Mapenzi ya mbali yana changamoto kubwa sana lakini ni aina ya mapenzi ambayo kutokana na mfumo wetu wa maisha basi hayaepukiki. Ninaposema mapenzi ya mbali simaanishi tu pale mmoja wenu anapokuwa akiishi mkoa wa mbali moja kwa moja.
Hapana lakini hata kama mpenzi wako akisafiri kwa muda wa kuanzia mwezi mmoja na kuendelea binafsi nasema ni mapenzi ya mbali.
Labda nidokeze kidogo, mpenzi akiwa mbali basi mmoja huwaza kuhusu kusalitiwa hilo halijalishi mmekaa mbali kwa mwezi mmoja au miaka miwili.
Sasa kama unampenzi nilazima ujifunze namna ya kuwasiliana naye kipindi hicho akiwa mbali. kwasababu mapenzi ya mbali kuvunjika kutokana na wenza kushindwa kujua namna ya kuwasiliana.
Ninaposema kuwasiliana simaanishi kupigiana simu kila sekunde na kila dakika hapana,
(1) UNAPASWA KUONGEA NAYE MARA NGAPI KWA SIKU?
Ingawa mawasiliano ndiyo msingi mkuu wa mahusiano ya mbali lakini yakizidi sana huwa kero.
Kumpigia pigia simu mume wako, mke wako au mpenzi wako aliyembali, ukiwa huna kitu cha maana cha kuongea, tena kwa kulalamika au kutaka akusikilize wewe tu haiwi tena mapenzi inageuka na kua kero.
Hapa kuna mambo mawili, kwanza nilazima uonyeshe kua unajiamini, hapa simaanishi kumuamini hapana kua unajiamini vya kutosha na kila wakati humuwazi yeye, una kitu kingine cha maana cha kufanya zaidi ya kumuwaza yeye, lakini pili nilazima umpe pumzi na kumruhusu akumiss.
Ongea naye asubuhi ukitaka kujua hali yake, jioni kuulizia siku yake na usiku kumtakia usiku mwema na kunyegeshana. Epuka sana kuongea mchana hasa kama yeye anafanya kazi kwani si wakati mzuri, utamkuta na stress na anaweza kukujibu vibaya na kuwa mwanzo wa kuvurugika kwa penzi lenu.
Umemtumia meseji hata hajajibu basi ushampigia, umetoka kumpigia umemtumia na mesji, yuko kaitwa na bosi umepiga, hajapokea akikupigia unaulizia mbona hukupokea, mbona hujajibu, unapiga simu mara kumi kwa siku, wewe ni kero, narudia wewe ni kero.
Ndugu yangu atakuchoka mapema, watu wanasema sukari pamoja na utamu wake kuilamba kila saa ni kero inageuka kua sumu. Kama unatabia hii kupiga simu mara kumi kwa siku, halafu hakuna hata cha maana unachoongea basi jua unamkera mwenza wako.
Kama unatabia kupiga simu mchana muda wa kazi kwakua wewe uko ‘bored’ huna kitu cha kufanya au ushamaliza kazi zako uko free unampigia wakati yeye ndiyo kwanza bosi kamsimamia au wateja wanamsumbua jua unakera na anashindwa tu kukuambia ukweli.
Kama unataka mpigie simu muda ambao unajua kabisa katulia, hana mawazo, kichwa kiko safi hapo mtaelewana. Lakini kila saa wewe tu kana kwamba wewe ndiyo Oxygen yake asiposikia sauti yako anakufa, badilika.
(2) VITU GANI MNAPASWA KUONGELEA MNAPOWASILIANA?
Kabla sijakuambia ni kitu gani unapaswa kuongea na mwenza wako labda nikuambie mambo ambayo yanakera ambayo anatamani hata akukatie simu.
“Mbona hukujibu SMS yangu…ulikua unaongea na nani? “Uuko wapi saa hizi”, “uko na nani”, hebu nipe niongee naye”...
“Kwanini mchana hukunipigia tena”, “yule uliyelike picha yake ni nani?” “Mbona jana uliwahi kulala”, “nipe flani niongee naye”, “uko sehemu flani kweli?” na vitu vingine kama hivyo. Kwamba umepata wasaa wa kuongea naye badala ya kuongea mambo ya mapenzi, ukamuambia siku yako unaanza kulalamika.
Labda nikuambie hakuna mtu ambaye anapenda kushutumiwa hasa kama huna USHAHIDI na kwakua hukua naye basi huna ushahidi. Yaani kusikiliza malalamiko ya kijinga ya mtu ambaye HAJIAMINI kwenye simu inaboa na anatamani kukukatia simu.
Ndiyo maana kila saa hujifanya kachoka, yuko bize, kuna kazi anamalizia kwakua unaboa na ujinga wako unaoongea. Labda nikuambie kitu kimoja hata kama nikweli kafanya yote yunayomshutumu tayari uko mbali huwezi kubadilisha chochote.
Mimi na mpenzi wangu tunaishi mbali, mikoa tofauti kabisa, kwa siku tunaweza kuongea mara moja au mbili, lakini tunaweza kuongea hata masaa matatu kwakua hatuboani. Kwamba nasisimkwa kabisa na namiss kuongea naye, ikipita siku sijaongea naye naona kama nimekosa kitu flani.
Hii nikwakua hatutumii muda mwingi kulaumiana, tunaongea mambo tu, umbea, siku ilikuaje, sijui nini na mambo mengine ambayo hata hatupangi kuongea. Namuambia siku yangu nayeye naijua yake, siulizii kuhusu meseji ambazo hajajibu, sijulizii kwanini hakupokea simu.
Akiniambia alikua kalala alikua bize namuelea na nasahau. Hii nikwasababau najua hata nikikasirika haitasaidia na najua kama nikitumia muda mchache wa kuongea naye kulumbana basi nitampoteza, nitamboa na hatatamani kuongea tena na mimi..
Tumia muda mchache kuongea kuhusu mapenzi na si migogoro. Kuna mengi ambayo yatasemwa hata yeye anasikia mengi lakini hebu amueni kusema hapana, mimi najiamini wewe jiamini hivyo tuaminiane na tuache kuzungumza wivu tuzungumze mapenzi.
(3) UNAKUSANYA MAKOSA!
Nikama mchana ulikua na kazi moja ya kukusanya makosa yake. Unaongea na marafiki zake kujua nyendo zake na kujua huko aliko mchana wote alikua akifanya nini, unampigia kila mtu unayemjua, unakusanya ushahidi, kupitia ukurasa wake kuwa kalike wapi na wapi.
Kacomment nini na sehemu gani, alikua online muda gani na hakua akichati na wewe. Usiku ukipiga unajiandaa kumsuta, akikuambia siku yake labda kakudanganya kidogo au kadanganya sana unaaanza kumsomea makosa yake, mbona hivi vile sijui vile.
Yaani badala ya kunyegeshana usiku basi ana kazi ya kujibu shutuma. Mtu kama huyu hatatamani kuongea na wewe tena, achana na mambo anayofanya huko hayakuhusu, labda kama unataka kumaucha lakini kama bado unampenda na kila siku nikufuatilia hata kaenda chooni mara ngapi?
Utampoteza, unaboa na kila siku atajifanya bize kwani anajua huna chakuongea. Lakini utamfanya na yeye kila siku nikutafuta ushahidi wa namna ya kujitetea kabla ya kuongea na wewe. Yaani anakua kama wakili anaenda kwenye kesi kila siku lazima atafute ushahidi wa kujitetea. Badilika utampoteza!
(4) MUELEWE ANAPOSEMA YUKO BIZE.
Hiki ni kitu ambacho unatakiwa ujifunze, mwenza wako anapokuambia yuko bize, hawezi kuongea kwa wakati huo, kwasababau yoyote ile acha kuwa king’ang’anizi. Inawezekana ana sababu za msingi hataki kuongea na wewe, labda kachoka, au kaudhiwa na mtu, ana mawazo.
Kuna mambo anataka awaze peke yake na labda akiwa tayari atakushirikisha. Lakini inawezekana umemuudhi wewe, kuna maneno kasikia na yanamchanganya, bado hajawa tayari kukuambia na kukabiliana nawe.
Sasa unapoanza kusema “Uko bize unaongea na nani”…”umeona mimi si wa muhimu”…”umeona nakupotezea muda”….”kama hunipendi si useme tu”…”unataka uongee na malaya wako”….”uko na nani hapo mpaka hutaki mimi nipige simu” kwakifupi unalaumu laumu, unalazimishia muongee wakati yeye hayupo kwenye mood.
Unaona kabisa analala, kwakua wewe huna usingizi unataka akusindikize kukesha, lakini unampigia usiku wa manane kachoka wewe hujachoka unataka muongee kakuambia mtaongea asubuhi lakini bado ni king’ang’anizi.
Yuko kazini kakuambia baadaye unaanza “kwahiyo kazi ni bora kuliko mimi” na maneno mengine mengi! Ndugu yangu unaboa, utampoteza na unazidi kumsukuma mbali zaidi na alipo. Jifunze
Mimi yangu ni hayo Kama wewe unatabia hizi badilika kwani utampoteza huyo mpenzi wako utamlazimisha akuache na asitamani kuongea na wewe wakati msingi muu wa mapenzi ya mbali ni mawasiliano
LUCAS LUMBASI