Kuna mambo mengi mazuri aliyokua akikufanyia X wako, kwamba pamoja na kuachana lakini kuna vitu unavipenda, lakini kuna mabaya ambayo alikua akikufanyia X wako na labda ndiyo sababu ya kuachana. Acha kumlinganisha huyu wa sasa na yule wa zamani, muache akufanyia mazuri yake na wakati huohuo mhukumu kwa mabaya yake. Hakuna kitu ambacho kinaboa katika mapenzi kama uko na mtu halafu anamtaja X wake.
Flani alikua anapika vizuri, falani alikua anajua kufua, flani alikua ananihudumia, flani alikua anampenda Mama yangu, flani hivi flani vile. Hata katika mambo mabaya, hata kama hufanya yaleyale lakini mhukumu kwa mabaya yake si kwa kumlinganisha na X wako, inaboa kama kila siku atasikia unanifanyia kama flani, hata flani alianza kama wewe, wanaume wote mko hivyo, sijui hivi na vile, wanawake mwalimu wenu mmoja, mwenzo alikua mvivu kama wewe.
Kwa kufanya hivyo hata kama ni kwa nia nzuri, ni kama unamkumbusha mwenza wako kuwa sijamsahau X wangu iwe unamsifia au unamrtukana lakini kama hatoki mdomoni kwao basi hujamsahau na kama ni mimi nakuambia ondoka kakae naye ukimsahau basi njoo kwangu sifia mazuri, omba kile unachoomba kama una shida, lalamika kama anakufanyia mabaya lakini kamwe usimtaje tena X wako, ni dalili kua hujamsahau hata kama unamtaja kwa kumuombea agongwe na gari au aote majipu ya makwapa!