Wanawake ni watu wa hisia sana wanapokua katika mahusiano tofauti kabisa na wanaume. Humchukua muda mrefu mwanamke kupona kimapenzi pale anapoachana na mpenzi wake wa muda mrefu kuliko mwanaume. Lakini pia hata kama hutawekeza kiuchumi kwa mwanaume lakini uwekezaji wako wa muda ni kitu ambacho hutaweza kukirudisha. Kukaa na mwanaume miaka mitano katika mahusiano ukitegemea kuolewa kisha anaolewa mtu mwingine kunaweza kukuchanganya na kukuathiri katika maisha yako yote ya mapenzi.
Wanawake wengi wanapotendwa hujikuta hawawaamini tena wanaume hata wanapotokea wale siriasi, lakini pia umri unakuwa umeenda na kwa mwanamke uwezekano wa kuolewa hupungua kadri umri unavyoongezeka hivyo mwanamke kujiona anazeeka anaweza kuamua kumkubali mtu yeyote yule ilimradi tu aonekane kama ameolewa. Anaweza kufanya maamuzi hayo kwakuwa tu ni mpweke na anaona anawajibu wa kuwa na mume au wakati mwingine kwa kutaka kumkomoa yule ambaye alimuumiza kwa kumuonyesha kuwa hata nayeye anaweza kupata mpenzi na kuolewa tena ndani ya muda mfupi tu.
Hakuna kitu ambacho kinauma kama kuwekeza katika mapenzi kwa muda mrefu kisha unakuja kuachwa kama mbwa, iwe kwa mwanaume au mwanamke na kwa mwanamke inauma zaidi kwakuwa ni ngumu sana kupata tena mwanaume mwingine wakukukuoa, wakati mwingine utahitaji kuingia tena katika uchumba sugu wa muda mrefu kupata mtu sahihi wa kuoana naye.
Iko hivi wakati mwanaume anapoachana na mpenzi wake wa muda mrefu, kuna wanawake zaidi ya ishirini ambao wapo katika mstari wanatamani awaoe, kwa mwanamke ni tofauti. Kuna wanaume zaidi ya kumi wanatamani wapiti naye tu, wamchezee basi na wengine saba wanatamani kuingia katika mahusiano naye wa mchunguze na watatu ambao wanatamani kumuoa.
Kwa bahati mbaya hawa watatu wanaotamani kumuoa wanakuwa hawana vigezo vya mwanamke husika, wanatamani kwasababu kwao kumuoa mwanamke huyo ni sawa na kushinda bahati nasibu. Mara nyingi wanawake wengi baada ya kuachwa na wapenzi wao wa muda mrefu hujikuta wanalazimika kuwakubali hawa watatu ili tu wasidode nyumbani.
Kwasbabu hiyo basi kama mwanamke unapaswa kuwa na msimamo wako na kutokuendekeza uchumba sugu! Unapojihisi kuwa umefikia wakati wa kuolewa na upoona mtu ambaye unadhani anasifa za kuwa mume wako, usisubiri mpaka akuambie kuwa anataka kukuoa, uchumba ukishafikia miaka miwili unaweza kumuuliza mipango yake kuhusu wewe.
Kama unaona kabisa kuwa yuko vizuri na hakuna kikwazo chochote cha kuwafanya msioane basi mkishafikisha miaka miwili muulize mipango yake kuhusu wewe na angalia majibu yake kama yanamsingi au la. Wanawake wengi wanaogopa kuuliza kwakuwa wataonekana kua wanalazimishia ndoa, ukweli nikuwa hata baila kuuliza mwanamke anayelazimishia ndoa utamjua tu.
Kuna vitabia flani flani mwanamke anapoanza kuvionyesha mwanaume hujua kuwa huyu anawaza ndoa hivyo hata bila kuuliza jua kuwa jamaa ameshajua, unauliza ili wewe kujihakikishia tu kama ana mpango na wewe au anakutumia tu lakini kiuhalisia yeye anakuwa ashajua unachotaka kwake.
Jinsi unavyojitoa kwake kwa kila kitu, kumfanyia mambo kama mume wako, kumpikia, kumfulia, anapokuwa na matatizo kuyajali kama yake, namna unavyomuulizia kuhusu ndugu zake, kutaka kuwajua na namna uavyosisitiza awasaidie, namna unavyo mhamasisha kumpigia samu mama yake, unavyojali kuhusu biashara zake na mali zake,unavyomshauri mambo ya maendeleo ni kengele tosha kua unahitaji ndoa.
Kwa maana hiyo basi unapaswa kujua msimamo wake, kwa anayokufanyia bali hata kwa kuuliza. Miaka miwili imepita hembu anza kuchunguza kama ana mwingine na kama yupo wakowakoje, fuatilia kwa marafiki zake ana ongeajeongeaje kuhusu uhusiano au mchunguze yeye mwenyewe anasemaje kuhusu kuoa.
Labda anataka nini kitokee ndiyo aoe, lakini ukiona kama humsomi kwa maana umeshindwa kugundua chochote basi sikitu kibaya kama ukimuuliza. Usimuulize moja kwa moja atakuoa lini bali muulize mipango yake kuhusu mahusiano yenu. Akuambie ana mipango gani na wewe ya kimaisha.
Mpe ukweli umri wako unaenda na muambie misimamo yako, muambie kila kitu ambacho wewe unataka kutoka moyoni kabisa. Usimlazimishie kitu kwa maana usiulize kana kwamba unamuambia nataka unioe bali muulize kana kwamba unataka kujua mipango yake ili ulinganishe na ile ya kwako.
Ongea naye kwa utaratibu na usionyeshe kama una munkari sana wakuolewa bali onyesha una malengo yako ya maisha hivyo unataka kuja kama yeye anaweza kuwa sehemu ya malengo haya. Kikubwa hapa ni kukuambia kuwa usisubiri miaka nenda rudi mwanaume akutamkie, ulizia na ujue msimamo wake.
Katika ulimwengu wa zamani wanawake walikuwa wakisubiria, hali ilikua tofauti kwakuwa wanawake walikuwa wakiishi kwao na hakukuwa na mahusiano ya namna hii. Sasahivi mambo nitofauti mnakuwa wapenzi kidogo mshaaanza kuishi kama mke na mume, kuanzia mapenzi mpaka kupikiana na hata kuishi pamoja. Kwasababu hiyo basi unatakiwa kujiongeza sio umpikie na kumfulia mwanaume miaka mitano halafu akishakuchezea na kukuzeesha anaoa mwingine. Miaka yote hiyo unaishi kwa matumaini ya ndoa ya ndoto yako, unaacha watu wanaokupenda kweli na kukomaa naye kumbe yeye ana wake anampenda, uliza jua jibu na ujipange kuanzia hapo.