-->

UNAFIKIRI NI KWANINI WATU WENGI HUYAPA NAFASI KUBWA MAHUSIANO YA AWALI JAPO YALIWAUMIZA KULIKO WALIYOPO?

UTAMUZAIDIAPP
Kila mtu anapenda kupendwa na kuthaminiwa na hiyo ndo FALSAFA YA MAPENZI. Huwezi kusema upo kwenye MAHUSIANO AMA NDOA na mtu ambaye hakupendi wala kukuthamini, Ili itimie maana ya MAPENZI ni pale mtu anapotengeneza DHAMANA YA UPENDO.
Wahenga walisema;
"AWALI NI AWALI" ndo maana mtu anapohisi MAHUSIANO AU NDOA yake haimpi AMANI kwa hakika MOYO HUUGUA na hapo njia za maridhiano kuwa wazi kwa yule ajuaye kukosea na kujisahihisha, Makosa ni sehemu ya u-bin adam na ndo maana HAKUNA MKAMILIFU.
Ubaya wa uvumilivu ni pale kila unapojaribu kumuweka sawa mwenza wako ili muendane lakini inakuwa kama HAIWEZEKANI.
Kwenye UPENDO WA DHATI uongo hujitenga, Na ndo maana THAMANI YA UHUSIANO AMA NDOA YA AWALI hujulikana pale mtu anapo kuwa amebaini kwamba ALIKOTOKA KULIKUWA NA UPENDO WA DHATI na hapo alipo DRAMA NI NYINGI KULIKO UKWELI😭😭😭
Yapo MAHUSIANO na NDOA nyingi tu zinavunjika kwa KUDHANIA lakini Mtu anapokuwa amekuacha ama umemuacha Kuna wakati atajua kwamba wewe ndiye ULIYEMPENDA kuliko alivyofikiria hata akaamua kukuondoka.
Na mara nyingi WAWILI WAKITENGANA NA KILA MTU KUWA NA MTU MWINGINE haiwezekani kurudisha ule UPENDO ambao wanaamini walikuwa nao awali, Kwa sababu UPENDO WA DHATI hauchangamani na USALITI Kwani kama ULIMPENDA kwa hakika usingeanzisha UHUSIANO mwingine UNGESUBIRIπŸ’ƒπŸ’ƒ
Akiishakuwa alikuwa ama anae mtu Mwingine na mkapanga kurudiana niamini MTALINDWA NA MAZOEA wala sio UPENDO 
Mwenye UPENDO WA DHATI hawezi kubeba watu wawili kwa wakati mmoja, Ukiona hivyo JIONGEZE MKO KWENYE MAZOEA wala sio kwa UPENDO.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU