-->

UNAWEZA KUTAMBULISHWA NA BADO UKAACHWA!

Mambo wanaM&U, nimshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kukutana nayi kwa siku nyingine tena, karibuni katika kujifunza kuhusu uhusiano katika maisha yetu ya kila siku.

Mada yangu ya leo nitazungumzia watu ambao wanadhani wakitambulishwa basi inakuwa nikifungo kwa mtu aliyemtambulisha kwa maana ya kuolewa au kuoa, wakati ukweli unaweza usiwe hivyo.
Swala la wapenzi kutambulishana katika familia za pande zote mbili kwa maana ya mwanamke na mwanaume ni sehemu ya utamaduni wa jamii kubwa ya Kiafrika na ni jambo jema sana. Ila kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza kwa baadhi ya wanaume na hata wanawake, nianza na wanawake.



Unaweza ukapata mchumba ambaye akapanga mipango yote kwa kuanza kukutambulisha kwa baadhi ya ndugu zake ambao yeye anaivana nao au anaelewana nao sana na wewe mwanamke ukaona kama umeishamkamata kwa kila kitu, kwani baadhi ya dada aua kaka zake wanakufahamu na kukuita wifi au shemeji na wakati mwingine hata shangazi. Wakati huo mwanaume mwingine anaweza kufanya taratibu zote za kuja kwenu kujitambulisha kwa utambulisho feki ili kukuaminisha lakini mwisho wa siku akawa hana dhamila ya dhati ya kutaka kukuoa zaidi ya kula tunda.

 Wanaume
Mara nyingi baadhi ya wanaume wengi wamekuwa wakilalamikiwa kuwa ni sehemu ya kuzalisha matatizo yanayosababishwa na uhusiano.
Kuna watu wamewahi kuumizwa vibaya kwa kutambulishwa na wapenzi wao lakini mwisho wa siku wakaachwa solemba kama waswahili wasemavyo.
Mrembo mmoja aliwahi kupata bwana na akaonesha msimamo mzuri wa kumwambia jamaa kama ana mpenda kwa dhati na ana malengo naye kwa maana ya kuwa mke na mume basi wakatambulishane, kijana alikubali wakapanga siku na muda wa kufanya huo utambulisho, siku ilipowadia mwanadada akatambulishwa lakini mwisho wa siku aliyeolewa ni mtu mwingine.

Inaumiza na ilimuuma sana binti yule kwanza ukiangalia umri wake alikuwa bado binti mdogo lakini hicho ndicho kilichotokea.

Kila mtu anapaswa kuwa na hofu ya Mungu anapaswa pia amuonee huruma mwenziye ni kwa namna gani ataumia pindi atakapomdanganya kuwa anamuoa aua kuolewa naye wakati moyoni mwaka anajua kabisa kuwa hana mpango wa kumuoa.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU