Tajiri mmoja alikuwa anakaribia kufa, alikuwa na marafiki matajiri wakubwa, wataalam, wasomi, wanasiasa na watu mashuhuri. Akaiita familia yake kuwapa wosia.
1. Nataka siku nikifa, wakati napelekwa kuzikwa jeneza langu libebebwe na marafiki zangu sita ambao ni madokta mahiri kuliko wote hapa nchini.
2. Nataka fedha zangu zote nilizo nazo zipangwe chini katika njia ya kwenda kaburini, magari yangu yote yawepo eneo la kaburi na picha za mali zangu zote zibandikwe kwenye magari.
3. Nataka mikono yangu iwe inaonekana na kila mtu, isiwe ndani ya jeneza. Kila mtu atakayekuwepo msibani siku hiyo aone mikono yangu.
Watu wakashangaa huu wosia una maana gani? Tajiri akaanza kuwafafanulia:
1. Nataka jeneza lenye mwili wangu libebebwe na wale marafiki zangu sita madaktari mahiri kwa sababu nataka wote wataokuwa msibani waone kwamba hata madaktari mahiri kiasi gani hawawezi kuzuia kifo bali Mungu peke yake.
2. Nataka fedha zangu ziwekwe chini watu waone, magari na picha za mali zangu zionekane wakati nazikwa ili watu wafahamu kwamba mali yote tunaacha hapa duniani.
3. Nataka mikono yangu ionekane ili watu wakumbuke kwamba dunia hii hatuondoki na chochote bali mikono mitupu kama tulivyokuja.
Mungu atujalie kukumbuka haya na kujua kwamba cha muhimu duniani ni utu wetu na kumuabudu yeye.
SHARE UJUMBE HUU TAFADHALI