-->

TATIZO SIO KWAMBA HUTONGOZWI NA VIJANA BALI HUJUI TONGOZA YA VIJANA!

Na Idd makengo
Juzi nilikua naongea na dada mmoja, akaniambia kua yeye anatamani kuolewa lakini kila mwanaume anayemtongoza ni mume wa mtu, hajawahi kutongozwa na vijana au vinaja wakija kwake basi hua hawako siriasi wanataka kumtumia tu. Kwanza nilicheka kidogo lakini nilimuambia tatizo lake si kwamba hatongozwi na vijana bali amekua akitembea na wazee kiasi kwamba hajui au kashasahau kua vijana wanatongozaje.
Labda nifafanue kidogo kwani najua mko wengi hapa mnasoma, una kamzee kako unajipa moyo kanakupenda bila kujua kua baada ya miaka mitano kuna mawili, kwanza inawezekana utakua bado uko naye unatamani ndoa au mtoto lakini yeye anakukwepa au jambo la pili nikua ashakuzalisha ukidhani atahudumia mtoto ila kashakutelekeza karubi kwa mkewe au kaenda kutafuta binti mwingine mbichi kama wewe ulivyosasa.
Iko hivi, utongozaji wa mume wa mtu ni tofauti na kijana, najua mnajiambia ooohhh wazee wanajali, wanadekeza, sijui nini na nini? Ni kweli lakini si kwakua wanajua kupenda bali nikwakua wanajua ndiyo kadi pekee ya kucheza, wasipojali sasa watakupa nini cha maana. Mbali na ufundi kitandani ambao mara nyingi unapatikana kwa vijana, ili mwanaume kumdthibiti mwanamke na kumlazimisha kukupenda kuna mambo mawili.
Jambo la kwanza ni utoe pesa, daa mwanamke ukimpa pesa hata kama sura yako ni kama nyama ya goti ni ngumu sana kukuacha maana unavumilika, ukamdekeza kidogo basi unavumilika. Lakini jambo la pili ni umpe matumaini ya ndoa, hapa mwanamke hasa wale ambao washakua watu wazima achana na vitoto vya shule hawa bwana akiwa na mwanaume ambaye anaona kua huyu anaweza kunioa, hata kama hanipi pesa lakini angalau anaweza kuwa mume.
Hapo mwanamke atavumilia kidogo. Sasa kijana ana hii kadi ya pili, kwamba hawezi kujali sana au kutoa pesa sana kwani anajua kua utamkubali na kumnyenyekea kwakua unawaza ndoa, mzee anajua kua unajua ana mke hivyo suala la ndoa halipo kazi yake kubwa itakua ni kutoa pesa na kukudekeza ili usichomoke. Sasa kama wewe unatembea na mume wa mtu na hela hakupi basi wewe ni FALA tu! Unahitaji maombi, unahitaji maombi zaidi kama unaamini kua atamuacha mkewe kwaajili yako.
Unahitaji maombi zaidi kama unaamini kua eti anajali sana, unachekesha hvi huoni kua kamtelekeza mke wake kaja kwako halafu bado unajiambia “Waume za watu wanajali, wanajua kupenda!” Nikisikia binti anasema hivyo natamani nimuone ndiyo katoka kujifungua mimba ya huyo mume wa mtu na hapokei simu zake tena kwakua kashakua kama mkewe ana elekea kwa binti mwingine mbichiii!
Nirudi kwenye mada kuwa, wanawake ambao washazoea kutembea na waume za watu basi wakitongozwa kizee hudhani huo ndiyo utongozaji wenyewe, wanadhani kua ni kazi ya wanaume kuwalaipia kodi ya nyumba, kuwanunulia Iphone X na kuwapeleka Hoteli za nyota tano. Kwakua hakuna kijana mwenye akili timamua anafanya huo ujinga basi hudhani kua vijana hawako siriasi na kujikuta wanavutia wazee tu hivyo kuishia kusema “Vijana hawanitongozi!”
Dada yangu wewe ni sawa na mtu aliyezoea kuvaa viatu virefu akivaa flat hajisikiia kama amevaa kiatu, si kwamba vifupi ni vibaya hapana ni mazoea tu. Najua ushazoea vihelahela lakini kuna umri inabidi uachane na hao wazee na kuwa siriasi na maisha, ukiendelea nao itafikia hatua unakata tamaa kua wewe si wakuolewa kumbe umejifunga kwa vibabu. Hivyo vihelahela vyote vitatoweka ukibeba mimba ya huyo mzee au na wewe ukishakua mhenga hutawaona tena na vijana ndiyo hata kuwasikia hutawasikia.
Image may contain: 2 people, people standing and outdoor
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU