-->

MWANAMKE, INAPOTOKEA MWANAUME ANATAKA KUKUOA, KABLA HUJAKUBALI FANYA HIVI.!

*Sikia nikuambie kitu mdada usitabasamu wala kufurahia pale inapotokea au anapotokea mwanaume kukuambia kuwa angependa kukuoa kufunga nawe ndoa, bali unatakiwa kujitafakari na kujiuliza maswali zaidi ya mia moja juu ya maisha ya ndoa hiyo, kisha piga goti na kumuomba mwenyezi Mungu ili mwanaume huyo akawe ni kiongozi wa ndoa na maisha yako kiujumla.*
*Omba Mungu mwanaume huyo akawe furaha na amani maishani mwako akawe chachu ya mabadiliko kuelekea mafanikio yako na akawe mume na baba mwenye kujali na kupenda familia na kizazi chenu na mwenye kuheshimu na kujipenda na kuithamini ndoa yenu, kwanini nakuambia umuombe Mungu?*
*Kwa sababu unaweza kuvaa pete ya ndoa leo na kesho ukatamani uivue unaweza kufunga ndoa leo lakini kesho ukatamani bora ulivyo kuwa single, jipange dada ndoa ni safari mpya katika maisha yako, take care mtegemee Mungu akupe mume bora na kabla hujamuitaji mume bora basi wewe kuwa mwanamke bora kwanza.*
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU