-->

MSIPO FANANA,MTASUMBUANA,MTALIZANA NA HATIMAYE MTAISHIA NJIANI.

My Blog – Page 10 – My WordPress Blog


Mahusiano ya kimapenzi siku zote yana nafasi kubwa sana katika maisha yetu.
Yanapokwenda vizuri,furaha ya moyo inapopatikana basi mtaishi miaka nenda rudi bila mikwaruzano na hata ikitokea,mnaimeza ndani kwa ndani.
Mapenzi yana changamoto zake,wengi wamejikuta yakiwashinda kwa sababu ya kutosoma alama za nyakati. Wanashindwa kuelewa kwamba wapo kwenye nafasi gani na kujikuta wakiishi tu kimazoea bila kujua wanafanana tabia au la.

Ndugu zangu,japo ni vigumu kuujua moyo wa mtu lakini hakikisha pindi unapoanzisha uhusiano na mtu awe kweli ni mtu ambaye mnafanana. Mnaivana kitabia,mnashibana vya kutosha na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza mbele yenu.
Hakikisha uliyenaye anakupenda kwa dhati kabla ya kuzama penzini.
Japo watu wanabadilika lakini angalau,jiridhishe kwa jinsi unavyoweza kiasi cha akili yako kuweza kung’amua kwamba kweli uliyenaye anakupenda kwa dhati au la.

Anayekupenda utamjua tu kwamba huyu ananipenda au ananizingua. Anayekupenda atakujali,atakuthamini na hayupo tayari kukupoteza.
Anayekupenda hawezi kukuweka kwenye matatizo.
Kila mara atahakikisha anaitafuta furaha yako kwa gharama yoyote,Hatopenda kukukorofisha,Atakupa faraja wakati wote, atakulinda.
Wakati wa matatizo yako,ataguswa nayo kama vile ambavyo yamekugusa wewe.
Huyo ndio mtu ambaye mtakuwa mmefanana na kweli mnaweza kuruka safari moja.

Kinyume cha mtu mnayefanana,ni mtu ambaye hamfanani. Ukiishi na mtu ambaye hamfanani tabia na mwenendo,basi jua wazi kwamba msingi wenu wa maisha ya uhusiano hauwezi kuwa imara.
Ni lazima tu utatetereka na hata kuanguka kabisa.
Ndio maana tunashuhudia ndoa nyingi sana za sasa hazidumu.
Watu wanaingia kwenye ndoa kutokana tu na tamaa mbalimbali.
Mwanamke anataka tu kuitwa bibi harusi au mume naye anataka tu kuitwa bwana harusi.

Ni vyema kua makini na mtu anayekuambi anakupenda je ana ishi maisha aina gani, je unahisi amekutongoza kwa kua anajua huwezi kukataa kisa ni maarufu au anaishi ki star.
Haya mambo mabinti kueni nayo makini sana

#2020 #LovefeelingsLoveZone
#WrongaRuelationShip
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU