SUALA la usaliti ni tatizo katika uhusiano na ndoa lakini lazima tuwe wakweli kwamba linakera zaidi kwa wanandoa. Kwa bahati
mbaya sana, suala hili linawahusu wanawake zaidi na wanakosa mbinu za kukabiliana nazo Hapa kwenye All About Love nimeandaa mbinu za kitaalam kabisa ambazo kama zikitumika sawasawa zinaweza kusaidia kwa kiasi
kikubwa sana kukabiliana na usaliti wa mapenzi.
Kwa wanandoa, kama mizizi ikikomaa kinachotokea mbeleni ni mume kuamua kuwa na nyumba ndogo. Hapo ndipo kwenye tatizo
zaidi na nyumba kuonekana chungu zaidi.
Je, wewe unafanya nini kukabiliana na usaliti katika nyumba yako? Huu ni mfululizo wa makala niliyoanza tangu wiki mbili
zilizopita. Sasa tunaingia katika hatua nyingine.
Rafiki yangu mpenzi, hebu twende pamoja tukaone mbinu nyingine muhimu ambazo kwa hakika zinaweza kukusaidia kuepukana
na usaliti katika nyumba yako.
FANYA MAMBO MUHIMU
Wakati ukiwaza jinsi ya kumfanya mumeo/mkeo asitoke nje ya ndoa, lazima pia uwe mtu wa kufanya mambo muhimu.
Unapofanya mambo muhimu katika ndoa yako, kunampa sababu mwenzi wako kutunza heshima ya ndoa hiyo.
Nasema heshima kutokana na ukubwa au ubora wa umuhimu wa jambo utakalokuwa umelifanya kwa ajili ya ndoa yako. Hapa
kuna vijisehemu vinne vinavyofafanua zaidi.
Ishi kwa bajeti
Kama wewe ni mwanamke, kati ya mambo ambayo yatamfanya mumeo akupe nafasi ya kwanza na kujikuta akishindwa kuisaliti
ndoa yake ni wewe kutengeneza bajeti nzuri. Kama mama, wewe ndiyo msaidizi wa familia.
Usaidizi hauishii katika kufua, kupika na kufanya usafi wa ndani pekee. Tengeneza bajeti ndogo ya chakula na mambo ya
maendeleo kisha mpatie mumeo na umfafanulie zaidi. Zungumzia kuhusu maendeleo na malengo yako kwake kwa ajili ya maisha
yenu ya baadaye kama wanandoa.
Hata kama wote ni wafanyakazi au wafanyabishara, kama mama bado jukumu la nini kifanyike vipi ndani ya nyumba ni lako.
Ukaribu huu na uwezo huu mkubwa wa ubongo wako utamfanya azidi kuona umuhimu wako kwake.
Mpe sababu kwa nini
asiwe na mwingine
Kutoka nje ya ndoa kunazalishwa na kutoridhishwa na mahaba ya nyumbani. Inawezekana kabisa, humfanyii mambo uliyokuwa
unamfanyia zamani. Mathalani, ulikuwa ukimtumia meseji kila mchana ukimkumbusha kula, ulikuwa ukimtakia kazi njema na
mengine mengi ya kufurahisha.
Wakati wewe ukiacha kufanya hivyo, kazini kwao yupo mwanamke anayemzimia na kazi yake kubwa ni kutunga mashairi ya
mahaba na kumtumia mumeo; atatoka kweli?
Kuwa naye karibu, tawala siku yake, mpe sababu ya kuwa na wewe. Mfanye aone umuhimu wa kukuwahi nyumbani mara baada
ya kumaliza kazi.
Mwanaume kuwahi nyumbani halazimishwi wala hafungwi kamba, ni ule umuhimu ambao unaonesha wewe mwenyewe kwake.
Namna ya kumfanya yeye aone wewe ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Mpongeze anapokosea!
Inaweza kukushangaza kidogo, lakini huwezi kuamini kabisa kwamba mwenzi wako anapokosea hutegemea zaidi lawama, matusi
na maneno ambayo hayatamfurahisha.
Kuwa tofauti, akichelewa kurejea nyumbani, mfungulie mlango, mkumbatie, mbusu na mpe pole kwa kazi.
“Hongera mume wangu, wewe ni mchapakazi na unajali familia yako, najua ulikuwa unahangaika, karibu nyumbani baba. Utakula
au utaoga kwanza?”
Unaona maneno hayo? Mwambie hata kama ananuka pombe! Hapo utakuwa umempa somo tofauti na kumwambia: “Najua
umetoka kwa wanawake zako...hili lijanaume sijui nimetoka nalo wapi mimi?”
Usilogwe dada yangu, kesho atarudi kulekule, ikiwezekana atalala hukohuko kabisa.
Linda ndoa yako
Sitafafanua sana kijisehemu hiki, lakini kikubwa nilichokusudia ni kwamba, kuwa bora faragha! Jifunze kila siku kuwa mkali
kwenye sayari ya wapendanao. Ukiweza kumkamata vizuri eneo hili, aende nje kufanya nini?
Utaalamu faragha si uhuni, kuwa bora, panua mawazo, peruzi mitandaoni, soma majarida lakini pia tafiti mwenyewe. Ukiweza, kila
wiki gundua sehemu moja mpya inayompa msisimko zaidi mwenzi wako. Atatoka kweli?
ZUNGUMZIA MUSTAKABALI WA FAMILIA YENU
Unaweza kumfanya mwenzi wako asikusaliti wala asifikirie kuwa na nyumba ndogo, ikiwa utapata wasaa wa kuzungumza naye
mustakabali wa ndoa yenu.
Katika hili, yapo maeneo muhimu zaidi ambayo ukiyakazia, ndoa yako itaendelea kuwa imara.