-->

#USHAURI: JE! UMETOKA KUACHANA NA UMPENDAE NA UNAFIKIRIA KUINGIA KWENYE UHUSIANO MPYA??!!!...FAHAMU MAMBO HAYA

Image may contain: 1 person

Hakika moyo sio chuma, mengine yanauma. Ni maumivu makali zaidi ya msiba pale unapothibitisha kuwa unaempenda toka moyoni kwa dhati ameamua muachane, hakika hata akiwa na sababu hutozielewa maana unakuta kwa namna mlivyokuwa mnapendana ulishaamini cha kuwatenganisha ni kifo tu.
Maisha ndivyo yalivyo, waeza mpenda mtu na kumpa dhamana ya moyo wako wote ila kumbe mwenzio moyo wake kashampa mtu mwingine, mwishowe mnaachana hapo ndipo wewe uliependa kweli utapoisoma namba wakati yeye atabaki na tabasamu kwa kuwa wala hata haukuwa moyoni mwake kama ulivyokua ukifikiri, ulijua umepata kumbe umepatikana, hupendwi kwa dhati, ulikua wa kuzugia tu. Ikitokea uhusiano huo umevunjika na mkaaachana usijute wala kusikitika bali chukua nafasi jipe mda Tafakari ujiridhishe nini chanzo na mwelekeo mpya wa barabara usijeangusha gari tena.
Si lazima uwe kwenye uhusiano muda wote, ukiona mambo hayajakaa vizuri usiyalazimishe.

Kabla haujaanza uhusiano mwingine, ebu JIULIZE ni kitu gani umejifunza Katika uhusiano wako uliopita.

Kuna msemo usemao KUJUA chanzo cha tatizo ni Nusu ya KUTATUA Tatizo, Je umefahamu tatizo lilofanya uhusiano wako wa 1, 2 na 3 kuvunjika? Ulishawahi kukaa chini kujiuliza? Ulipata majibu gani?

1) Usiingie kwenye uhusiano mpya haraka haraka kabla haujapona MAJERAHA ya uhusiano uliopita, Kujipa muda kuwa peke yako ni TIBA tosha.

2) Usiingie kwenye uhusiano mpya haraka haraka ili kumkomoa X wako, Isije ukajikomoa mwenyewe.

3)Usiingie kwenye uhusiano mpya haraka haraka ili kupoza moyo wako isije ukawa unazidisha Kidonda,

4)Usiingie kwenye uhusiano mpya ili kuondoa upweke, isije ukauzidisha huo upweke.

5)Usiingie kwenye uhusiano mpya haraka haraka ukitegemea kumpata mtu BORA kuliko X wako, isije ukawa unaruka Mkojo, unakanyaga.........?

FUNZO:
Usiwe kama Nyani kuruka-ruka kwenye miti, mara tawi hili, mara tawi lile. Lakin pamoja na uhodari wote wa Nyani wa kuruka kwenye miti lakini kama siku ya KUFA imefika, miti yote HUTELEZA.

SI LAZIMA MUDA WOTE UWE KWENYE UHUSIANO, JIPE MUDA KUWA PEKE YAKO, CHUKUA LIKIZO YA MAPENZI.

Mara nyingi "MOYO ULIOJERUHIWA, HUJERUHI, MOYO ULIOPENDWA HUPENDA "

#kumbuka
UKIANZA NA MUNGU UTAMALIZA NA MUNGU

Kabla hujaingia katika uhusiano au ndoa mtangulize Mungu akuepushie kunasa tundu bovu.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU