Wengi wanaingia katika ndoa siku hizi ili mradi tu jamii iwaone nao wameolewa au wameoa wamesahau kua ndoa ni Taasisi nyeti ambayo mbali na kuiingia kimazoea bali yahitaji maandalizi ya kutosha kuhusu namna ya kuishi na mme au mke, mahitaji yake makuu na namna ya kuyatimiza ili kuepusha hatari ya usaliti.
Ndoa nyingi miaka hii huingia katika matatizo makubwa na migogoro isiyo ya lazima sababu kuu imekua mke au mme kutoridhishwa na huduma ndani ya ndoa.
Leo napenda niongelee kwa ufupi mahitaji makuu ya MUME ndani ya ndoa ambayo mke anapaswa kuyatimiza ili kuhakikisha mme wake anatulia na kuienzi ndoa. Mahitaji hayo ni kama ifuatavyo:
1. Anahitaji kutoshelezwa ktk tendo la ndoa, (kushiba), kama unatumia sex kama adhabu na unavigezo na masharti kibao, huu muziki utakuwia mgumu.
2. Anakiu ya kula chakula cha mkewe (hata kama uko bize kama shetani, basi jitahidi hata mara chache basi)
3. Kuna baadhi ya shuhuli hapendi kuona dada wa kazi anazifanya bali wewe, sio kwamba anataka akutumikishe, la hasha, anajisikia furaha kuwa served na mke wake. (Najua pia uko bize but you can do something)
4. Anataka kuona unavutia, sio kwasababu ameshakuoa basi unajiachia tu, huyo sio kakako, anahitaji kuvutiwa kingono, be sexy, hata kama unanyonyesha, jiweke atractive. (Sasa hapa pia mwanaume usiwe bahili kwenye kugharamia)
5. Anakiu ya kuiona heshima kutoka kwako, ukianza kuleta ushindani, majibizano na kusaka usawa itakula kwako mazima (hata kama mama yako alikuwa anafanya hivyo kwa baba yako)
6. Hata kama uwezo wake ni mdogo kuliko wewe, appreciate kile kidogo anachokiweza au anachokifanya
KUMBUKA
Mahitaji hayo ni kwa mwanaume anayejitambua tu, mwenye hofu ya Mungu, aliefunzwa na wazazi na mwenye utu na adabu ILA mwanaume muhuni, kimeo, mchafu wa tabia, mwenye pepo la ngono na umalaya hata umfanyie yote hayo na mengine 1000 bado hataridhika na vya ndani ya ndoa maana tabia yake ndio ULEVI wake hakika cha kumuokoa ni neema ya Mungu pekee hivyo maombi yako itabidi utilie mkazo kumuomba Mungu akuokolee jahazi.
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda