-->

WANAWAKEEE!!! LEO MTANISAMEHE NGOJA NIWAPE MAKAVU LIVE

Image may contain: one or more people
LEO MAMA ZANGU MTANISAMEHE! Lakini ni jambo jema kuwashauri wanawake wenzenu wenye tabia kama hizo, Nimekutana na Mwanaume analia na nilipo muuliza unalilia nini? Kwakweli majibu yake yalinipa simanzi moyoni "NDUGU YANGU USIOMBE UKUTANE NA MWANAMKE MUONGO INAUMA SANA" Pole sana kaka, hebu niambie linalokusibu pengine naweza kushare nawe japo mawazo, Asante kaka kwanza niseme MAPENZI TATIZO LAKE KUMZOEA MTU NA AKITAKA KUONDOKA AMA WEWE KUONDOKA HAPO NDIPO PALIPO NA SHIDA... Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye nilimpa kila kitu, nimeshiriki nae dhiki lakini pia kwenye faraja tumekuwa pamoja, Kwa bahati mbaya sana Mwenzangu amezaa mtoto mmoja na kwa maelezo yake anaishi peke yake japo baba wa mtoto yupo ila hawana mawasiliano kwani dada huyo anamhudumia mtoto wake na anajimudu, shida imekuja wapi ndugu yangu? Mimi napambana kumjenga ki akili, ki mwili, hata kwa moyo ili mwenzangu aweze kusahau mapito aliyopitia lakini akiwasiliana na mzazi mwenzie anafuta juhudi zangu zote, Yaani kila ninapojaribu kutaka kuondoka ananisihi nisiondoke bali nimngojee akifanya mipango ya kuachana na mzazi mwenzie, Ndugu yangu naugulia MOYO Sina Amani wala sisikii furaha kabisa, Tumaini limeniondoka nabaki kulia na kukondeana bila majibu ya nini nifanye, Kwa ufupi ni hayo tu.
Pole sana rafiki yangu, Mimi naitwa Elista kazi yangu KUWAPA MATUMAINI WAHANGA WA MAPENZI... Nimekusikiliza na kuvaa viatu vyako kwa hakika siwezi KUJARIBISHA maana nami yaliwahi nikuta hayo lakini nilipopona nikainuka na kusonga mbele, Je unajua USALAMA WAKO NI MAISHA? Je unajua AFYA YAKO NI MAISHA? Hayo yote yako kwenye uwezo wa akili na moyo wako, Ni kweli unampenda na pengine anakupenda MBONA WEWE UMEMPA UHURU KULIKO YEYE? Huyo mwanamke atakuwa anampenda mzazi mwenzie ila wewe amekufanya "TULIZO LA STRESS ZAKE" Yaani upo kuituliza akili yake iweze ku-relax ndo maana anaporudiwa na huyo mzazi mwenzie anakusahau maana UPENDO WAKE UPO KULE na kama unabisha jikumbushe nyakati ambazo hawako Sawa na mzazi mwenzie kwako anakuaje? Pole sana ila unawajibika kuachana na mawazo mgando eti huwezi kuishi bila yeye, Mwenzio analo tatizo dogo sana nalo ni "ANACHUKIA TABIA ZA MZAZI MWENZIE BUT STILL ANAMPENDA AWE NAE MAISHANI MWAKE" Baada ya kusema hayo JITAFAKARI SANA NA UJUE WAPI UMETOKA NA UNAKWENDA WAPI ni rahisi tu, Yabebe akilini yanayokuumiza na uweze kupata maamuzi sahihi.

Ujumbe huu UNANIFUNDISHA NINI?
Iko tabia fulani kwa baadhi ya wanawake kuwaweka wanaume kama SPARE Yaani yuko na mtu "MUME/MZAZI MWENZIE lakini anamsumbua mpaka anafikia wakati wa kutafuta mtu mwingine, na anampata na wanayaanza mahusiano baadaye yule mtu wa mwanzo "MUME/MZAZI MWENZIE" akipenyeza neno la msamaha anakosa msimamo mwisho wake ni kuumiza upande wa pili, Yamewakuta wanaume wengi sana, Unakuta Mwanamke amezalishwa ama aliolewa na mwanaume lakini ndoa yao ikaingia migogoro sasa huyo Mwanamke anatafuta mahala pa kupozea stress zake bila kujua mtu huyo atajiachia na kuamini ni wake kumbe kipo kikwazo, Wanawake chukueni maamuzi kwa mambo yenu msiwaingize wanaume wasokuwa na hatia kwenye mateso na wakati mkijua PENDO LAKO LIKO KWINGINE! Hilo ndilo linawapa jina baya la "MALAYA" kumbe ni vile umekosa kuchagua vyema ama kuchukuwa maamuzi sahihi, Niwaombe sana mkae mkijua KILA TESO ANAPITIA MWANAUME AMBAYE ANAKUPENDA KWA DHATI NA UMEUMIZA MOYO WAKE MALIPO YAKO MBELE YAKO na usije lalamika wakati utakuwa unapigwa dana dana kama mpira wa mazoezini Kwani hapo ndo utakuwa UNAKINYWA KIKOMBE  chako, Malipo ni hapa hapa DUNIANI ili tukifa KITABU 📙 CHAKO KIFUNGWE.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria👊🏿
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU