-->

MREJESHO; NISAIDIENI NIFANYE NINI NIMEKUA MCHEPUKO WA MUME!

Close up studio face shot of charming young african girl with braided hairstyle. Stock Photo - 79224056
“Nimkuambia kuwa huyo mwanaume huwezi kumuacha, kubali kulea huyo mtoto basi maisha ya endelee, kwa hatua mliyofikia mume wako hawezi kumrudisha huyo mtoto kwa Mama yake, ni kweli alichepuka lakini umemsamahe, mtoto kashazaliwa mkubali. Hata kama ni mimi, kwa unavyosema nisingeweza kumrudisha mtoto kwa Mama yake, hapana, huyo mwanamke ni mshenzi anaweza kumuua mtoto kwaajili ya kumkomoa mwanamke, mchukue mtoto mlee kama wako basi!” Nilimuambia mteja wangu mmoja mwaka 2017.
“Hivi kwanini wanaume mnateteana sana, yaani wewe hembu vaa viatu vyangu, ingekua ni wewe mke wako kaenda kuzaa huko akakuletea mtoto ungekubali kulea!” Ananijibu kwa hasira.
“Hapana, nisikudanganye mimi sina huo moyo, achana na kulea mtoto ila nisingemsamehe hata yeye, ila kama nikimsamehe nisingemhukumu mtoto, kwamba nisingeacha mtoto wake ateseke kisa mke alinifanyia kosa. Lakini huyo ni mimi, ili nikushauri vizuri sitakiwa kuvaa viatu vyako kwani nitatumia moyo na si akili. Wewe sasa hivi unatumia moyo, moyo umeumizwa, ila mimi sijaumizwa, natumia akili.
Kwa unavyoongea unampenda mume wako, mna watoto wawili, huwezi kumuacha mume wako, najua unasema unaweza ila kumbuka unaongea na Iddi Makengo. Yaani kwa sauiti yako tu nakuambia wewe dada, hata mume wako akichepuka mbele yako utamsamehe, hata akikuletea watoto 10 utamsamehe, sasa hivi una hasira, tulia , mchukue mtoto kwani baada ya mwaka utaona ulifanya ujinga kama ukiondoka. Huyo mtoto anateswa na Mama yake, anatakiwa kuishi na Baba yake, hivyo kwakua wewe unasihi na Baba yake ni lazima uishi naye, acha kujidanganya kuwa utamuacha!”
“Hapana, mimi siwezi kuishi na mtoto wa mtu, uamuzi ni wake, achague mimi au mtoto, kamaa kichagua mtoto basi naondoka, mimi nina kazi yangu, nina wanangu nitalea mwenyewe na ndugu zangu wapo wana uwezo hata asipohudumia wtanisaidia!”
“Sawa, uamuzi ni wako, ila ushauri wangu leo, kesho, mwakani mpaka miaka 100 ijayo nikuwa usiondoke, si kwakua mume kafanya kitu kizuri, hapana, nikwakua bado unampenda, kaomba msamaha na kajuitia, umemsamehe na mtoto ni Baraka si kosa, najua unawaza atakuletea na wengine na wengine ila mwisho wa siku huwezi kuishi kwa hofu, shida yangu si wewe kumuacha bali shida yangu nikwakua najua utamuacha na utamrudia, nina uhakika asilimia 100 kuwa ukimuacha huyo mwanaume utakuja kumrudia sasa kwanini kuleta usumbufu na kisirani tu….”
“Nashukuru kaka uwe na siku njema, ila nishafanya maamuazi yangu.” Alikata simu, hakusubiri hata nimalizie, ila nilijua kuwa atakuja kunitafuta tena kwani si mtu wa kuacha, ana hasira na anaendeshwa na mashoga zake, nilijua kuwa hataki kuondoka ila anataka mwanaume amuambie basi namrudisha mtoto kwa mama yake sisi tubaki, lakini Mama wa mtoto alikua anampiga mtoto, hampeleki shule, anamnyima chakula ili tu kumuumiza mwanaume kwakua alimdanganya atamuacha mkewe amuoe ndiyo akabeba mimba hivyo analipa kisasi, mwanaume mwenye akili hawezi kumuacha mwanae kwa mwanamke kama huyo.
Miaka miwili baadaye huyu dada alinitafuta, aliacha kusikiliza ushauri wangu, akaamua kuondoka, kumbe kuna nyumba alikua anajenha kimya kimya bila kumuambia mume wake. Aliimalziia akachukua watoto akaondoka, akamuacha mume wake na mtoto, mume aliomba msamaha, wakaita ndugu ikashindikana, basi jamaa akamua kutafuta binti wa kazi, akabaki na mtoto wake, wale wengine akawa anahudumia tu kwakua mwanamke aliwang’ang’ania.
Baada ya miezi sita hivi mwanaume bado alikua anaomba msamaha, lakini mwanamke aligoma kumsamehe, akamuambia kuwa amuondoe mtoto ndiyo arudi, ila wakati huo huo mwanamke alianzisha mahusiano. Ndiyo alianzisha mahusiano na Bosi wake ambaye ni mume wa mtu, yaani akaondoka kutoka kuwa mke, akamuacha mume wake kwasababu ya kuzaa nnje ya ndoa eti akaenda kuwa mchepuko wa mwanaume ambaye ana watoto watano, Baba mtu mzima, baada ya kumpata huyo mwanaume basi alidai talaka, mume alipochunguza akajua mkewe kaanza mahusiano mengine akampa talaka.
“Kaka baada ya mume wangu kunipa talaka nikawa hutu basi nilijikuta naanza kumuonea wivu Bosi wangu, mwanzo nilikua namtumia kama kiburudisho ial nikaanza kumpenda nikawa naona wibvu akinichanganya na wanawake wengine. Tukawa tunagombana, ikaleta shida ofisini mpaka mimi nikahamishiwa wilaya nyingine kwani Bosi aliona kama nataka kumharibia kazi. Maisha yaliendelea, mume wangu aliendelea kuhudumia watoto na mimi nikawa niko peke yangu, kwakua alinipa talaka moja nilijua kua atakuja kunirudia tu.
Kusema kweli kukaa mbali na kutokua na mtu kulinifanya kumkumbuka sana mume wangu, nilijikuta natamanai aniombe msamaha ili nimsamehe lakini haikua hivyo. Sikumoja niliamua kwenda kwake, nilitaka kuwatumia watoto ili kumrudisha, wakati wote yeye akitaka kuwaona watoto ndiyo alikua anakuja, wakati tunaachana hatkua na nyumba, tulikua tumepanga mimi ndiyo nilikua najenga kivyangu ila baada ya kuachana alijenga na kuwa na kwake, nilikua napafahamu hivyo siku moja nilifunga safari na wanangu kuwapeleka.
Nilifika wakati wa jioni makusudi ili tu nichelewa hata anitake nilale ili turudiane, nilifika lakin sikumkuta, nilifunguliwa na Binti wa kazi, hakua akinifahamu bali alikua akwafahamu watoto kwani walishawahi kwenda. Nilijitambulisha, niliposema kuwa mimi ni Mama wa wale watoto alishtuka, mwanzo alsihanikaribisha ndani lakini baada ya kusikia hivyo aliniambia nisubiri. Aliingia ndani lakini hakutoka, alitoka mwanamke ambaye alikua kaza naye, tulikua hatujawahi kuonana lakini nilikumbuka picha zake ambazo alikua akituma status mara kwa mara.
“Unafanya nini hapa?” Nilijikuta nashikwa na wivu na kumuuliza kwani niliona kama nkaniingilia kwangu.
“Aliniangalia kwa dharau kisha akanionyesha kidole chake.
“Nimeolewa Bibi, hivi hujaambiwa, nimepanda cheo sasa hivi mimi ni mke, hivyo kama ni watoto waache mimi ntalea tu ila wewe ondoka…” Alianza kuniongelesha maneno ya dharau, tukagombana na kuanza kutukanana kidogo tupigane gari ya mume wangu iliingia.
“Huyu ni nani na anafanya nini nyumbani kwangu?” Nilimuuliza kwa hasiara baada tu ya kushuka, lakini kistaarabu kabisa aliniambia kuwa yule ni mke wake, wamefunga ndoa na wana miezi miwili sasa hivyo mimi niondoke na kama ni watoto basi atakuja kuwachukua akitaka na kama nataka kuwaacha pale siku ile basi niwaache moja kwa moja.
“Ndiyo uwaache mimi nipo tayari kuwalea hawa watoto kama wangu!” aliniambia, pozi ililiniishia nikawachukua wanangu nikaondoka, sikua hata na nguvu za kubishana anaye. Nilienda na wanangu kutafuta nyumba ya kulala, kesho yake asubuhi mume wangu alinipigia simu, alikua anaomba msamaha.
“Nilipaswa kukuambia kuwa nimeoa, sikufanya sawa, nimekuaibisha, naomba nisamehe nataka kuwaona watoto mimi ndiyo nilikukosea ulikua na haki ya kuondoka naomba unisamehe.”
Aliongea sana na kuniuliza niko wapi, kwa naman alivyoomba msamaha sikua na namna, nilimsamehe na kumuambia nilipo, tuliongea siku hiyo, akazunguka na watoto, nilikaa siku mbili nikarudi. Baada ya hapo akawa ni mtu wa kunipigia simu, mtu wa kunijali tena, mara tukajikuta tunaingia kwenye mahusiano upya. Nimeingia naye kwenye mahusiano lakini mke wake wa sasa hajui, nikimuambia amuambie kuwa tumerudiana ananiambia hapana, hawezi kurudiana na mimi tuendelee hivi hivi.
“Mimi sitaki kufichwa fichwa, utaishije na mwanamke ambaye humpendi?” Mara nyingi namuuliza lakini jibu lake nikuwa nimheshimu kwani ni mke wake na hawezi kuachana naye./
“Nitaonekana mjinga kama nikiwa mtu wa kaucha na kurudia, kwahiyo unataka nimuache tena yule mke wangu nikurudie wewe unafikiri watu watanielewake?
“Lakini mimi nilishakua mke wako, ulinipa talaka moja tu, unaweza kunirudia, kumbuka tuna watoto?” Namuambia lakini hakubali, yaani nashindwa hata nifanye nini, nampenda na natamani wanangu kulelewa na Baba yao, lakini sasa hivi najiona kama mchepko wake.
Nikipiga simu kama yuko na huyo mwanamke hapokei, huyo mwanamke anamsumbua sana, najua ananipenda mimi na mimi nampenda ila nashindwa nifanye nini nirudiane naye. ulikua sawa Kaka kuniambia kuwa siwezi kumuacha mume wangu, ni kweli nilikua siwezi kwani niliondoka ili aniombe msamaha na kunichagua mimi lakini bado aliendelea kuishi na mtoto wake. Kaka nipo tayari kumlea mtoto wake, sitaki tena kuwa mchepuko, nisaidie nifanye nini?”
“Kwanza pole, najua ulifanya maamuzi kihisia ila nikuambie tena huyo mwanaume hakurudii, kubali umeshaachwa, wewe ni single mother, acha kujidhalilsha kwa kuwa mchepuko wa mume wako, maji ulishamwaga hayazoleki, kubali matukeo maisha yaendelee la sivyo utaendelea kuwa mchepuko wa kudumu ila hakuna ndoa tena hapo.”
MWISHO
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU