-->

HATA KAMA HUWEZI KUMUACHA MUME WAKO HEMBU JIPENDE WEWE BASI!

Simulizi ya mwanamke mmoja ambaye anadai kuwa ndoa yake iliingia ...
Kuna wanawake wengi wakikupigia simu na kukuomba ushauri unajiuliza hivi huyu anasubiri nini? Mbona jibu analo tayari na alipaswa kuondoka siku nyingi! Lakini ukweli nikuwa kama si wewe unayepitia maumivu yake basi hujui chochote anachochopitia na ukweli mwingine unabaki kuwa ni ngumu kwa wanawake wengi ambao wapo kwenye mateso kuondoka katika ndoa au hata katika mahusiano ya kawaida.
Sababu kubwa hata si mapenzi bali ni kipato, kuogopa macho ya watu na matumaini ambayo wanawake wa namna hii hujipa kila siku wakijiambia kama atabadilika, atabadilika wakati katika sehemu flani ya akili zao wanajua kabisa kuwa mhusika hawezi kubadilika. Mara nyingi ninapoongea na mtu najua kabisa huyu hawezi kuondoka hii ndiyo maana kila wakati hujitahidi kumuambia mtu namna ya kubaki kama akichagua kubaki.
Sasa kama wewe uko kwenye mahusiano ambayo yanakuumiza kila siku, kila siku nunalia na nunajua kabisa huwezi kuondoka. Huna furaha na huna nguvu yeyote hembu fanya kitu kimoja ambacho kipo ndani ya uwezo wako “JIPENDE” ndiyo kama uko katika hali hii hembu kuwa mbinafsi kidogo. Kwamba wakati mume wako akiendelea kufanya madudu yake huko, hembu wewe chukua muda kidogo na anza kujipenda wewe kama wewe.
Kuna nguvu kubwa katika kujipenda, kuna faida kubwa katika wewe kuwa na furaha, wakati mwingine mume wako anaendelea kukufanyia hayo anayokufanyia kwakua tu anakuona ni mnyonge, anakuona huwezi kuwa na furaha bila yeye, huwezi kuwa na maisha bila yeye. Hivyo hata kama huondoki hembu muonyeshe kuwa pamoja na kubaki kwako unaweza kuwa na furaha ndani ya hiyo hiyo nyumba tena katikati ya manyanyaso.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU