
Hapa ndipo unatakiwa kujua asilimia kubwa ya watu watakuja katika maisha yako watapita itafika kipindi wengine utawasahau, wengine utaendelea kuwakumbuka...hii ni kwa sababu maisha ni safari ndefu sana, yupo ambae atashukia njiani ...na yupo ambae utafika nae mpaka mwisho ...yule ambae utafika nae mpaka mwisho ndie mtu ambae ulitakiwa kuwa nae ..na yule ambae atashukia njiani hakupangwa kuwa sehemu ya mwisho wako, bali alikuwepo katika safari yako kukusindikiza tu.
Usitaabike mtu anapoamua kupita njia yake na kwenda anakojua mkiwa katikati ya safari maana hakuwa sehemu ya mwisho wako.. Alie sehemu ya mwisho wako mtafika nae haijalishi kutatokea dhoruba gani njiani, haijalishi kutatokea ajali ngapi njiani kama imepangwa mtafika wote mwisho trust me mtafika tu.
Mmenisikia uko nyuma au niongeze sauti