-->

MJUE MWANAUME WAKO; UNAPOMUAMBIA HUTAKI MARAFIKI FLANI WANAMSHAURI VIBAYA NI TUSI!

▷ @iddimakengo - IDDI MAKENGOπŸ‡ΉπŸ‡Ώ - Hii ni kwa wale wadada ...

idd makengo
Hii ni tabia ya wanawake wengi, anapokua na mwanaume awe menzi au mume ambaye anamarafiki wenye tabia za aina flani, labda ni walevi, labda ni wazinzi na hata wezi. Kitu cha kwanza kinachokuja katika kichwa cha mwanamke ni kujaribu kumbadilisha mwanaume kwa kumuweka mbali na wale marafiki akiamini kuwa watamharibu mwanaume wake.
Kila siku utaiskia sitaki kukuona na flani, falni anakufanyia hivi, ananuna, sitaki kumuona flani kwangu, falani ndiyo anakuharibu na vitu kama hivyo. Labda nikuambie tu dada yangu, tofauti na nyie wanwake ambao mnaweza kukatazwa kuwa karibu na rafiki flani kutpokana na tabia flani na mwanamke ukakubali kwa mwanaume hili ni tusi kubwa sana kama kila siku wewe ni kumpangia marafiki.
Unapomuambia mume au mpenzi wako sitaki kukuona na flani kwasababu flani ni kama unamuambia “Wewe huna akili ya kujiamulia mambo yako unapelekwa pelekwa tu na marafiki hivyo acha kuwa karibu nao watakuharibu!” Sijui nyinyi dada zangu lakini kwetu hili ni tusi kubwa, kuona kuwa mume wako hawezi kujisimamia mwenyewe eti kwakua rafiki yake ni mlevi naye atalawa.
Sisemi kuwa hakuna wanaume wa namna hii, hapana wapo wengi na ambao hupelekwa pelekwa na marafiki, hawana maamuzi yao yaani wakati mwingine hata wao wanajijua lakini kumuambia sitaki hiki na kila si suluhu. Kwanza kabisa kuna uwezekano mkubwa kuwa kabla ya kukutana na wewe alikua na hao marafiki, haohao ambao unaona wanamshauri vibaya na kumpangia kila kitu alikua nao na kuja kuwa na wewe hivyo kama walishindwa kumshauri kuhusu wewe sijui kwanini una wasiwasi.
Kamauko na mwanaume wa namna hii na unajua kabisa kweli hana akili za peke yake na marafiki humuendesha hembu acha kulalkamika, acha kumchimba mkwala wa kauchana na marafiki zake, acha kuongea na marafiki zake eti waachane na mume wako au mpenzi wako, hapana hawataacha na kubwa kabisa watamuona jama ayako kama ‘fala’ flani ambaye huendeshwa endeswa na mwanamke.
Watamuambia na mbaya zaidi kwakua kweli anaendeshwa endeshwa na marafiki atajaribu kufanya kinyuma na mambo unayoyataka ili tu kuwaonyesha marafiki zake kuwa humuendeshi. Ndiyo maana kila siku unaongea, kila siku unalalamika lakini haachi anchokifanya, anazidisha dharau na haachani na hao marafiki. Mwanaume wa namna hii hutakiwi kumuambia bali wewe kueweka malengo ya familia.
Kwa mfano kama unaona pesa yake yote anamalizia kwenye pombe na washikaji, badala ya kumuambia kuachanana nao basi unaanza kumuweke amalengo, unajua naapata kiasi falani hembu weka malengo ya kimaendeleo ambayo unaona anaweza kuyafikia. Mfano unajua anapata hela siku falni, mpeleke kuangalia viwanja, mna kiwanja anapata hela ongea kuhusu kupeleka mawe.
Hapa nikimaanisha kuwa badala ya kelele zako kuwa sitaki nikuone na flani, sitaki hiki na kile wewe kelele ziwe nataka tufanye hiki, nataka hiki na kile. Baada ya muda ataona namna unavyomsukuma vizuri, ataona namna mabavyo wewe ni jembe na kuona ubora wako zaidi ya marafiki. Lakini si atakua hana hela hata kwa marafiki atakua anaboa. Ndiyo dada yangu unaweza kucheza na akili za mwanaume bila kumfanya aone umemtawala
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU