake ukajikuta..... au mdomo wake ukatelezaaa...
6. Unapokua mke jizoeshe kutafuta hela. Yaani kuomba omba huwa kunaweza kukakushushia thamani yako jishughulishe, fanya kazi, na mtumikie Mungu.
Unajua ukiwa na hela yako:
(i) Inakuongezea heshima
(ii) Inamjengea mtu heshima na ujasiri wa kutonyanyasika.
(iii) Unapata baadhi ya vitu, ambavyo ungevikosa bila pesa, ungejisikia kunyanyasika
(iv) Unaweza kutoa ushauri, mchango wa maana, kuliko kila siku kuchangia hoja za bila kusaidia gurudumu
(v) Itakupunguzia misongo ya mawazo, ambayo inakufanya uwe mke mwenye mdomo na kuchochea kunyanyasika
(vi) Utakuwa msafi, nakuambia kuna usafi hata ufundishweje, sijui chumbani, sijui sebuleni jikoni, mazingira ya nje, huwezi bila hela, kuna vitu ili ufanye unahitaji kua na hela.
Utajikuta una makufuli yamejaa kutu, na huna hela ya kununulia.
MWISHO nimalize kwakusema katika jitihada za kuwa mke mwema namtii, jua kabisa kutii maana yake siyo kunyanyaswa.
na nawaombea kwa Mungu awape hekima ya kuishi kwa furaha kwenye ndoa, na pia Mungu awape hekima zaidi na utayari wa kuwa wake wema na watii.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU